Yatunze Macho Yangu

Yatunze Macho Yangu

SHOOyaKIBABE

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2014
Posts
2,182
Reaction score
1,718
Kulitokea msichana mmoja ambaye hakujipenda kwa kuwa ni kipofu.

Hakumpenda mtu yeyote isipokuwa mchumba wake.
Alisema kama atapata kuona, ataoana na mchumba wake.

Siku moja, mtu mmoja alijitolea macho yake kwa ajili ya msichana huyo na akapona, akawa anaona vizuri kila kitu, hata mchumba wake.
Mchumba wake akamuuliza, "kwa kuwa sasa unaona, tutaoana?"
Yule msichana alishtuka baada ya kuona kuwa hata mchumba wake ni kipofu pia, akakataa kuolewa naye.

Mchumba wake aliondoka akiwa na majonzi tele, na baadaye alimuandikia barua iliyosema - "Yatunze Macho Yangu".


Hivi ndivyo tabia ya binadamu hubadilika kama mambo yakibadilika kwenye maisha yake, ni wachache ambao hukumbuka jinsi maisha yalivyokuwa kabla ya mabadiliko hayo, na huwa pale kwa ajili ya wenzao hata katika wakati mgumu sana.

 
Hii hadithi ya jongoo na nyoka.we mkuu kwa fix....loading error.....
 
haya tuambie mafunzo ya hadithi hii...
 
Ihamishiwe jukwaa la jokes na utani
 
if you can still say "photosynthesis" after drinking, just know that you have wasted your money....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom