Yawezekana wananchi hatuambiwi ukweli huu mgogoro na Kenya kuna issue nyuma ya pazia na wala sio COVID-19

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Baada ya Kenya kuzuia ndege na abiria kutoka Tanzania, na sisi tumejibu mapigo. Mamalaka ya usafiri wa anga TCAA imepiga marufuku ndege zote zinazomilikiwa na shirika la ndege la Kenya Airways kutua katika ardhi ya Tanzania. Hii ina maana abiria wanaosafiri na Kenya Airways kutoka mataifa mengine kuja Tanzania watalazimika kuishia Nairobi, na kuunganisha ndege nyingine.

#MyTake:
Kwanza nadhani kuna mgogoro wa kidiplomasia ambao mamlaka hazitaki kuuweka wazi. Sidhani kama tatizo ni Covid19 kama inavyoelezwa. Nahisi kuna mengine yanaendelea ambayo wananchi hatuyajui. Ukiangalia trend ya matukio baina ya Kenya na Tanzania ni kama Korea Kaskazini na kusini. Hakuna kuaminiana, hakuna kuheshimiana, hakuna tena ujirani mwema. Kila mmoja anaonesha ubabe wake.

Pili, ukweli ni kwamba bado tunahitajiana sana. Kwenye biashara, kijamii, na kisiasa. Kuna watanzania wameoa Kenya and the vice versa. Wakenya wanategemea mazao ya chakula kutoka Tanzania. Zaidi ya 60% ya mazao ya nafaka (mahindi, mchele) yanayoliwa Kenya yanatoka Tanzania.

Na Tanzania inatumia sana bidhaa za viwanda kutoka Kenya. Takwimu zinaonesha kuwa Kenya ni nchi ya pili tunayofanya nayo biashara zaidi duniani. Yani tunafanya biashara zaidi na Kenya kuliko tunavyofanya na China, Marekani, au mataifa mengine makubwa.

Kwahiyo tunahitajiana sana. Hatua hii ya kutumishiana misuli inaathiri zaidi wananchi kuliko viongozi. Atakayeumia si Raila Odinga au Kassim Majaliwa. Ni kijana wa Sirari ambaye anategemea kuvusha mazao Kenya kujipatia riziki. Ni kijana wa pale Taveta mwenye kampuni ya utalii anayetegemea mlima Kilimanjaro.

Hii approach ya kutunishiana misuli si sahihi hata kidogo. Tukumbuke hata Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki ilivunjika mwaka 1977 baada ya chokochoko kama hizi.

Hivi tumekosa wanadiplomasia wazuri wa kusawazisha hizi tofauti hadi kufikia kutunushiana misuli hadharani? Kwanini Corona itusababishie uhasama?

Kama kila nchi imeamua kutafuta njia yake ya kupambana na Corona basi kila mmoja aheshimu maamuzi ya mwenzie na maisha yaendelee. Sio kuzozana na kutengeneza migogoro isiyo na sababu. Athari za kuwekeana uhasama na kuharibu undugu wetu ni kubwa kuliko athari za corona yenyewe.!

Na: Malissa GJ
 
Taifa letu limerudi nyuma sana kidiplomasia. Viongozi wanategemea alivyoamka mkuu na kutamka. Rejea ya Shigella zuio malori kauli ya kibabe na baadae mkuu kutoa baraka kauli ile akiwa Singida, akirejea toka Self Lockdown Chato.
 
Pia inawezekana tatizo ni hio coronna tu, corona ni agenda ya mataifa ya magharibi na nchi zote zinatakiwa kufata maelekezo ya corona kutoka nchi za magharibi(WHO) kwa hio ikitokea nchi inayokwenda kinyume na maamrisho au maelekezo Mara nyingi wanajaribu kuziwekea vikwazo nchi hizo zinazokiuka maelekezo, nadhani hapa ndio tatizo linapokuja na kenya itakuwa wameamrishwa kutoka magharibi wazuie usafiri na tz, tz wameamua kutunisha misuli, tusubiri tuone yajayo,
 
amini nakwambia Kenya ndie muathirika mkubwa sana kwa sasa, Tanzania inaanza kufufua na kuanzisha viwanda vyake vya ndani hili pia ni pigo kwa kenya, ... Mkenya ajitafakari kukurupuka kwake zama zimebadilika
Kwenye suala la biashara pande zote mbili tunahitajiana! Na wakatao umia kwenye hili ni raia
Si jpm wala uhuru

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Wal
Taifa letu limerudi nyuma sana kidiplomasia. Viongozi wanategemea alivyoamka mkuu na kutamka.Rejea ya Shigella zuio malori kauli ya kibabe na baadae mkuu kutoa baraka kauli ile akiwa Singida,akirejea toka Self Lockdown Chato.
Kwa hiyo diplomasia inawataka watanzania kuzuiwa malori yao na kufungiwa ndege zao? halafu tuinamishe vichwa?
This is absolute none sense!
 
Kungekuwa na kitufe cha dislike, hapa ningeweka.

Yaani wewe unalaumu Tanzania tu kwa kila changamoto zinazotokea ndani na nje? Mbona unaonekana kama si mwenzetu vile? Kenia wamekuambia nini kama TZ wanaficha? Kenya wameambiwa nini na viongozi wao? Nani aliyeanzisha hii sintofahamu na kwa nini usimwulize unanyooshea vidole nchi yako ambayo nayo imeshtukizwa?

Kwa hiyo kama watu wengi wanavyokuwa "Ndiyo Mwalimu", kwa China na uanfikik wote unataka na sisi tuwe "ndiyo afande kwa Kenya"? Kitu gani ambacho kwa kutokufanya biashara na kenya au KQ tutakosa wa tanzania?

PLease, naomba tusivurugane. Rudisha uungwana kwa Taifa lako na mengine yatafuata. Sasa hivi kampeni za fitina hazina tija na Watanzania hatuzitaki. Tunataka kweli bin wazi.
 
Mkuu madawa tunayotumia huku mashambani 80% yanatoka kenya...... ziwe za ukungu, ziwe mbolea za pakti, ziwe sumu vyote vinatoka kenya na vichache india


Na mazao yetu tutauza wap? kuna mwaka mahindi tuliuza 5000 debe kisa tumewazuia kenya wakaenda zambia........ wakulima tutaumia sana!
 
Tuna option nyingi ikiwemo kuagiza bidhaa toka nchi za SADC sisi tuna chakula wao hawana juzijuzi tumefungua terminal 3 issue ya ndege kuishia kenya haipo tena sasa hivi ndege zimeanza kusafirisha mbogamboga na matunda hapa huu mgogoro utawasaidia zaidi watanzania kuchangamkia fursa zilizopo kuliko kuendelea kuitegemea Kenya
 
Mkuu madawa tunayotumia huku mashambani 80% yanatoka kenya...... ziwe za ukungu, ziwe mbolea za pakti, ziwe sumu vyote vinatoka kenya na vichache india


Na mazao yetu tutauza wap? kuna mwaka mahindi tuliuza 5000 debe kisa tumewazuia kenya wakaenda zambia........ wakulima tutaumia sana!
Hicho ulichosema ni wachache wanakijua Ila kwakifupi Hali ya uingizaji bidhaa kutoka Kenya umekuwa wamashaka mno hasa Sisi wafanyabiashara wadogo ambao tunaagiza bidhaa kutoka kenya
 
Back
Top Bottom