Kauli ya Magufuli kuwa Kabudi na Lukuvi hawatagombea Urais haikuwa ya ghafla, ilipangwa siku nyingi na ndio mwanzo wa mgogoro ndani ya CCM

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,210
2,000
Siku Magufuli alipotamka hadharani kwamba Kabudi na Lukuvi hawatagombea Urais kwa sababu ya umri wao mkubwa, wengine walicheka wakiichukulia kama ni kauli ya ghafla. La hasha, hii ilikuwa ni kauli ya kimkakati ambayo Magufuli alikuwa ameitafakari na kupanga kuisema kabla hata ya kuingia Uchaguzi Mkuu.

Ni kauli ambayo iliwashangaza sana Kabudi na Lukuvi, kuwashitua, kuwakatisha tamaa na hatimae kuwaudhi sana. Ilibidi tu wajichekeshe mbele za watu.

Magufuli ameitoa kauli hiyo akiwa amesoma wazi nia za Kabudi na Lukuvi kutaka kuwa Marais wajao. Ukiangalia kwa makini, Kabudi na Lukuvi wamekuwa waaminifu sana kwa Magufuli, wakiwa nyuma yake kwa 100%, wakimpamba kila wanapopata nafasi, na lengo lao ilikuwa kupata kuungwa mkono na Magufuli ili kuwa Rais awamu ifuatayo. Kuna wakati mtu kama Kabudi anajitoa kabisa maarifa na akili (wisdom and intelligence) ili mradi tu ajiweke upande wa Magufuli na Magufuli amuone ndio Waziri anaefaa kuwa Rais ajaye.

Sasa kwa kauli hii Magufuli amefanya kosa kubwa sana. Ametangaza vita na mgogoro ndani ya CCM katika suala la Rais atakaemrithi. Magufuli ameshaanza kumpigia debe "kijana" anaetaka amrithi, kijana ambae Magufuli ataweza kumtawala (kum-influence) kirahisi wakati amemaliza awamu hii. Na watu wanajua ili Magufuli awe na "mrithi" wa kumtawala, lazima awe ni kijana wake mtiifu kabisa kama vile Makonda, au kijana wa kutoka kanda ya ziwa.

Sasa ndani ya CCM kuna watu wameanza kuliona hilo na hawataki kabisa! Kuna watu wanaona Lukuvi au Kabudi ndio Mawaziri "wenye hekima na busara" wanaofaa kumrithi Magufuli.

Magufuli amekuwa na haraka mno kuanzisha vita ya wa Rais ajae, akidhani kuwakatisha tamaa mapema Kabudi na Lukuvi itasaidia kuwaondoa uwanja wa mapambano. Magufuli alipaswa ajifunze toka kwa Kikwete, ambaye alijua kabisa Mwandosya alitaka kuwa kumrithi kiti cha Urais, na Kikwete akajifanya kumuunga mkono Mwandosya hadi dakika za mwisho kabisa ndio akatoa majina yake mfukoni. Mwandosya akawa amepigwa knock out kwa " sucker punch" hakuamini betrayal ya Kikwete! Sidhani hata kama hata wanasalimiana hadi leo. Kikwete mtoto wa mjini, Magufuli mtu wa kuja, ndio tofauti zao.

Sasa athari za Magufuli kuonyesha karata zake mapema ni kwamba ile support aliyopata toka kwa Kabudi na Lukuvi katika awamu ya kwanza hataipata tena! Hilo ndilo kosa kubwa Magufuli amefanya. Sasa Kabudi na Lukuvi hawatampta tena ile 100% waliyompa huko nyuma. Kibaya sana kinachoweza kutokea ni kwamba wataunda makundi yao ndani ya CCM ya kuwa support, lengo likiwa kupanda mbegu ndani ya watu wa CCM kwamba Magufuli ni kiongozi asie na hekima hata kumuunga mkono juu ya chaguo lake la Rais ajae itakuwa ni kosa kubwa!

Kwangu mimi, Hotuba ya Kabudi aliyotoa kwa wafanya kazi wa mambo ya ndani ina kila namna ya viashiria kwamba ameanza mapambano na kujitofautisha ili watu waone anaweza kuwa Rais wa namna gani!

Yajayo ndani ya CCM yatafurahisha sana. Mpambano ndio kwanza unaanza!
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,210
2,000
Very sad. Wamekosa sifa gani? Kwani katiba inasema anayezidi umri gani ndio asigombee urais?
Inasikitisha sana rais wa nchi badala ya kuchaguliwa na wananchi, tunachaguliwa na Mwenyekiti wa CCM
Mkuu Bujibuji, sio kwamba wamekosa sifa. Kama ni umri angalia Ali Hassan Mwinyi alikuwa na umri gani alipokuwa Rais wa Tanzania. Kina Joe Bidden wana umri gani?

Haki ya umri aliyo nayo Magufuli ni katika kuunda baraza lake la Mawaziri. Ana uhuru wote hapo, hata kuchagua Mawaziri wanaovalia suruali matakoni. Lakini suala la Rais ajae atakuwa na umri gani sio lake kabisa, ni la CCM na wananchi kwa ujumla.

Suala la umri Magufuli anatumia kama kisingizio tu cha kutaka kuwaondoa Kabudi na Lukuvi mapema kwenye kinyang'aniro cha Rais ajae ili amtengenezee njia mtu wake. Sasa utaona reaction ya chini chini ndani ya CCM, na pia reaction ya Kabudi na Lukuvi. Ni vita!
 

Ralph Tyler

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
2,275
2,000
Very sad. Wamekosa sifa gani? Kwani katiba inasema anayezidi umri gani ndio asigombee urais?
Inasikitisha sana rais wa nchi badala ya kuchaguliwa na wananchi, tunachaguliwa na Mwenyekiti wa CCM
Kwani Kabudi ana nguvu gani huko CCM? Ameshaambiwa wakichemsha watarudishwa walikotoka, na anajijua alikotoka kwani haoni aibu tutaja hadharani mara kwa mara kuhusu alikoibuliwa na kuketishwa na mfalme. Lukuvi hana alikotoka maana hana taaluma yoyote, hakuna taaluma ya ukuu wa mkoa, kwa hiyo hana pa kurudi. Hawa wawili inabidi wawe watiifu tu, hakuna namna.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
54,683
2,000
Mkuu Bujibuji, sio kwamba wamekosa sifa. Kama ni umri angalia Ali Hassan Mwinyi alikuwa na umri gani alipokuwa Raisi wa Tanzania. Kina Joe Bidden wana umri gani?

Haki ya umri aliyo nayo Magufuli ni katika kuunda baraza lake la mawaziri. Anaweza uhuru wote hapo. Lakini suala la raisi ajae atakuwa na umri gani sio lake kabisa, ni la CCM na wananchi kwa ujumla.

Suala la umri Magufuli anatumia kama kisingizio tu cha kutaka kuwaondoa Kabudi na Lukuvi mapema kwenye kinyang'aniro cha raisi ajae ili amtengenezee njia mtu wake. Sasa utaona reaction ya chini chini ndani ya CCM, na pia reaction ya Kabudi na Lukuvi. Ni vita!
Au anataka ku prolong enzi yake?
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,210
2,000
Au anataka ku prolong enzi yake?
Exactly! Kama ambavyo Kikwete alijua wazi Mwandosya akimrithi Urais hatakaa amsikilize kamwe, ndivyo Magufuli anajua kamba Kabudi au Lukuvi wakimrithi Urais hawatakaa wamsikilize kamwe! Kwa hiyo kama vile Kikwete alijua Membe ndie atamwezesha ku-prolong enzi yake, ndivyo ambavyo Magufuli anatafuta kijana wa ku-prolong enzi zake, ila jina bado kaliweka mfukoni.
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,210
2,000
Kwani Kabudi ana nguvu gani huko CCM? Ameshaambiwa wakichemsha watarudishwa walikotoka, na anajijua alikotoka kwani haoni aibu tutaja hadharani mara kwa mara kuhusu alikoibuliwa na kuketishwa na mfalme. Lukuvi hana alikotoka maana hana taaluma yoyote, hakuna taaluma ya ukuu wa mkoa, kwa hiyo hana pa kurudi. Hawa wawili inabidi wawe watiifu tu, hakuna namna.
Kabudi is very very intelligent. Anajua kujishusha ili akwezwe. Hivyo hiyo yote ni strategy. Nimewahi kuwa na Kabudi. He is very calculating. Hivi unaona mtu kama Kabudi kusema yeye ni mtu wa jalalani inaendana na profiling yake ya kuwa presumptuous, flamboyant, cocky na pompous? Anasema hivyo ili kujijenga. Ni strategy ili kumpa confidence Magufuli kuwa ni kitwana wake na pia kuwafanya watu waone ni mnyenyekevu sana. Ndio maana nikasema Kabudi anaweza kujitoa akili na maarifa (wisdom and intelligence) kwa muda mfupi ili kutimiza lengo la muda mrefu.
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,210
2,000
Kwani Kabudi ana nguvu gani huko CCM? Ameshaambiwa wakichemsha watarudishwa walikotoka,
Hewaaa! Hiyo nayo ni strategy ya Magufuli katika kutaka kuwa -tame Kabudi na Lukuvi (kuwadhibiti). Magufuli anajua wazi kwamba anawahitaji watu kama Kabudi na Lukuvi kwenye Baraza la Mawaziri, lakini hataki waanze kupata mawazo (ideas) kwamba kumbe wanaweza sana kazi na hivyo hata Urais wataweza!

Kumbuka Mwandosya alipata wazo la kuwa Rais baada ya watu, ndani na nje ya Tanzania, kuwa wanamwambia alikuwa Waziri makini sana!
 

ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
9,873
2,000
Kwani Kabudi ana nguvu gani huko CCM? Ameshaambiwa wakichemsha watarudishwa walikotoka, na anajijua alikotoka kwani haoni aibu tutaja hadharani mara kwa mara kuhusu alikoibuliwa na kuketishwa na mfalme. Lukuvi hana alikotoka maana hana taaluma yoyote, hakuna taaluma ya ukuu wa mkoa, kwa hiyo hana pa kurudi. Hawa wawili inabidi wawe watiifu tu, hakuna namna.
Jini walilokuwa wanalitegemea na kulisifu sana, sasa limemaliza kula vya kwa majirani limeanza kuwaguguna wa ndani, walewale lililokuwa linawalinda.
Sasa limeshaota pembe, wanaoathirika wasiache waendelee kulishashangilia na kulisifu kwa uthubutu.
 

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
234
500
Mkuu,

Kwa hiyo ndio wamekutuma kuwasemea Kabudi na Lukuvi?

Tangu lini wewe mwenye itikadi kinzani na haumo kwenye mfumo wao hao CCM tamko la Mh Dkt Magufuli likakuumiza sana?

Kilichotokea ni kufinya watu ili watu muanze kujitokeza mkishabikia halafu ndio mwisho wao mtakuwa mmeukamilisha bila kujijua.

Ukitaka kumfahamu mtu vizuri undani wake hasa ambaye ni mkimya na mwenye kuonesha nidhamu tete ni kumfinya ipasavyo

Rais ajaye sio huyo unayemuwaza wewe na wenzio kwa kufuatilia matukio ya watu na harakati zao binafsi.

Tangu mwanzo haumsemi vizuri Mh. Rais Magufuli na siku zote unashabikia ukinzani leo imekuaje badala ya kutafuta mtu mwenye nasaba ya itikadi yako kuliko kupoteza muda kuzungumzia watu wengine kwa mambo ya kubuni na kuonesha malengo yako ni yapi.

Lengo lako ni kuchochea mtafaruku ndani ya CCM kitu ambacho hukiwezi abadani hata jua lishuke. Hao watu unadai watafanya vita ya chini-chini washauri waanze halafu wataishia wapi-jifunze kusoma alama za nyakati hutayumbisha na matamko ya aina yoyote hiyo huwa ni mbinu tu kutaka kujua hisia miongoni mwa makundi ikoje halafu hatua zinachukuliwa bila wewe kujua chochote utashangaa ushabiki wako unakutumbukiza shimoni pasi na tija yoyote. ACHANA na WANASIASA hao ni SAWA na CHAMELEON
 

Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,381
2,000
Kwani Kabudi ana nguvu gani huko CCM? Ameshaambiwa wakichemsha watarudishwa walikotoka, na anajijua alikotoka kwani haoni aibu tutaja hadharani mara kwa mara kuhusu alikoibuliwa na kuketishwa na mfalme. Lukuvi hana alikotoka maana hana taaluma yoyote, hakuna taaluma ya ukuu wa mkoa, kwa hiyo hana pa kurudi. Hawa wawili inabidi wawe watiifu tu, hakuna namna.
I agree!
 

Nzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
13,890
2,000
Kabudi is very very intelligent. Anajua kujishusha ili akwezwe. Hivyo hiyo yote ni strategy. Nimewahi kuwa na Kabudi. He is very calculating. Hivi unaona mtu kama Kabudi kusema yeye ni mtu wa jalalani inaendana na profiling yake ya kuwa cocky na pompous? Anasema hivyo ili kujijenga. Ni strategy ili kumpa confidence Magufuli kuwa ni kitwana wake na pia kuwafanya watu waone ni mneyeyekevu sana. Ndio maana nikasema Kabudi anaweza kujitoa akili na maarifa (wisdom and intelligence) ili kutimiza lengo la muda mrefu.
Mtu wa namna hii hafai kuwa hata Balozi wa nyumba kumi kumi!!
 

msafwa93

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,641
2,000
Rais ajaye ni UMMY MWALIMU..

Lakini hii ni kama ,Rais Magufuli ataachia ngazi muda wake ukiisha..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom