You left me but remember


Kuna vitu vingine katika maisha hutokea,ambavyo hatupendi vitokee, na once vitokeapo hutuachia majonzi sana na majereha yasiyosahaulika moyoni...

Ni msichana tuliyekutana naye wakati yeye akisubiri matokeo ya kidato cha sita,meanwhile nilikuwa dissappointed na Lilian Girlfriend wangu wa kwanza whom aliamua alibadilika kutokana na makundi almaaruf kampani, nikajaribu kumbadili sana ikiwa ni pamoja na mimi kujibadili ili walau tuendane but akili ya bi dada huyu huwa inachange often,nikaamua kukaa kimya na kuachia ngazi....

Tokea hapo nikawa muda mwingi ambao siko kazini naumalizia kwenye novel na wakati mwingine nikawa mhudhuriaji mzuri sana kwenye viti virefu ambako kwa kiwango kikubwa kuliniwezesha kusahau maswahibu yangu kwa Lily...Kisha ikaja hii siku ambayo siwezi kuisahau...

Alikuwa anaolewa Vai, binamu yangu,kwa kuwa ilikuwa ni mwishoni mwa mwaka tukaona as family ni busara kutumia nafasi hiyo kukutana pamoja na kufahamiana kwa kuwa kutokana na pilika za kutafuta maisha tulikuwa scattered sana. Ni siku moja kabla ya send off nilipojiamulia kwenda kusabahi marafiki zangu waliokuwa wanaishi mji wa pili kwenye mkoa wangu...

Nikiwa stend ya mabasi najisomea kitabu cha Dale Carnegie ( how u can win friends and influence people) wakati huo huo nikiwa kwenye dala dala kwa mbali namwona binti mmoja matata sana ambaye kwa sala za papo kwa hapo nilikuwa naomba awe anaelekea safari moja na mimi,ukweli ukawa hivyo...

Akaingia kwenye gari nililokuwa nimepanda na kikubwa zaidi akaja kwenye seat nearby,alinisabahi huku akiachia tabasamu lililomeza umakini wangu kwa sec kadhaa kisha nikapunga mkono pasi kusema neno,punde safari ikaanza huku nikijititahidi kusoma kitabu changu of which niliacha baadaye baada ya kugundua kwamba mstari niliokuwa napitia baada ya kumwona mgeni huyu ndio huo huo nilikuwa narudia rudia though kuna kitambo kilishapita!

Mtoto wa kiume nikaamua kujilipua kwa kuanzisha mazungumzo ambayo hata hivyo sikuwa na uhakika sana kama ningepata ushirikiano kutoka upande wa pili,ila haikuwa hivyo,tuliongea mawili matatu concern maisha na kufahamiana japo kwa uchache. Ni hapo nilipogundua kwamba alikuwa amehitimu kidato cha sita na alikuwa anasubiri matokeo ili aweze kuendelea na elimu ya juu.

Kwa kuwa alikwisha nieleza kwamba safari yake ingeishia wapi na kwa kuwa mimi ningeishia midway nikaomba kama asingejali tubadilishane # of which hakusita akanipa no nami nikampa yangu! Tokea hapo ikawa ni mwanzo wa kuwasiliana na kutakiana moment njema njema...Kadiri muda ulivyoenda tukajikuta tumevuka urafiki na tayari tukaanzisha mahusiano rasmi...

Matokeo yalipotoka akachaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dodoma huku mahusiano yetu yakipamba moto,vilikizo vidogo vidogo vyoote kipindi chote cha masomo nilivitunza,na wakati mwingine hata ikibidi nilikuwa nakoroga kazini kwa kuzingizia kifo cha mtu immaginary ama alokwisha kufariki miaka mingi ili niende Dom ama yeye aje town (Dar) Dada zangu wakajua,mama akajua na baba akabidi niwe wazi bila shuruti na kwa upande mmoja tukawa tume officialize....

