Yeke Yeke!!...

Wakati umeenda wapi jamani loh! Enzi hizo huo wimbo nakumbuka kila mtu alikuwa akiuimba ajuavyo... Hadi raha yani! Kulikuwa pia na London Beat, Black Box, Mob house, Mob masters nk.. Ilikuwa raha! Tulikuwa tunaruka debe kiuhakika!! Mzee Ruksa ndo anaingia madarakani na video zikaingia...! Nashanga vijana wa siku hizi video zipo na hawajui kucheza wamebaki kujitingisha huku mkono umeshika Mbeleni..!! Sisi hakukuwa na video na tulijua kuruka majoka!! Ha ha ha ha ha.
 
wee! Hiyo list ukija kuweka sasa na zile za reggae za alpha brond.na wimbo wake wa jamaica.na kulikuwepo na wimbo mmoja nimeusahau kidogo embu jaribu kuukumbuka (makret ya soda.,...cret za soda.......cret za soda mamaa.......) kwa tafsri ya utotoni nadhani utaukumbuka.
 
sana tu. Ukiona siku imeanza kwa tabasam bashasha basi ujue kila utakalo lifanya siku hiyo litakuwa powaa.
Umeonaee!Ngoja na kuna kademu kako mtaa wa pili ngoja nikaingize "voko" hakatanitolea nje!Teh,teh,teh,teh!
 
wee! Hiyo list ukija kuweka sasa na zile za reggae za alpha brond.na wimbo wake wa jamaica.na kulikuwepo na wimbo mmoja nimeusahau kidogo embu jaribu kuukumbuka (makret ya soda.,...cret za soda.......cret za soda mamaa.......) kwa tafsri ya utotoni nadhani utaukumbuka.
Ilikuwa raha Mkuu! Unakumbuka radio za wakati huo Player (chenja)? Na badae zikaja radio za tape (kaseti) na redio aina ya Hitachi double spiker, JVC, zikaja Lasonic double deck zikiwa na spika za kuchomoa kila upande.! Hizi Lasonic sijaona mbadala wake kwa umadhubuti. Wale wanaozifahamu watakubaliana nami. Umeme wa betri ya gari kutoka YUASA. Raha raha raha ilikuwa!
 
Dogo huo wimbo wa alfa blond hauitwi Jamaica,unaitwa Afriki!
 
Ilikuwa raha Mkuu! Unakumbuka radio za wakati huo Player (chenja)? Na badae zikaja radio za tape (kaseti) na redio aina ya Hitachi double spiker, JVC, zikaja Lasonic double deck zikiwa na spika za kuchomoa kila upande.! Hizi Lasonic sijaona mbadala wake kwa umadhubuti. Wale wanaozifahamu watakubaliana nami. Umeme wa betri ya gari kutoka YUASA. Raha raha raha ilikuwa!
acha!acha kabisa.kuna dj mmoja alikuwa anaitwa chongo huyo dj alikuwa anazunguka tz nzima akipiga disco.akiwa na kina black moses. Hapo unanikuta nami nimepiga pamba zangu za ukweli.sulu ndeefu mpaka kifuani tulikuwa tunaita mtambo,viatu clipper,na shati la bahama au uji uji, na sun gogos weee!
 
Na mtindo maarufu wa nywele kwa vijana ulikuwa ni Punk! Umenifanya nianze kupekua makabrasha ya picha zangu za enzi hizo. Niliweka punk kama ile ya Shabba Ranks na nilijulikana kwa jina hilo kunako maeneo yangu... Weweeee!! Acha hiyo maneno. Nilikuwa natoka kijijini naenda mjini (wilayani)mwendo wa miguu takriban 30km! kulikuwa na fundi mmoja matata alikuwa anaweza kunyoa hiyo kitu kama ya Shabba Ranks tena kwa mkasi na wembe Topaz! Ukimwi ulikuwa ndo kwanza unaingia mijini. Vijijini habari hatuna, tunakula maini kiulaiiini...!
 
ha ha ha.... post yako imesafisha moyo wangu kwa tabasamu kubwaaaa....lol
 
Dada we acha tu,nawakumbuka watangazaji wa RTD akina anko Julius Nyaisanga,Fank Bujaga Izengo Kadago,Dominic Chilambo..R.I.P..We acha tu!
 
Back
Top Bottom