Yeriko Nyerere mwanachama wa zamani wa CHADEMA aliyejiunga CHAUMMA hivi karibuni, amepewa kazi maalum.
Kazi hiyo maalum ni kuhakikisha anawadhoofisha kimkakati baadhi ya viongozi wa CHADEMA na Chama chao kwa ujumla.
Katika kazi yake hiyo mpya ndani ya CHAUMMA, Yeriko ameelekeza Moja kwa moja mashambulizi kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu kuwa ndiye chanzo cha matatizo ndani ya CHADEMA na kudai kuwa yeye yuko tayari kurejea kwenye Chama hicho kama Lissu hatakuwa Mwenyekiti.
Aidha ameendelea kumshambulia kada mwingine wa Chama hicho God bless Lema. Kwa trend hii, Yeriko ataendelea na mashambulizi zaidi kwa viongozi au makada wengine wa CHADEMA.
Jambo Moja la kujiuliza ni kwamba; kama Yeriko ameshajiondoa kwenye Chama hicho, kwa nini asiachane na ya huko na watu wake akaanza maisha mapya huko aliko kwa kujifunza Kisha kunadi sera na Ilani za Chama chake kwa wapiga kura ili wawachague?
Kwa kuhitimisha hii inaonyesha wazi kuwa aliyosema Humphrey Polepole kwamba CHAUMMA na Chama cha akina Luhaga Mpina ni projects ni ya kweli.