Yono + Majembe Auction Mart = CCM 2010

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Kampuni ya Yono ambayo ni kampuni ya udalali na ile ya Majembe zote zinamilikiwa na wana CCM Maslahi.Wakati Yono inamilikiwa na Mbunge wa Njombe Magharibi, Yono Kevela. Majembe inamilikiwa na Seth Moto ambaye ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Hizi kampuni mbili ndizo kampuni pekee za udalali ambazo hupewa tenda kubwa kubwa za kukusanya madeni ya serikali au kusimamia ukusanyaji wa fedha za serikali.

CCM mwakani haitatumia hela za EPA, lakini watu kama Majembe na Yono watatoa pesa ili chama chao kishinde waendelee kutafuna hela za walipakodi wa Tanzania.

Huu ni mtego mwingine,wadanganyika tumeshanasa!!!!!
 
Mtu yeyote aliye makini atahoji mienendo ya kampuni hizi mbili, maana zinapewa ulaji wa aina yake..something behind!
Lazima kuna retirement fulani inafanyika mwisho wa siku...N/W/SEARCHING!
 
halafu hawa wahuni wanasababisha foleni,WIZI MTUPU1!leo kimara palikuwa hapaenei
 
Kigarama, kwa upande wangu hizi kampuni mbili lazima zitakuwana na mkono wa mafisadi wa CCM. Na ni kweli tupu hili zoezi ambalo majembe wanafanya kukamata dala dala na mabasi ya mikoani ndio njia ya kukusanya uchakavu wa uchaguzi 2010. Tena hawa jamaaa ni wasumbufu sana wanapofanya hiyo kazi yao. Ni jana tu pale morocco kituoni walimkata dereve wa dala dala kwa kutovaa sare wanataka kushusha abiria gari iende yard kama hawatalipwa 250,000 faini mpaka abiria walipochachamaa ndio mmoja wao ikabidi apande mle kwenye gari hadi mwenge. Hivi kweli SUMATRA ndio nao wanashiriki kwenye haya mazingaombwe?? Kweli huyu aliyetupulizia dawa ya usingizi wadanganyika mungu amlani kesho asiamke kabisa!!
 
CCM mwakani haitatumia hela za EPA, lakini watu kama Majembe na Yono watatoa pesa ili chama chao kishinde waendelee kutafuna hela za walipakodi wa Tanzania.

Huu ni mtego mwingine,wadanganyika tumeshanasa!!!!!

Hivi hii inji, mungu wake ni FISADI?!!!!!
 
Mtu yeyote aliye makini atahoji mienendo ya kampuni hizi mbili, maana zinapewa ulaji wa aina yake..something behind!
Lazima kuna retirement fulani inafanyika mwisho wa siku...N/W/SEARCHING!

Acheni kulalama anzisheni makampuni yenu yashindane na hizo, kwa hela gani wanapata mpaka aifadhili CCM???? Kigezo cha mmiliki wa kampuni kuwa mwanaCCM basi kazi zote nchi nzima ni za ufisadi, fanya utafiti wa kutosha sio unakurupuka tu.........

Wacha hata foleni zije ni suala la muda, tumechoka na MADEREVA WAHUNI...........
 
Kampuni ya Yono ambayo ni kampuni ya udalali na ile ya Majembe zote zinamilikiwa na wana CCM Maslahi.Wakati Yono inamilikiwa na Mbunge wa Njombe Magharibi, Yono Kevela. Majembe inamilikiwa na Seth Moto ambaye ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Hizi kampuni mbili ndizo kampuni pekee za udalali ambazo hupewa tenda kubwa kubwa za kukusanya madeni ya serikali au kusimamia ukusanyaji wa fedha za serikali.

CCM mwakani haitatumia hela za EPA, lakini watu kama Majembe na Yono watatoa pesa ili chama chao kishinde waendelee kutafuna hela za walipakodi wa Tanzania.

Huu ni mtego mwingine,wadanganyika tumeshanasa!!!!!
ndio maana hata samaki wa Magufuli mwanzoni ni kampuni hii ya YONO tuliambiwa imeshinda tenda ya kuwauza kwaniaba ya serikali, aah CCM wanamambo. ASANTE KWA KUFIKIRI KWA KINA INALETA MAANA.
 
Back
Top Bottom