Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Status
Not open for further replies.

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,986
1,282
1474825695567.jpg


"Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, MTU ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo."

Yohana 8:40

Katika andiko hilo YESU kwa kinywa chake yeye mwenyewe amejiita kuwa ni "MTU". Kama kuna mtu ana ushahidi wowote katika biblia YESU akijiita MUNGU, basi nami hapo nitaamini kuwa YESU Mungu.

Hata hivyo, mnaweza kusema pia, kuwa YESU alikuwa Mungu na Pia alikuwa mtu. Hata hivyo tukitazama sifa mbalimbali za mungu kama zilivyo tajwa au ainishwa na biblia, utaona hata kiduchu YESU hana sifa hizo.

Mathalani.

"Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza.."

Hesabu 23:19

Tumeona katika Yohana 8:40 Yesu akijiita Mtu, na hapa katika hesabu tunaambiwa Mungu si mtu, sasa wewe unayemuita Yesu Mungu umepata wapi?

NANI KAFUNDISHA YESU NI MUNGU?

"tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; "

Tito 2:13

Hayo maneno katika kitabu cha Tito, kimsingi ni barua ya kimisionari aliyo andika Paulo kwa watu wa Tito, kama tuonavyo katika barua hiyo, pamoja na mambo mengine Paulo anawaambia watu wa Tito kuwa Yesu ni Mungu Mkuu, maneno haya ya Paulo yanakwenda kinyume kabisa na maneno ga Yesu mwenyewe aliyo yasema katika Yohana 8:40 lakini kinyume kabisa na mafundisho ya kinabii kutoka katika kitabu cha Hesabu 23:19.

YESU ANASEMAJE KUHUSU PAULO?

Awali ya yote Paulo hakuwahi kuwa mwanafunzi wa Yesu na hakuwahi kumuona Yesu Kristo. Yesu kabla hajapaa kwenda mbinguni aliwahi kusema maneno haya.

"Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi"

Yohana 16:1-3

Hapa Yesu anatabiri kuwa wanafunzi wake watakuja kuuliwa, anatabiri wakristo na wafuasi wa kanisa lake watakuja kuuliwa, na akasisitiza huyo atajaye wauwa wanafunzi wake hamjui yeye wala Baba(Mungu)

Nani huyo aliyeua wanafunzi wa Yesu? Jawabu ni Sauli ambaye ni Paulo.

"Lakini Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu."

Matendo 9:1-3

Kwa hivyo Mtu aliyetajwa na Yesu katika injili ya Yohana 16:1-3 kuwa atawaua wanafunzi wa Yesu si mwingine Paulo, na katika kitabu cha matendo tunaoneshwa ukatili wa Paulo kwa wanafunzi wa Yesu. Hata hivyo, Bwana Yesu anaendelea na utabiri wake juu ya Paulo katika aya hii.

"Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo"

Yohana 8:44

Katika aya hiyo Bwana Yesu anasema huyo Paulo si kwamba ni muuaji tu, lakini pia mtu muongo sana. Na uongo mkubwa alio ufanya Paulo ni pale aliposema kakutana na Yesu na kisha akajifanya kipofu.

"Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda"

Matendo 9:3-7

Baaada ya Paulo kuwaua sana wanafunzi wa Yesu na kuwatesa sana ili waache mafunzo ya Yesu, lakini wanafunzi wa Yesu waligoma na walikataa katakata kuachana na mafunzo Yasu. Pia naomba mjue, mafunzo ya Yesu yalikuwa mwiba kwa serikali(Dola ya Rumi) na Paulo alikuwa anatumiwa na serikali katika kuhakikisha wanafunzi wa Yesu wanaachana na ukristo/uyaudi.

Pamoja na juhudi hizo za Paulo lakini alishindwa, hivyo njia aliyo amua kuitumia si nyingine bali ni kujiunga na wanafunzi wa kristo. Na ili aaminike ndipo hapo alipotengeneza stori ya kumuona Yesu na maagizo ya upofu, lakini kubwa zaidi alimnunua Anania ili msaidie kufanikisha lengo lake. Kwa kumtumia Anania na kwa kudanganya kwake kuwa kamuona Yesu, wanafunzi wa Yesu walimkubali.

Na hapo ndipo Paulo alipoanza kuyachakua mafunzo ya Yesu, na ndio maana ukristo wa sasa si ule alio ufundisha Yesu.

YESU NA MFARISAYO.

"Ewe FARISAYO KIPOFU, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi. Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote."

Mathayo 26:23

Paulo msomi mkubwa alikuwa Farisayo, lakini Yesu alisema nini juu mafarisayo? Kama tulivyo ona, Yesu anawaona mafarisayo kama vipofu, lakini kubwa katika andiko hili Yesu anamtabiri pia Paulo na maigizo yake ya upofu.

"Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu"

Matendo 23:6

Kwanza Paulo amekiri kwa kinywa chake kuwa yeye ni farisayo. Lakini hiyo haitoshi Paulo alijitia upofu aso kuwa nao.

"Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi."

Matendo 9:8-9

Katika aya hizi tunaona kuwa Paulo amekiri kuwa Farisayo lakini pia tunaona Paul yuko katika maigizo ya upofu. Yote haya mawili yanakamilisha unabii wa Yesu pale aliposema

"Ewe farisayo kipofu.."

Mathayo 26:23

Katika aya hizo inatajwa sifa kuu au tabia kubwa ya Mafarisayo, na ambayo imethibiti(ilitimia) kwa Paulo. Sifa hiyo si nyingine bali UNAFIKI.

Paulo alikuwa mnafiki, yaani alijifanya muumini wa mafundisho Yesu ili mradi apate kuwapotosha wanafunzi wa Yesu, na hili kwakweli kafanikiwa sababu hakuna hata kanisa moja ambalo linafuata mafunzo ya asili ya Yesu. Kila kanisa lina kituko chake.

MWISHO.

Kwa kifupi huku nikizingatia maelezo yangu yote ya huko juu, kuwa YESU SI MUNGU, lakini hakumaanishi kuwa hakuna wanao muita au wanao amini Yesu Mungu. La kuzingatia kama tukiambiwa kauli ipi ya kushika kati ya YESU mwenyewe na ya Paulo kwa vyovyote vile tunatakiwa kushika kauli ya Yesu.

Kauli zote za Paulo ambazo hazipingani na za Yesu, kauli hizo tutazifuata, lakini kauli yoyote ya Paulo inayo pingana na Yesu, kauli ya Paulo itapuuzwa na kuanguka, alafu watu wote wanatakiwa wafuate kauli ya Yesu.

Hakuna kauli ya Yesu anayo alijiita Mungu, lakini zipo nyingi akijiita Mtu au mwana wa adamu. Na siku zote alijitafautisha na Mungu. Yesu anakata mzizi wa fitina katika andiko hili.

"Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma"
Yohana 17:3

Nasema YESU SI MUNGU, na Paulo ana kesi ya kujibu kwa kudanganya ulimwengu, na kwa kuharibu mafundisho ya Yesu na kubwa zaidi kwa kuwatesa na kuwaua wanafunzi wa Yesu na wafuasi wake.

Katika kuendeleza urongo wa Paulo, watu wameambukizwa urongo, sasa wanatusambazia picha na sanamu za wacheza sinema na kisha wanataka tuziheshimu kama Yesu, kweli watu wanaangamia kwa kukosa maarifa.

TUJADILI!

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whatspp 0622845394 Morogoro.
 
Paulo anaweza kua sawa tu,kwa MUNGU yote yawezekana kama alivyoweza kumtengeneza popo.wengine wanamuita ndege na wengine humwita mnyama.yamkini YESU alikua BINADAMU na MUNGU pia
Duuuh yani binadamu na Mungu pia. Labda unamaanisha mungu mtu kama ilivyo kwa miungu watu na viumbe vinginevyo kama ng'ombe nakadhalika na sio kwamba yesu ni Mungu muumba mbingu na ardhi.

Yohana 20:17

Yesu akamwambia, “Usinishike kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ninakwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.”
 
Duuuh yani binadamu na Mungu pia. Labda unamaanisha mungu mtu kama ilivyo kwa miungu watu na viumbe vinginevyo kama ng'ombe nakadhalika na sio kwamba yesu ni Mungu muumba mbingu na ardhi.

Yohana 20:17

Yesu akamwambia, “Usinishike kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ninakwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.”
Kuna shida gani MUNGU kujigeuza mtu ili watu wabishi wamuelewe? ilihali ana sifa ya mpaka kuijua kesho na ndo kaumba kila kitu hapa duniani,hua anaweza kutamka jambo liwe na linakua, leo kaona watu hawabadiliki kwa kumsikia tu bila kumuona akaamua aje kwa umbo la kibinadamu na ajifananishe na sisi kwa kua alituumba kwa mfano wake shida iko wapi?
 
Dotto: du umeleta hoja tatanishi.

Paulo hana kesi ya kujibu hata kwa vifungu vya Biblia ulivyonukuu.

Biblia siyo kitabu cha kawaida ambacho unasoma kifungu kimoja na kutoa tafsiri.

Siri ya Umungu wa Yesu ni uumbwaji wa binadamu (Ufunuo 4:11 - Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa). Wote tumeumbwa kwa mfano wake. Ni watoto wa Mungu

Paulo
 
Mathew1:23. Tazama bikira atachukua mimba na atamzaa mwana nao watamwita jina lake Emmanueli maana yake MUNGU pamoja nasi.
Mungu pamoja nasi. Hakukumaanishwa kuwa yesu ni Mungu yupo pamoja na binadamu. Bali ni kwamba Kutokana na dhambi walizokuwa wanatenda waisrael ndipo Mungu akaleta mwalimu kwaajili ya kuwafundisha njia sahihi ya Mungu ambaye ndio yesu. Hivyo Mungu alikuwa pamoja nao hakuwaacha wanaisrael wapotee nawala hakuja maanisha kuwa yesu ni Mungu.

Matayo 1:21-22

Atajifungua mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu, kwa kuwa yeye atawaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao."
1:22 Basi, haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema kwa njia ya nabii:
 
Kuna shida gani MUNGU kujigeuza mtu ili watu wabishi wamuelewe?ilihali ana sifa ya mpaka kuijua kesho na ndo kaumba kila kitu hapa duniani,hua anaweza kutamka jambo liwe na linakua,leo kaona watu hawabadiliki kwa kumsikia tu bila kumuona akaamua aje kwa umbo la kibinadamu na ajifananishe na sisi kwa kua alituumba kwa mfano wake shida iko wapi?
Yakobo 1:17

Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.
 
..Yesu alikua 1oo% GOD na 1oo% Human akiwa duniani mkuu sasa inategemea na circumstances ndo tunaweza kujua alikua katika Hali gani
Yakobo 1:17

Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.
 
Paulo kwenye nyaraka zake amasisitiza tu Umungu wa Yesu kama mwana wa Mungu akirejea ya Agano la Kale "Mika 5:2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israel; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele."

Yesu mwenyewe anajibu swali alipoulizwa na Nathanaeli "Yohana 1:49 ...Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israel. 50 - Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya".

Yesu anathibitisha Umungu wake "Yohana 6:38 - Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka" na "Yohana 8:23 - Akawaambia, Ninyi ni wa chini, mimi ni wa juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu".

Nukuu za maneno ya Yesu, kama yalivyoandikwa na wafuasi wake, ni ya kutafakari na kutafakuri sana ya kukanusha Umungu wake.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom