You are not alone Mwana JF

You are not alone Mwana JF

Pure nomaa

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2011
Posts
1,158
Reaction score
1,388
Bwana Yesu asifiwe wapendwa

Maisha ni safari ndefu yenye milima na mabonde,furaha na huzuni,utajiri na umaskini ndani yake

Kila Binadamu kwa wakati wake alishapitia au anapitia changamoto mbalimbali maishani ambazo zinatusababishia huzuni na majonzi zaidi kuliko furaha

Mpe nguvu Mwana JF kwamba changamoto anazopitia hata wewe ulishapitia na ukazishinda au unapitia na unaamini utashinda

Kwangu mimi ni hizi hapa
*Nilitapeliwa Tsh300000/-
*Toka nimalize chuo mpaka sasa sina ajira
*Toka nizaliwe sijawai kuwa na rafiki wa kike
 
Kuna wenzio waliotapeliwa pesa ndefu sana ndugu! wakapoteza mda wao mwingi na wakafeli masomo kabisa.
Wakaafectika kisaikolojia.
Na wengine walipata ukimwi kabisa mkuu sahivi wako icu wanahesabu siku tuu na mateso makali. Wengine ni marehemu waliopotea bado wakiwa wadogo na kutegemewa na familia.
Wameipotezea familia pesa nyingi sana na ubaya zaidi unakuta ndio mtoto pekee na wazazi wameshakuwa wazee!
embu niambie ni uchungu gani watakao kuwa nao wazazi wao au kama ni single parent!

Mkuu wacha kabisa mkshukuru Mungu kwa kukulinda hadi hapo.
Shukuru pia hujajichanganya na wanwake maana hujui ungekua katika hali gani saivi!
Fanya vibarua na kujiajiri usiwe tegemezi kwa serikali tuu.

Mwish omba Mungu akubariki zaidi.
 
Hahhaa... Yaani alafu JF inaharibu watu sana, kila mtu humu ana-gene za usalama wa taifa... Hehhehe mtu anajiunga JF akiwa bwege tu, lakini baadae JF inamjanjarusha na anakuwa hashikiki...
Usalama wa taifa ki vp mkuu?
 
Mmh!
1. Pole sana! Mungu anasema alaaniwe mwizi na nyumba yake. Aliekutapeli kaondoka na matatizo na laana zako zote. Usijali utamiliki zaidi ya hicho kiasi.
2. Ndo maisha! Soon ajira zitatangazwa na utapata nafasi yako. Mtangulize Mungu.... Ukipata kamtaji anza biashara.
3. Sijui ni msimamo wako kua hivyo au una matatizo... Ila usihofu, mda wako utafika. Mungu akuongoze na akusaidie.
 
ivi kumbe kama huna rafiki wa kike ni challenge nayo!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom