Yawaje sasa kwangu akuite ni kichinjioni?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,427
911,172
pulsecapM040512_01.jpg
pulsecapM040512_01.jpg

pulsecapM040512_01.jpg
[PHOTO:STANDARD/COURTESY] [h=2]Pulse Cover Girl[/h]


Huyu binti ni mateso kwani kauli yake ni matope!
Mie kupenda yeye sasa kanigeuzia kibao kijumla!
Nimemfungulia moyo wangu kwake sasa ni kivuno!
Kumkaribisha kwangu kang'aka tena kwa ghadhabu!
Yawaje sasa kwangu akuite ni kichinjioni?

Yaani hii kauli yake ilinitia majonzi manene...
Nami kufadhaika na kupatwa na kigugumizi..
Sikutarajia kudhalilishwa kwani nampenda vilivyo...
Sikutarajia anikosee adabu hata kunikashifu hivyo..
Yawaje sasa kwangu akuite ni kichinjioni?

Malengo yangu kwake hayana harufu ya utata..
Kumjua haikwepeki, nikikhofu kununua mapanki..
Nia yangu dhahiri kama mtihani atafaulu juu kwa juu.....
Mie siafiki zoezi la kusaili kufanyika bila ya majaribio..
Yawaje sasa kwangu akuite ni kichinjioni?

Moyo wangu wataabika ingawaje yeye aniona vinginevyo..
Kumchumbia siyo hoja na hata trela ningelifungasha
Lakini hii kauli yake kweli yanitia kichefuchefu....
Kumtapika sasa ni lazima na mateso kukaa nayo mbali!
Yawaje sasa kwangu akuite ni kichinjioni?
 
hahaha,, balaaa dunian ,, sasa utakubalije uyo kimwana akurushe roho? na jengine nn maana ya kununua mapanki? haha ruta watoto wako tele wazuriii, find parfect match f u best :A S thumbs_up: ,atajua thamani yako huyo ikiwa hakuon
 
hahaha,, balaaa dunian ,, sasa utakubalije uyo kimwana akurushe roho? na jengine nn maana ya kununua mapanki? haha ruta watoto wako tele wazuriii, find parfect match f u best
A%20S%20thumbs_up.gif
,atajua thamani yako huyo ikiwa hakuon

wahida mbona unanikatisha tamaa hivyo......nilidhani anatikisa kiberiti tu kumbe ndiyo hanitaki..........
 
Last edited by a moderator:
dah hii ya leo kali anayekuita kichinjio hajakosea kabisa!!kabinti size namba ngapi?nikusaidie maunjanja kijana.

ummu kulthum.....ana 24...............msaada wa haraka unahitajika
 
Last edited by a moderator:
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom