Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Status
Not open for further replies.
PIA LINGANISHA HIZI STATEMENTS!!..
1474919739516.jpg
1474919749858.jpg
1474919759274.jpg
1474919766730.jpg
1474919777213.jpg
1474919816546.jpg
 
..Yesu alikua 1oo% GOD na 1oo% Human akiwa duniani mkuu sasa inategemea na circumstances ndo tunaweza kujua alikua katika Hali gani
Kwahiyo Yesu amegawanyika sehemu ngapi? Katika kugawanyika huko je ana uwezo na mamlaka yaliyo kamili au ni tegemezi? Kama ni tegemezi je anamtegemea yupi zaidi ya yeye mwenyewe.

Yohana 17:3-4

Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
4 Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye
 
UKITAKA HATA USHAHIDI WA QURAN SEMA NIKUPE!!!..
Tatizo unabandika maandiko mengi kwa wakati mmoja. Weka moja kwanza upate ufafanuzi. Hilo swala la yesu kusema kwamba mimi na baba ni wamoja au aliyeniona mimi kamuona baba. Yesu hakumaanisha kuwa ni wamoja kiuungu bali ni wamoja kimafundisho. Yesu alitumwa na Mungu hivyo anachonena ndio kile kile alichoagizwa na Mungu.

Yohana 14:23-24

Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
24 Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka
 
UKITAKA HATA USHAHIDI WA QURAN SEMA NIKUPE!!!..
Watu wa israel walimuona sura ya Yesu na pia hata sauti yake pia. Lakini sio sura ya Mungu na sauti ya Mungu hawakusikia.

Yohana 5:37-43

Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona.
38 Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye.
39 Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.
40 Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima.
41 Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu.
42 Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.
43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.
 
Wanqoshutumu Yesu ni kwqvkuwa alijifanya yeye ni sawa na Mungu (Yohana 5:18 - Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake; na Yohana 10:30 - Mimi na Baba tu umoja".

Lakini wafuasi wake hawakumwona Yesu kama sawa ba Mungu, hata Paulo kwenye waraka wake kwa Wafilipi 2:9 anaandika "Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina". Ni hakika Paulo hakuamini Yesu alikuwa Mungu.

Hivyo basi ni vizuri tutofautishe Mungu, Mwana wa Mungu na Umungu. Mungu ni mmoja aliyeumba mbingu na dunia. Wanadamu wote ni wana wa Mungu. Yesu ni mwana wa Mungu mwenye Jina lipatalo Majina yote kwa kuwa ana Umungu.
 
Umungu (divine)ni tafsiri ya andiko takatifu Yohana 1:1 - "Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu".
 
  • Thanks
Reactions: MJM
Kwa kukusaidia;-Wafilipi 2 ;5-8
5.iweni na nia hiyohiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo ndani ya kristo Yesu.

6.ambaye yeye mwanzo alikuwa na namna ya Mungu,naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa si kitu cha kushikamana nacho;7.bali alijifanya kuwa hana utukufu,akatwaa namna ya utumwa akawa ana mfano wa wanadamu;8.tena,alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti,naam mauti ya msalaba.
 
Hizi sarakasi humu jamvini zilikuwa zimetulia naona kidogo kidogo zinaanza kurudi..hivi mnaamini kabisa kwa hii mistari yenu miwili mitatu mnayotusua tusua kutoka kwa Bible kuja kuchallange watu wenye akili zao itauuwa Ukristo?

bora mngeanza kuzitetea nafsi zenu na mabaya myatendayo kuliko kuja kuwafundisha watu imani yao waliokua wakiishi na kuiamini.
 
Paulo anaweza kua sawa tu,kwa MUNGU yote yawezekana kama alivyoweza kumtengeneza popo.wengine wanamuita ndege na wengine humwita mnyama.yamkini YESU alikua BINADAMU na MUNGU pia


Ukimwita popo ni ndege lazima utoe sifa za ndege

ukimwita popo ni mnyama lazima utoe sifa za mnyama

kutokana na sifa zake ndio unaweza kumweka popo kwenye kundi gani

Pia kwa yesu ukimwita yesu ni binadamu lazima utupe sifa za kuwa binadamu ni zipi ???

ukisema yesu ni mungu , utupe sifa za kuwa mungu ni zipi ???

haiwezekani mungu akawa mtu wala mtu akawa mungu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom