You are not from around,are you? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

You are not from around,are you?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Diana-DaboDiff, May 20, 2010.

 1. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  why do people especially foreigners assume anybody speaking good English is not a Tanzanian? i have come accross this several times,how many of you here have also been asked this odd question?
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  may inglish is bedy...so they won't even bother to ask me!

  On a serious note, inapokuja suala la kiingereza watanzania wengi bado tuna matatizo makubwa. Naona sasa kuna msukumo wa kurudisha matumizi kiswahili katika ofisi na taasisi za umma...labda tunaweza kufanikiwa....maana kwa sasa kiswahili nacho bado kinatupa shida.Tuliobahatika kwenda shule kidogo ndo hivyo tena tunatumia 'kiwanglish'.
   
 3. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ahhhh kumbe sio peke yangu... what a relief :target: hivi kiswahili kwanini kigumu?
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Tatizo lako huwazungumshi Kiswahili cha kutosha.Ukiwazungumzisha Kiswahili cha nguvu na kuwafanya wafunue kamusi zao hawatakuuliza ujinga ujinga huu.
   
 5. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Kuna baadhi yenu munaona sifa kuzungumza kiingereza chenye accent ya kimarekani, kama wale waigizaji wa kinijeria wanaojidai kuzungumza hivyo siku hizi. Ndio maana munaulizwa hivyo.

  Aaaaaagh munaniboa kweli!
   
 6. JM Aristotle

  JM Aristotle Senior Member

  #6
  May 23, 2010
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I have already been faced with such a circumstance...
  The problem is; they are used to hearing our broken-English... but when someone stands up and beat them at their game, they tend to think it's not a Tanzanian...
  Ukweli ni kwamba; tunaweza... We only need practice...
   
 7. JM Aristotle

  JM Aristotle Senior Member

  #7
  May 23, 2010
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fine! nakubaliana na wewe kuwa kuna watu, wanaopenda kujifanyisha, kwa kuongea, "American slang/ ghetto-talk", na si, "American English"...
  American English ni nzuri tu na wala haina shida... Shida ipo kwa wale wanaoiga "American slang", ambayo hutokana na black-Americans...
  Shida nyingine ni kwamba; wabongo wengi tunashikwa na wivu tunapoona wenzetu wanaongea kingereza kizuri, na tunasingizia kwamba; eti tunaboreka...
  Fanya vizuri! na wewe utasifiwa...
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Give it straight to their face.....simple but real! Kakague thanks juu mkuu!
   
 9. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Beat them!!! teh teh teh ..... So u nw think u beat them...Hii inachekesha sana yaani .......
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,199
  Trophy Points: 280
  Kwanza kabisa, kama wengine wanavyojua hapa - kwa gharama ya kuitwa mjivuni nise kiasi katika ulimbwende nakshi uso mipaka-, mimi napenda sana umahiri katika lugha.Si Kiswahili na Kiingereza tu mpaka kilatini, Kifaransa, lugha za makabila yetu na lugha nyingine zote muhimu.Unavyojua lugha zaidi unajua mengi zaidi. Kwa msingi huu basi, Kiingereza nacho nakipenda, kuanzia historia yake, tamthiliya na nahau zake, ngeli ovyo zake, mashairi yake mpaka istilahi na lahaja zake za kijiografia na kijamii .

  Lakini huku kujifaragua na kujitutumua kiushindani nilikokunukuu hapo juu kwa kweli ni kukosa mantiki kama si ulimbukeni uliobobea.

  Ulimbukeni huu wa "when someone stands up and beat them at their game" unachekesha sana. Ni akili za kitoto tu ambazo hazijapevuka kutoka mawazo ya ushindani usio tija, kuonyeshana ulimbwende usio kina na unaoweza kabisa kuwa na mabaki ya mshikemshike wa "kindumbwendumbwe chalila", kwa wale wanaoelewa ngoma hiyo.

  Una "stand up" vipi kwa kutumia lugha ya mwenzako? Mimi naona una "bow down" tu!

  Wenyewe wanakuangalia huku wakisema "G'head with your barely utilitarian globish that merely passes for some outsourced I.BM call centre English !"

  Kwa nini utake kushindana na mtu katika lugha yake? Au hata isiyo yako? Unaamini kujua lugha yake/ isiyo yako ndiyo kuwa na akili? Kwa hiyo ukiongea lugha yake vizuri ndiyo atakuona unafaa na kukuachia makombo ya mezani?

  Nilikuwa nafanya kazi na MSkoti mmoja nilivyokuwa Tanzania, alikuwa ana shauku sana ya kutaka kujifunza lugha mbalimbali, na alikuja Tanzania huku akitaka sana kujifunza Kiswahili, lakini tatizo kila alipoanzisha mazungumzo kwa Kiswahili na Watanzania, Watanzania walikuwa wanamjibu Kiingereza, kama vile hawamsikii kwamba yeye anaongea Kiswahili, au kama hawataki "bwana mkubwa" apate shida kuzungumza Kiswahili kama vile wao hawajasoma na hawajui Kiingereza (kwao kujua Kiingereza ilikuwa ni alama ya kusoma na daraja) basi huyu Mskoti alipata tabu sana kuzungumza Kiswahili, ikatokea kukawa na mpishi mmoja alikuwa anampeleka peleka Kiswahili ndiye akaja kuwa rafiki yake mkubwa, na huyu Mskoti akawa anamheshimu sana yule mpishi, kwa maana hakutaka kumtetemekea yeye kwa sababu mzungu, na kujitia kuongea Kiingereza.

  Funzo la habari hii ni, kama kweli hutaki wageni wajiulize kuhusu kama wewe ni Mtanzania au vipi, usiwazungumzie Kiingereza, zungumza nao Kiswahili, watajua.

  Ukizungumza Kiingereza unawapa haki ya kukuuliza wewe mtu wa wapi, maana Kiingereza kinazungumzwa kama lugha ya kwanza na watu wa sehemu zote za dunia.

  Na Watanzania wengi hatujui Kiingereza.

  Zaidi ya hapo, utakuwa si mkweli kujifaragua kushangaa kuulizwa kama wewe ni Mtanzania, wakati pengine moyoni mwako ulianza na nia ya kutaka kujitenganisha kutoka Watanzania wa kawaida tusiojua Kiingereza vizuri, ili bwana mkubwa mzungu akuone kwamba wewe si kama wale.

  Na baada ya kusema yote hayo, kwa mtu anayefuata uzuri wa lugha na logic, Kiingereza hakifui dafu kwa Kiswahili. Na kama unabisha kamsome poet/ playwright laureate George Bernard Shaw (Nobel for Literature and Oscar) uone alivyokisagia Kiingereza, halafu soma tenzi za Kina Shaaban Robert na Saadani, uone Kiswahili kilivyojipanga vizuri. Na siongei hivi kwa sababu ya uzalendo, mnaonijua mnajua ninavyounyea uzalendo utafikiri reincarnation ya H.L Mencken.

  Utumwa wa mawazo mgumu sana kuuondoa.
   
 11. JM Aristotle

  JM Aristotle Senior Member

  #11
  Jun 19, 2010
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Whatever man...
  Suit yourself!!!
  Kiswahili bongo????????????
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  kama hujasoma literature usilaumu sana. kuna somo linaitwa phonology (study of speech sound of a particular language). ukiongea kizungu si uongee na milafudhi ya kwenu. ongea kwa ile accent ya mzungu. mbona kuna wazungu wengi tu na wachina huwa wanaongea kiswahili na kuweka mapozi yanayostahili katika lugha yetu?
   
Loading...