Nilikuwa Kipofu, Sasa Ninaona – Haleluya!

Nilikuwa Kipofu, Sasa Ninaona – Haleluya!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,863
Reaction score
7,724
Mara nyingi, ukipoteza kitu ndio unajua thamani yake! Huwezi kujua sana thamani ya macho yako mpaka uwe kipofu kwanza.

Ukipoteza uono, yaani macho yako yasipoweza kuona kwa muda mrefu, kisha ghafla ukaanza kuona tena, ni kama dunia inasherehekea nawe! Nuru inakuingia kwa nguvu, rangi zinacheza mbele ya macho yako kama siku ya tamasha kubwa. Kila kitu kinakuwa kipya kana kwamba kimeumbwa kwa ajili yako tu.

Ni hisia inayoweza kukufanya ulie na kucheka kwa wakati mmoja, kwa sababu safari ya kutoka gizani hadi kwenye mwanga ni tukio la kushangaza. Huo ndio uzuri wa kuona baada ya kutokuona kwa muda mrefu. Ni furaha isiyoelezeka kwa urahisi, na shukrani isiyo na kikomo.

Mimi sio wa kwanza kupitia mabadiliko haya makubwa. Katika Biblia kuna habari ya mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Mtu huyo aliponywa na Yesu kwa muujiza. Kwa furaha na mshangao, akasema: “Nilikuwa kipofu, sasa ninaona” (Yohana 9:25). Tofauti yake na mimi ni kwamba, yeye alikuwa kipofu wa kimwili, lakini mimi nilikuwa kipofu wa rohoni, fikra zangu zilikuwa zimepofushwa na ibilisi.

Kwa sababu ya upofu wa rohoni, matusi, chuki, kusema uongo, vyote hivyo sikuona ubaya wake. Maisha ya uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo sikuona hatari yake, hadi Yesu aliponiondolea upofu wa rohoni. Hiyo ilitokea miaka kadhaa iliyopita, katika mkutano wa Injili. Siku hiyo Yesu alinigusa, akanipa macho mapya ya rohoni. Sasa ninaona nuru yake ang’avu. Natambua waziwazi dhambi ni nini na mshahara wa dhambi naujua. Hiyo ndiyo hali anayokutana nayo kila mtu aliyekuwa dhambini kisha akaokoka.

Yesu alipoingia ndani ya moyo wangu alileta badiliko halisi la maisha. Ukinikasirisha, mimi nacheka tu. Ukinichukia, mimi nakupenda tu. Ukinidharau, mimi nakuhurumia. Ukinitupia mawe, mimi namshukuru Yesu. Haya ndiyo maisha ya kila mtu aliyeokolewa kwelikweli na Yesu.

Asante Yesu kwa kuniokoa. Asante Yesu kwa kuwa sasa ninao uhakika wa kuingia mbinguni.
 
Wewe ambaye bado unaishi gizani - katika upofu wa rohoni, njoo kwa Yesu leo. Yeye ndiye nuru ya ulimwengu. Anangoja kukugusa na kukupa macho mapya. Ataondoa giza lote, na utatembea katika mwanga wake.
 
Na hata kama upofu wako ni wa kimwili, bado Yesu anaweza kuyaponya macho yako. Amekuwa akifanya hivyo tangu zamani, na bado ana nguvu hiyo hiyo hata leo - ukiamini. Haleluya!
 
Na hatimaye umeona chaguo la moyo wako PB au POOR BRAAAIN
Sina mengi zaidi ya kusema setfree ipo siku utasikia maneno yangu
 
Punguza kamba basi mpaka unaboa
We issac77
Hivi unajua maana ya jina lako? Isac maana yake. "Anacheka" au "Atacheka."
Ni ajabu kwamba wewe badala ya kucheka unaboreka🙂
Mimi nilikuwa naboa zamani kabla sijaokoka. Sasa hivi nawafurahisha sana watu kwa sababu nawapa habari za matumaini. Habari za uzima wa milele.
 
We issac77
Hivi unajua maana ya jina lako? Isac maana yake. "Anacheka" au "Atacheka."
Ni ajabu kwamba wewe badala ya kucheka unaboreka🙂
Mimi nilikuwa naboa zamani kabla sijaokoka. Sasa hivi nawafurahisha sana watu kwa sababu nawapa habari za matumaini. Habari za uzima wa milele.
Kumbe unawapa habari za matumaini fine!
 
Wewe ambaye bado unaishi gizani - katika upofu wa rohoni, njoo kwa Yesu leo. Yeye ndiye nuru ya ulimwengu. Anangoja kukugusa na kukupa macho mapya. Ataondoa giza lote, na utatembea katika mwanga wake.
Usitoe rushwa ili upige au usipige kura. Piga 113 kutoa taarifa za rushwa
 
Asante zumbemkuu
I profoundly appreciate your felicitations; indeed, the illumination of my inner being has been nothing short of a transcendent awakening
You're welcome. May your journey ahead continue to shine with clarity and purpose.
 
Walishika msahafu wakatuuza kama watumwa huku wakiwatafuna dada zetu
Walishika biblia wakatutesa kwa viboko na wakaiba rasilimali zetu
 
Dini ni silaha ya kuwamaliza wanadamu maskini
Ndugu yangu Mangwea1900, inaonekana hujajua kwamba kuna dini safi na dini nzuri. Wanaotumia dini kama silaha ya kuwamaliza wanadamu maskini ili kujitajirisha, waliishatajwa zamani katika 1 Timotheo 6:5. Hao hawakubaliki mbele za Mungu kwa sababu hawana dini safi.
Yakobo 1:27 inafafanua kwamba dini safi ni kumsaidia yatima na mjane, na kujilinda na uchafu wa dunia. Hiyo ni kinyume kabisa na silaha ya kuwamaliza wanadamu maskini.
 
Back
Top Bottom