You can change your Genetic code

Kwa mujibu wa Imani yake ni sawa
Na tukumbuke Imani ni dhahania yani aina uhalisia
 
According to Sadhguru. Unakubaliana naye??

Cc DR Mambo Jambo min -me


View attachment 2946839
Ndio, lakini sio kama tunavyoijua jenetikia

Badala ya kuchange genetics, utakachofanya ni kubadili EPIGENETICS.

Epigenetics ndugu yangu, tuifafanue kiasi:
EPI - Iliyo juu ya (above)
Genetics - Ndiyo vinasaba sasa
So epigenetics ni vilivyo juu ya vinasaba. Hivyo ni mipangilio inayoiongoza mipangilio ya msingi.

Yaani ni kwamba mazingira huongea na epigenes kuziomba ziongoze kufunga au kufungua genes fulani. So haiongei na mbwa inaongea na mwenye mbwa. Yule bossi kabisa sio mtunzaji wake tu (shamba boi -genetics)

Mfano issue ya unene. Inawezekana kila mmoja katika familia akawa na vinasaba vinavyopelekea unene.

Lakini mtoto A akaishi mazingira ambayo kimwili na kihisia hayajahitaji epigene iiite gene ya unene kufanya kazi. Hivyo anabakia mwembamba hata kama vinasaba vipo.

Ila mtoto B akaishi mazingira ambayo kimwili na kihisia yanamuhitaji anenepe, basi hapo ndipo epigene inapoiita gene ya unene ifanye kazi ya kumpatia unene anaouhitaji huyu mwamba.

Sasa sisi wanadamu kwa vipimo na macho ya nyama, tutamuona huyu mtu ni kama amecotroll gene zake kabisa. Alipohitaji unene akawa na gene za unene. Alipoacha kuhitaji paap! Zikapotea!!

Tafuna hiyo
 
Back
Top Bottom