Yeriko Nyerere aendelea kusota rumande

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
YERICKO.jpg

Mke wa Yeriko Nyerere, (kada wa Chadema) Neema Alex amesema mumewe ameshindwa kufikishwa mahakamani jana kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya mambo.

Hata hivyo, Neema hakuwa tayari kutaja kilichokwamisha Yeriko kufikishwa mahakamani na kusema kila kitu kiliandaliwa na nyaraka zote zilikuwa tayari kwa ajili ya Yeriko kufikishwa mahakamani.

“Wakati tukimsubiri atoke na kuelekea mahamakani ghafla simu ikapigwa na mmoja wa wakubwa wa polisi akitoa amri ya kwamba asipelekwe mahakamani hadi atakapopiga simu tena.

“Nahisi bado hawajaridhika na maelezo aliyoyatoa mume wangu (Yeriko) ingawa sina uhakika,” alisema Neema wakati akizungumza kwa simu na gazeti hili jana.

Yeriko alikamatwa saa tisa alfajiri juzi akiwa nyumbani kwake Mbutu, Kigamboni na watu wanaodaiwa kuwa maofisa usalama wa mitandao kisha kumpeleka katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu.

Katika tukio hilo, maofisa hao waliambatana na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbaragande, Jamal Hassan anakoishi Yeriko. Neema alisema kuwa jana wakiwa na baadhi ya viongozi wa Chadema walikwenda Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kumsubiri mumewe ambaye hakupelekwa kama walivyotarajia.

Hata hivyo, Neema alisema alifanikiwa kuonana na kuzungumza na Yeriko ambaye alisema yupo katika hali nzuri na hana wasiwasi wala tatizo lolote.

Wakili wa Yeriko, Peter Kibatala alisema hadi jana mchana hakupata taarifa zozote kutoka polisi kwa kuwa alikuwa na majukumu ya kushughulikia kesi nyingine.

“Sijui chochote kwa sasa? Kwa sababu asubuhi niliamkia mahakamani kwa ajili ya kesi ya Lissu (Tundu-Mwanasheria wa Chadema),” alisema Kibatala.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbaragande, Hassan alilieleza gazeti hili juzi kuwa maofisa hao walimwambia wanamkamata Yeriko kwa sababu ya makosa ya mtandao.

Chanzo: Mwananchi
 
Inshaaalah mwenyezi Mungu atamlinda.
 
Hawa wanaamua kupotezea watu muda kwa kupeleka kesi mahakamani wakijua uwezo wao mdogo wa kuthibitisha pasipo kutia shaka. Wanasheria wa Serikali rudini shule
 
Chadema Wako wapi kutoa tamko kuhusu kada wake ? Mbona Kipindi Wema Sepetu alipokatwa alipata full support ya chama tena alikuwa bado hajajiunga na CDM?
Au Yericko alikuwa akijipendekeza ndani ya Chama wakati Chama kilikuwa hakina mpango nae na kuamua kumuacha hali iliyosababisha kukosa misimamo.

By the way...JAH will find out the way.
 
Back
Top Bottom