Yawezekana maamuzi ya nchi yakawa yanafanywa na maofisa wa chini, wakubwa wamegoma kutumia TEHAMA. Tupo salama?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Ngoja leo niawachane wakurugenzi na manyapara wote waliomaliza chuo kikuu cha DSM 1997/2002 na wakapata kazi serikalini. Wengi kwa sasa ndio wakurugenzi, makamishna, wakuu wa polisi mikoa nk. Wengi ni marafiki zangu na wakija huku kanda ya ziwa tukikutana tunapiga gambe na moja mbili tatu.

Ila lipo jambo nimejifunza kwao ambalo nimeamua kuliandika leo nikiwa napata ulabu na mmoja wao. Nimemsikia akielekeza zaidi ya watu watatu wafanyie kazi issue ambazo anadai zipo kwenye mfumo wa serikali. Nimemchana live kwa kumuuliza inakuwaje yeye aruhusu watu waingie kwenye mifumo kwa password yake? Anajibu yeye sasa hivi ni boss anasubiri kula kunywa akiwa anaelekea kustaafu hivyo vijana wafanye kazi.

Huu ni uzembe mkubwa sana kwenye sekta ya umma Tanzania. Hakuna nchi unaweza kwenda hata Kenya tu hapo au Rwanda password ya bosi ikatumiwa na mlinzi, au kuhudumu au msaidizi wake. Password ni siri na kinachotumwa kwa bosi ni siri .

Nataka kueleza nini hapa, viongozi mbalimbali wa serikali awafanyi maamuzi ila wanaonekana na kuaminiana kwamba wao wanafanya maamuzi. Badala yake upo uwezekano afisi mdogo kabisa let say msaidizi wa mkurugenzi akawa anajibizana na katibu mkuu wa wizara bila katibu mkuu wa wizara kufahamu.

Kama serikali inataka kufanya utafiti kwenye huu uhuni wa viongozi wazembe, wawaite pamoja na kuwakabidhi computer kama wataweza kulog in. Nasema haya kwa sababu karibia viongozi 30 ambao nimekuwa nagongana nao lazima usikie akipiga simu zinazoashiria yeye siyo mtumiaji wa mfumo ila vijana waliochini yake.

Hali hii ina athari kubwa sana. Nenda benki classmate na college mate hao hao ambao tulisoma pamoja ni vigumu kusikia amekabidhi password kwa mtu mwingine. Nenda mashirika ya kimataifa uone , nenda hata mataifa yanayotuzunguka uone.

Kama serikali inapiga kelele matumizi ya mitandao, mbona viongozi wake wanakataa kutumia mitandao? Je, kuna siri tena serikalini? Je, kama viongozi wanakosa msukumo wa kutumia mifumo hakuna uwezekano kwamba watoto wao, mademu zao na wake zao wanaweza kuona taarifa za serikali bila mabosi hawa kuwafahamu kwamba wamedululiwa?

Kwanini serikali isiwafute kazi hawa viongozi kuiweka nchi Sehemu salama? Siku serikali ikianza kutumia huduma mtandao nchi itabaki salama?

Badilikeni ndugu zangu, nchi ni yetu sote. Tusipoilinda tutavamiwa na kukosa pa kwenda. Tulinde taarifa zetu na nchi, hasa ninyi wenye dhamana ya maamuzi na mnaopewa mambo mazito.

Data Privacy 🔏
 
Ngoja leo niawachane wakurugenzi na manyapara wote waliomaliza chuo kikuu cha DSM 1997/2002 na wakapata kazi serikalini. Wengi kwa sasa ndio wakurugenzi, makamishna, wakuu wa polisi mikoa nk. Wengi ni marafiki zangu na wakija huku kanda ya ziwa tukikutana tunapiga gambe na moja mbili tatu.
Hii ni hatari sana kama ni kweli
 
Hilo tatizo lipo kwa pande zote private mpk serikalini.

Mwaka juzi nilikuwa nafanya research ya Cyber Security hasa ktk kudevelop cracking softwares za passwords over bruteforcing attacks.

Nilitengeneza phishing environment ambayo ili harvest password 1,024.

Passwords hizo nikaziongezea ktk custom crafted DICTIONARY ambayo itaenda kucrack Password moja moja mpka mfumo ufunguke.

Passwords nyingi sana kwa sisi Watz ni weak.
Passwords nyingi ni Common
Passwords nyingi ni rahisi ku guess
Watz hawajui jinsi ya kutunza passwords.
Passwords moja inatumika ktk mifumo zaidi ya miwili. HII NI MBAYA MBAYA MBAYA.
 
Ni kweli uzembe upo hata mimi nilikua naingia kwenye zoom meeting juu nimevaa Shati koti la suti na tai ila chini nimevaa boksa
Alaf kwenye ukuta nimeweka picha ya Rais jamaa wakawa wanajua nipo ofisini kumbe nimejipa likizo
 
Ni kweli uzembe upo hata mimi nilikua naingia kwenye zoom meeting juu nimevaa Shati koti la suti na tai ila chini nimevaa boksa
Alaf kwenye ukuta nimeweka picha ya Rais jamaa wakawa wanajua nipo ofisini kumbe nimejipa likizo
Daaah mwana nimecheka kifala sana
 
Back
Top Bottom