Yapo mengi ila frankly tumepita moments zote nzuri nzuri ambazo kwa mbali zinaendana na hizi tamdhilia za kikorea and likely,hakuwahi kuninunia muda wote niliokaa naye,hatukuwahi kupishana lugha,hakuna hata mmoja kati yetu aliyewahi kumtendea mwenzie hiyana na kila siku kwetu ilikuwa nzuri kuzidi jana yake...Nilimpenda sana Rose,nampenda though ameshapata mwingine!

Ni juzi niliamua kusum up vitu vingi vingi na kujumlisha hapa na pale baada ya kuona kuna badiliko katika mahusiano yetu na kuhisi kuna mdudu keshaingia ambapo kwa upole nilijaribu kutaka kiini cha kunyauka huko kwa pendo letu,ndipo aliponiambia ukweli wake wa moyoni,ambao kwangu ni mchungu na umeniachia majeraha ambayo sina hakika kama yatapona...

Aidha natambua kuna mabinti wazuri sana na kwamba kila kukicha wanazidi kuchomoza wazuri kuliko wa jana ila hakuna kama Rose wangu,aliyepata kunipenda,nikampenda,daima nitaheshimu mawazo yake na nitamwombea kwa Mungu dua njema ili upendo alioupata kwangu aupate kama huo ama zaidi kwenye mahusiano yake mengine aliyoyaanzisha ambapo jana alitambulishwa rasmi ukweni kwao kwa maana kinachofuata huenda ni engagement labda na ndoa!
 
Mbona mie mweusi kama wewe and i still blush? Muache banaa aombolezee maji yake yamemwagika.

Maadam kwa hawa hit and run inahitaji darasa pana sana kuwaeleza existence ya upendo wa kweli...
Wakati mwingine mnajikuta mnafanya craizy things pamoja unconsciously na hata kutoongea kwa muda mrefu ili hali mko pamoja na still mkawa na furaha tele mioyoni...
 

Maji tunayotumia kwenye kijiji chetu yanatumika kulishia mifugo kwenye kijiji jirani ambako ndipo kwenye chanzo,kanuni ya afya inanitaka nichemsha maji kwa matumizi ya kunywa, hivyo niliamua niyachemshe kwanza ili nisipate amoeba. Zoezi la kunywa sumu nimelisitisha kwa kuwa kuna marafiki zangu wengi wangekosa fursa ya kuniaga kwa kuwa tayari ilikuwa ni usiku mwingi..
 
......inauma hiyo! Dahhh.....pole sana bro, pick up your pieces, accept the fact and move on.

Hebu nitakie R.I.P kabisa mkuu maana muda si mrefu nitakuwa kwenye ulimwengu mwingine...halafu nisisahau,karibu msibani,kula,kunywa itakuwa juu yangu...
 
Hahahahaaaaa usiombe kuachwa!!!!! Mapenzi ya ujanani ni matamu balaa sawa na mke WA mtu au mume WA mtu......nilishakesha nalia usiku Mzima kwahio hata simlaumu kijana wangu. Take courage and move on......
 
Mapungufu niliyonayo aliyapenda tokea kwanza,ningebadilika ningeweza kumpoteza mapema so far ningeongeza/punguza ambacho hakukinote mwanzoni...sijalala hadi muda huu nasubiri maji ya kuchanganyia sumu yachemke nikoroge ninywe kabisa uuuw!

unachelewa mezea na mate usisubiri maji yachemkefanya fast unywesumu hiyo.
 
You will love again...don't you worry. Been there done that.

Pamoja na kuficha ficha mengi hapa JF na wakati mwingine tujijitengenezea wake feki kwa majina ya mama bhooke and likely, leo hii nina miaka ishirini na tisa,miezi minne na siku tano,najiuliza nitaanzia wapi tena kupenda...nawezana tena na ooh baby,ooh baby za kishule shule? Eventually no,vije nikimpata aliyekwisha kuwa kwenye mahusiano ni itakuwa ni mwendo wa kucompare siku zote? Maana however atafanya nitakuwa najaribu kulinganisha na alivyofanya Rose wangu kitu ambacho kitaweza kumkosesha raha then GF wangu mpya!
 

una haki ya ku2hwa kwa kingereza hiki kibovu
 
bado tu hujanywa sumu unatuchelewesha bana mi nishanunua ndizi tayari ujue ya pilau lako

Ngoja nikaoge na kupiga mswaki kwanza, kisha nipate na chai na spanish omlet kisha ningwe sumu, lakini kabla sijafa ngoja nikutahadharishe,angalia sana usije kunywa sumu kama mimi kwa sababu kama zangu kisha tukutane huko juu...nitakulima makwenzi ya kutosha!
 
