Yondo Sister: Malkia wa soukous

Yondo Sister: Malkia wa soukous

Dada Yondo,aliyezaliwa Denise Kusala Yondo mnamo Aprili 23,1958, huko Bukavu, Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), ni mwanamuziki mashuhuri wa Kongo anayejulikana kwa mchango wake katika muziki wa soukous na kwassa kwassa. Anatoka katika familia ya muziki yenye baba kutoka Kongo na mama wa Ubelgiji-Kongo.

Yondo alianza kazi yake mwaka wa 1975 akiwa na bendi ya Tabu Ley Rochereau, L'Afrisa International, pamoja na dadake Chantal Yondo. Hapo awali alipanga kuwa dansi, anamsifu Rochereau kwa kumtia moyo kuwa mwimbaji.

Yondo alijishughulisha na maisha ya peke yake mwaka wa 1982 na baadaye akajiunga na bendi ya Soukous Stars. Anaadhimishwa kwa vibao kama vile "Bazo na albamu kama vile "Derniere Minute" na Agenda".
Kwa sasa anaishi Paris, Sister Yondo anaendelea kutamba na muziki wa Kiafrika kwa sauti yake ya kipekee na uwepo wa jukwaa la kuvutia.

View attachment 3281158
Bila kawimbo kake uzi haujakamilika
 
Enzi zile yuko na kundi la soukous stars mwanamama huyu akiwa na umri kama miaka 40+ alikuwa ana uwezo wa kukata kiuno balaa, hawa kina luiza mbutu wakasome. Huyu mama sijui kapotelea wapi miaka hii? Enzi hizo miziki ya kizaire/kikongo ilikuwa imetawala anga la Tanzania
 
Kipindi hicho hatuna identity ya muziki ilikuwa ni full miziki ya Congo na kuiga ya huko ukibadilisha sana unakwenda majuu; afadhali kabla (bendi zetu zilikuwepo)

Wabarikiwe sana madogo wa sasa atleast DJ asipoweka Jingle anaweza kucheza full playlist mwanzo mwisho Miziki ya ndani

Anyway kipindi hicho kilikuwa kipindi chao ila nadhani sasa hivi Bongo are better off; Kudos kwa Madogo wa Sasa...
 
1. Yondo Sister
2. Soukoss Stars
3. Gatho Beevans
4. Mbilia Bell
5. King kester Emeneya
6. Kanda Bongoman
7. Pepe Kale
8. Koffi Olomide (huyu dingi yupo vizazi vyote)
 
Back
Top Bottom