Mtoto halali na hela
JF-Expert Member
- Aug 10, 2012
- 47,707
- 40,918
Habarini za mchana wana jukwaa, ni matumaini yangu kuwa muu wazima na mnaendelea na maandalizi ya kumpokea mtoto Yesu kwa wale wakristo wenzangu. Baada ya kusema hayo nirudi moja kwa moja kwenye mada, binafsi nimepita katika mapito mengi upande wa mahusiano napenda nikiri hilo. Na baada ya kutafakari sana nimeona yatosha kwa kuwa hakuna kitu kigeni kwenye swala la wanawake, ndipo nimechukua uamuzi wa kwenda kucheki afya na kukuta afya yangu bado ni nzuri na namshukuru Mungu. Sasa ni wakati wa kutulia hadi Mungu atakapaponipa mwenza wa maisha, Ee Mungu nisaidie.