Yeye RC, mimi Luthelan

Akilitime

JF-Expert Member
Dec 27, 2017
565
1,000
Anasema hayupo tayari kuhamia Lutheran.
Anadai abaki kwenye dhehebu lake na mimi nibaki kwenye dhehebu langu hata tutakapoingia kwenye ndoa.
Wakuu hali kama hii si kukaribisha migogoro ya hapo baadae?
Ushauri
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,237
2,000
Anasema hayupo tayari kuhamia Lutheran.
Anadai abaki kwenye dhehebu lake na mimi nibaki kwenye dhehebu langu hata tutakapoingia kwenye ndoa.
Wakuu hali kama hii si kukaribisha migogoro ya hapo baadae?
Ushauri
Hakuna mgogoro wote ule. Anzeni maisha aisee. RC wanaruhusu ndoa za mseto. Watoto mtakaojaliwa wataamua wenyewe upande wa kwenda.

Mzee Yusuf Makamba ni muislam, ila mke wake ni RC hadi kesho. Mary Majaliwa ni RC kindakindaki na mh. Waziri Mkuu ni Muislam, maisha yao yanaendelea vizuri. Mifano ni mingi. Hizi dini zimeletwa tu na wageni, haziwezi kututenganisha na wapendwa wetu kihivyo.
 

carcinoma

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
4,844
2,000
Watu wanikomalia mambo ya dini unakuta mpaka sasa mlishakulana papuchi (mmezini) bado mnakomaa na dini. Unakuta mnasema uongo yaani kwa ufupi mnavunja amri zote za Mungu lakini bado mnakomaa na dini..

Hakuna atakayeenda mbinguni kisa dini

Sent using Jamii Forums mobile app
 

okyo

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
2,006
2,000
Anasema hayupo tayari kuhamia Lutheran.
Anadai abaki kwenye dhehebu lake na mimi nibaki kwenye dhehebu langu hata tutakapoingia kwenye ndoa.
Wakuu hali kama hii si kukaribisha migogoro ya hapo baadae?
Ushauri
Dini zenu ndo zina oana?

Kwani kuna tatizo Gani wewe ukimfuata au yeye akiamua kukufuata mnaabudu mungu huyo huyo hizi mbanga za sitaki kwenda kule sitaki enda huku mnazitoa wapi?

Yaonyesha nyinyi nyote mnaujeuri Fulani hivi hivo sio rahisi kuelewana jaribuni tafuta suruhu kwanza kwa Aya mambo madogo maana ndoa Ni taasisi inavimbwenga vya kila Aina sijui kama mtaweza kama mtashindwa Na hili dogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: bbc

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom