Kweli kabisa.ila Unajua ukimjibu kwa kiswahili hata mnaweza kuendeleza mazungumzo akajua hata kwa nini humpendi yeye. Na ukamkataa kwa amani. Ila ukishamwambia MTU "your my type" hata nguvu ya kuendeleza maongezi unakuwa hamna
Muache maana sio sentensi nzuri kabisa.Tutaacha basi. ..
Hahaàa haya bana tena ulivyokuaga mwembamba enzi hizo wkt sasa hivi umejinenepea mwenyewe je ningejidai ww sio wa type yangu ?? kisa nawapenda wanene wakt wembamba wa leo ni wanene wa keshoAsante, waambie ndiyomaana we ulistuka mapema ukaamua uje kuzeekea kwangu, la sivyo ungezeekea kwenu![]()
Hahaha unatamani ardhi ipasuke au bahari itokee ikumezeKauli kama hii itamkwe na mtu anayejua kukunja midomo ikasindikizwa na kamsonyo kwa sauti ya juu tena kwenye kadamnasi.
Mzee mzima unajikuta Viatu vimekuwa vikubwa kma tairi za trekta kutembea huwezi tena mdomoni kama umewekewa supa glue
Macho unashindwa utazame juu au chini au umtazame yeye.
Duh inahitaji ujasiri.
Ulimfanya nini binti wa watu jamaniKuna binti, miaka hiyo nipo Advanced level na yeye akiwa Olevel alinijibu hivyo, nikaacha kumfuatilia tukawa na mawasiliano ya kawaida, alipomaliza Digrii yake akazidisha mawasiliano. Nilichomfanyia hadi Leo hanisahau. Majibu kama hayo huwa wanatoa mabinti wadogo.
Wanaume na wanawake, let's say umetongoza au unampenda mtu yeye akakujibu 'You are not my type' au ukasikia anamwambia mtu kuwa you are not his/her type utalipokea vipi?
Mimi ninavyojua mtu akisema wewe sio type yake anamaanisha wewe si aina ya mtu ambaye angependa kuwa naye, haimaanishi amekudharau, amekushusha na kukuona una hadhi ya chini kuliko yeye kama wengi tunavyofikiria.
Kwenye mapenzi kila mtu kipo anachopenda iwe ni katika mwonekano au personality kiujumla. Wapo wanaume wanapenda chubby girls, wengine wanapenda English figure, wapo watu wanapenda mtu mchangamfu, anayeweza kufanya acheke muda wote lakini wengine wanapenda makauzu, kuona jino lake mwaka mpya hadi mwaka mpya. Kwa hiyo akikutana na wewe upo kinyume cha hapo ni kwamba wewe si type yake.
Japo si busara kumchana mtu live kuwa 'wewe si type yangu' lakini haina haja ya kukasirika, kuumia na kujenga chuki ukisikia kitu kama hicho. Maana wengine wakiambiwa hivyo wanaanza kuchambua demu mwenyewe miguu yote ya kushoto, sura kama anaramba ndimu anawezaje kutamka maneno kama hayo? Relax, kunywa maji then tafuta wa kufanana na wewe, yupo mahali anakusubiri.
Pengine kilichomfanya Diana asikupende ndio hichohicho kitakachomfanya Mwajuma asilale kwaajili yako.
Thanks


Kuna binti, miaka hiyo nipo Advanced level na yeye akiwa Olevel alinijibu hivyo, nikaacha kumfuatilia tukawa na mawasiliano ya kawaida, alipomaliza Digrii yake akazidisha mawasiliano. Nilichomfanyia hadi Leo hanisahau. Majibu kama hayo huwa wanatoa mabinti wadogo.
Hahhhahhhahhaa..balaa..Muwe mnayasema hayo maneno kwa Kiswahili hatutachukia lakini yakija kwa Kimombo ni vita.
Hilo neno sio tatizo kuambiwa tatizo lipo pale unaambiwa huku unaangaliwa juu chini, chini juu na msonyo juu aiseee. Wakati mimi mwenyewe nilimfata kwa kupunguza mwanza nyegezi tu.
Ndukiiiii![]()


kama ulitaka kupunguza nyegezi huna haja ya kuumiaHahahahaHiyo jeuri nilikuwa nayo enzi zile za UB 40, siku hizi wa type yangu naona wanazidi kuwa wengi. Lakini nimeshikilia kwa Asprin
Kauli kama hii itamkwe na mtu anayejua kukunja midomo ikasindikizwa na kamsonyo kwa sauti ya juu tena kwenye kadamnasi.
Mzee mzima unajikuta Viatu vimekuwa vikubwa kma tairi za trekta kutembea huwezi tena mdomoni kama umewekewa supa glue
Macho unashindwa utazame juu au chini au umtazame yeye.
Duh inahitaji ujasiri.
Ni kweli blaki woman hata mimi nimesema kwamba si busara kumtamkia mtu hivyo lakini yapo na yanatamkwa, unaweza usitamke wewe ila ukatamkiwaKwani kuna haja ya kumweleza hayo maneno maisha yanazunguka kuna siku atakuwa type yako huwezi jua maisha haya. Kama humtaki mtu tumia neno la busara achana naye. Kwa mtazamo wangu