Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Huyu binti ni mateso kwani kauli yake ni matope!
Mie kupenda yeye sasa kanigeuzia kibao kijumla!
Nimemfungulia moyo wangu kwake sasa ni kivuno!
Kumkaribisha kwangu kang'aka tena kwa ghadhabu!
Yawaje sasa kwangu akuite ni kichinjioni?
Yaani hii kauli yake ilinitia majonzi manene...
Nami kufadhaika na kupatwa na kigugumizi..
Sikutarajia kudhalilishwa kwani nampenda vilivyo...
Sikutarajia anikosee adabu hata kunikashifu hivyo..
Yawaje sasa kwangu akuite ni kichinjioni?
Malengo yangu kwake hayana harufu ya utata..
Kumjua haikwepeki, nikikhofu kununua mapanki..
Nia yangu dhahiri kama mtihani atafaulu juu kwa juu.....
Mie siafiki zoezi la kusaili kufanyika bila ya majaribio..
Yawaje sasa kwangu akuite ni kichinjioni?
Moyo wangu wataabika ingawaje yeye aniona vinginevyo..
Kumchumbia siyo hoja na hata trela ningelifungasha
Lakini hii kauli yake kweli yanitia kichefuchefu....
Kumtapika sasa ni lazima na mateso kukaa nayo mbali!
Yawaje sasa kwangu akuite ni kichinjioni?