Yohana Mjinga bana..........!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yohana Mjinga bana..........!!!!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by gambachovu, Feb 24, 2012.

 1. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Alipewa shilingi mbili(coins) aende kununua maziwa..
  Njiani akakuta watoto wenzake wanaokota mawe na kuyarusha kwa nia ya kuapopoa shorwe(aina ya ndege). Naye (Yohana),akaamua kupopoa ndege wale.. Baadaye akaamua kuendelea na safari ya kwenda kununua maziwa. Alipofika,aliulizwa hela.Akatafuta shilingi mbili zile bila mafaniko.ndipo akakukumbuka alizitumia kupopolea ndege!

  Aliporudi bila maziwa,bibi yake alimsema na kumkaripia sana! Na akampa hela nyingine huku akimsisitizia sana,kuwa anaweka kila anachotumwa mfukoni mwa kaptura yake kuepuka kupoteza.

  Akapimiwa maziwa,akalipa. Wakati wa kurudi,aliyakumbuka maneno ya bibi yake alipokuwa akimkaripia.. Akaona kweli amefanikiwa kurudi na maziwa baada ya kutunza hela mfukoni. Akaona amfurahishe zaidi bibi yake,akchukua maziwa yale akaanza kuyamimina kwenye mfuko wa suruali yake! Akashangaa kuona yanapenya na kumlowesha mguuni,akamimina mpaka yakaisha! Akashangaa sana! Lakini akasema atamweleza bibi yake yote yaliyotokea.

  Aliporudi alikaripiwa sana na bibi yake,na akamwita mjinga,na Yohana alisikitika sana. Hakutumwa tena maana bibi sasa alienda mwenyewe.

  Siku nyingine bibi alitaka nyama ya kitoweo. Akampa hela. Akafika bucha,akauziwa nyama. Njiani akajisemea kuwa leo hatakosea tena. Sasa kwa kuwa enzi hizo hakukuwa na mifuko ya Rambo kama sasa,na yeye alitaka kufuata masharti yote ya bibi yake ,akaamua kuchukua kamba ndefu na kuifunga vizuri nyama ile,kisha nye akajifunga mkononi akawa akielekea nyumbani huku akiiburuta njiani nyama ile.. Alipokaribia kufika nyumbani,aliona aukague mzigo wake aliokuwa akiuburuta.. Cha ajabu hakuona nyama ile aliyotumwa! Akaona arudi kuitafuta..
  Alirudi taratibu huku akitafuta kwa makini,ndipo aliwaona mbwa wawili wakiila nyama ile. Akaona aende kuwanyang'anya,nao wakmtishia kwa kubweka sana mpaka akakimbia kwa bibi yake...

  Pata picha ya ujinga wa Yohana mjinga!
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  mmmmh, wee Gee Cee
  umempeleka wapi yule mtu wa 3?
   
 3. libent

  libent JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Aisee Yohana ni mjinga lakini bibi yake ndiye aliyesababisha yote
   
 4. libent

  libent JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kongosho mbona unakimbia salamu yangu?
   
 5. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Aaah Kongosho...
  Mi najua wapi nyendo zake!
   
 6. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Shida ya Yoahana,hakuchanganya na zake...source:Kikwete
   
 7. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Una namba ya yohana ya simu?
   
 8. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na ujinga wote huo,awe na simu, aringe....!!

  Lazima atakuwa alifungiwaga kipande cha sabuni,na akakata tamaa tangia hapo.. We ukimwangalia personality yake,unamwonaje kwani.. Mwangalie kwa makini...
   
 9. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  We yangu ulijibu?

  Au... Haya basi.. Mambo libent....?
   
 10. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Umenikumbusha mbali mkuu!
  Nadhani kama umekumbuka hii, basi wimbo wa 'Pauli mchafu ...' bila shaka unaukumbuka.
   
Loading...