Sometimes its better kupata stress za mapenzi kabla hujaoa na huna mtu wa kukutegemea kulikokuja kuzipata ukiwa una familia inayokutegemea hivyo kupoteza dira na kuwapotezea mwelekeo wanaokutegemea.
 
una haki ya ku2hwa kwa kingereza hiki kibovu

Usijali, kiingereza ni lugha ya kikoloni, na hata kiswahili ni mkusanyiko wa lugha za kibantu,hivyo Mwl Nyerere asingetuunganisha ningetumia lugha mama yangu!
 

That you will have to conciously work on wewe mwenyewe. Kabla hujampata jitahidi kusahau.

Good thing is, it is never late to fall in love even if you were 39 years four months n five days.

And you may be surprised kila unapojaribu kulinganisha huyu mpya anamzidi Rose kwa kila kitu. Utashangaa...and then you will realise, 'after every storm comes a calm' when you fall in love again. You will tell us..all the best bro.


PM Moderator,
Mentor.
 
Mapungufu niliyonayo aliyapenda tokea kwanza,ningebadilika ningeweza kumpoteza mapema so far ningeongeza/punguza ambacho hakukinote mwanzoni...sijalala hadi muda huu nasubiri maji ya kuchanganyia sumu yachemke nikoroge ninywe kabisa uuuw!

Pole mkuu, just accept that she is already on an open road long gone you can't have her back
 
Sometimes its better kupata stress za mapenzi kabla hujaoa na huna mtu wa kukutegemea kulikokuja kuzipata ukiwa una familia inayokutegemea hivyo kupoteza dira na kuwapotezea mwelekeo wanaokutegemea.

Brother nina mama yangu,ambaye hata nisipomuita mpendwa haibadilishi dhana kwamba nampenda sana, nina dada yangu Lightness ambaye nilimuahidi kusimama naye bega kwa bega na kwamba ningekuwa mtu wa mwisho kumchoka baada ya ulimwengu mzima kumkataa...

Namfahamu Mwenyezi Mungu,ambaye alitumia muda wake adhimu kunipa pumzi hii ya uzima,nina wadogo zangu mtaani ambao kwa namna moja ama ningingine nimekuwa roll model wao kwenye aspects tofauti tofauti, nina Rose wangu huyu ambaye pamoja na uamuzi aliouchukua nadhani ataumia sana akijua nimejidhuru kwa sababu yake,na kwa kuwa nilimwahidi kwamba nisingependa kushududia akidondosha chozi kwa sababu yangu...,

Sasa basi najaribu kureview nakala ya sababu zinazonifanya nifikirie kujiua,ili nijikatie rufaa mwenyewe kwenye mahakama ya rufani ya mapenzi kisha nafsi ikishinda moyo nisitishe uamuzi wa kujiua na kama itaonekana niliviolet vifungu vya sheria wakati wa uamuzi wa kuijiua basi Rose anihukumu kwa kunirudisha kwenye kifungo cha kumpenda maisha!
 

Naamini katika upendo, hata usiokuwa wa kimapenzi, naamini katika mshikamano,hasa yanapotupata makuu, naamini katika ushirika,kwa kuwa katika huo ndipo tunajua walio wetu..naamini katika kuheshimu hisia za watu,ndiyo maana hata mtu akiwa na crazily proposal naamini ameamua hivyo purposely, naamini katika marafiki na leo niadmire kwa moyo mkunjufu kuwa br Mentor uu rafiki mwema, kwa maana ya rafiki hasa! Bravo bro...kuna maisha baada ya mapenzi, kwa kuwa yalikuwepo pia kabla ya mapenzi!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…