Yathibitika: Kutooa au kuolewa ni kaburi la mapema…!

Yathibitika: Kutooa au kuolewa ni kaburi la mapema…!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,442
4fc7afcae8b30.image.jpg

Hivi sasa imethibitika kwamba, watu wasiooa au kuolewa, wanaishi kwa umri mdogo zaidi ukilinganisha na wale ambao wameoa au kuolewa.

Ukweli ni kwamba, taarifa hizi siyo hadithi bali ni ukweli ambao, una vigezo vyenye kuusimamia. Kwa mfano, kwenye jarida la Epidemiology and Community Health la nchini Marekani, imebainishwa kuhusu utafiti ambao, kwa ujumla ulihusisha zaidi ya washiriki 80,000.

Utafiti huo pamoja na tafiti nyingine, zimeweza kuthibitisha kwamba, watu ambao hawajawahi kabisa kuoa au kuolewa maishani mwao, hufa mapema ukilinganisha na wale ambao walioa au kuolewa na kisha kuachana.

Hii ina maana kwamba, ile tabia ya kuingia kwenye ndoa ili kutoa nuksi, ina manufaa zaidi kwa wanaofanya hivyo, kuliko ile ya watu kutooa au kuolewa kabisa maishani mwao.

Kwa nini watu ambao hawajawahi kabisa kuoa au kuolewa wako kwenye hatari ya kufa mapema? Inaonekana kuna sababu kadhaa, lakini kubwa ni pamoja na ile ya kiafya. Kwa kutooa au kuolewa, mtu anakuwa na maisha ya rahisi kuanzia kwenye kula na wakati mwingine hata kutunza afya yake inakuwa ni vigumu.

Ndani ya ndoa watu husaidiana kukumbushana na kujaliana kuhusu afya ya kila mmoja wao. Kuna kuhimizana katika kukagua na kujali afya, bila kujali hali ya kipato ya mtu. Wanaume wanaonekana kuathiriwa zaidi na adhabu hii ya kutooa, ingawa wanawake nao huathirika.

Tafiti nyingi za kutosha zinaonyesha kwamba, watu ambao hawajawahi kuoa au kuolewa, hukabiliwa na matatizo ya shinikizo la juu la damu na lehemu (Cholesterol) ya ziada mwilini. Pengine hii inatokana na ile hali ya mtu kukosa mwenzake wa kusaidiana naye kubeba mizigo ya maisha.

Inaonekana pia kwamba, wale watu ambao, hawajawahi kuoa au kuolewa maishani mwao, hukabiliwa na uwezekano wa kufa kwenye ajali, kuuawa au kujiuwa kwa mara mbili zaidi ukilinganisha na wale ambao wameoa au kuolewa.

Bila shaka wale wanaokufa kutokana na maradhi ya moyo ndiyo wengi zaidi, kwani hufikia asilimia 40 ukilinganisha na wale waliooa au kuolewa. Kwa hiyo upweke na kushindwa kuwa na msaidizi, huenda ni sababu kubwa.

Wale ambao hawajawahi kuoa au kuolewa na wakawa hawana watoto au wakawa hawana ndugu na jamaa wengi wa kuwa nao karibu, hawa hufa mapema zaidi. Walioolewa na kuachwa au waliooa na kuacha, wanakuwa na mtandao fulani, ambao wanandoa huwa nao kwa kawaida.

Tafiti nyingi za siku za nyuma na hivi sasa zinaonnesha kwamba, kutengwa au mtu kukosa watu wa kuwa karibu naye katika masuala ya kijamii, husababisha kifo cha mapema. Ndoa hujenga ukaribu huo kwa sababu, mtu hujiongezea watu wanaomhusu kutoka kwa mwenzake.

Huenda moja ya sababu ya jamii nyingi kusisitiza suala linalohusu kuoa au kuolewa ni hii ya kutaka watu wake waishi zaidi. Inawezekana wana jamii hawajui ni kwa sababu gani wanasisitizwa kuoa au kuolewa, wanajua baadhi ya sababu tu , lakini hii ya kuishi muda mrefu walikuwa hawajaigundua.

Heaven on Earth, Nivea, Neylu, Husninyo, MwanajamiiOne, King'asti, lara 1, miss chagga, miss neddy, Munkari, MankaM, Kaunga, Kongosho, BADILI TABIA, Karucee, charminglady, Elizabeth Dominic, snowhite, AshaDii, Fixed Point, mwaJ, Ruttashobolwa, Kaizer, Asprin, Kiranga, Nyani Ngabu, The Boss, ayanda, mayenga, Arushaone, Mr Rocky, PakaJimmy, kabanga, Thomas Odera, Mentor, Ukwaju, sweetlady, Preta, Asnam, Elli, Lisa, miss strong, Tina, sister, Ennie, Paloma, Sista
 
Ndoa ni muhimu kwa kweli ndo mana naonaga ambao wameoa au kutokuolewa wanakuwa na stress
 
Ndoa ni muhimu kwa kweli ndo mana naonaga ambao wameoa au kutokuolewa wanakuwa na stress

Samahani mkuu sijui hapo kwenye bold ulikuwa unamaanisha nini? hebu zingatia kwenye rangi nyekundu....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
NAtamani nimtolee mahari tena mke wangu, kha! Sijui hawa Wabondei watataka bei gani this time, MANI njoo hapa unishauri. Asante Mpwa wangu Mtambuzi nimeisoma kwa ufasaha sana na nimepata neno
 
Last edited by a moderator:
Mmmmh... Lakini mkuu Mtambuzi ukiangalia mapadri wengi bado wana nguvu na afya tele ukilinganisha na watu wa rika lao.

Wanadai kuwa stress za familia zinawafanya walio na familia kuzeeka mapema na kuchoka kulinganisha na wao.

Hili unalizungumziaje!
 
Tutadai mara mbili ya mwanzo
 
Last edited by a moderator:
Mmmmh... Lakini mkuu Mtambuzi ukiangalia mapadri wengi bado wana nguvu na afya tele ukilinganisha na watu wa rika lao.

Wanadai kuwa stress za familia zinawafanya walio na familia kuzeeka mapema na kuchoka kulinganisha na wao.

Hili unalizungumziaje!
Wale ambao hawajawahi kuoa au kuolewa na wakawa hawana watoto au wakawa hawana ndugu na jamaa wengi wa kuwa nao karibu, hawa hufa mapema zaidi. Walioolewa na kuachwa au waliooa na kuacha, wanakuwa na mtandao fulani, ambao wanandoa huwa nao kwa kawaida.

Hebu soma hapo kwenye bold halafu weka kwa kinyume chake.

Utafiti umebainisha kwamba sababu za kufa mapema, zinazotokana na kutooa au kuolewa, mojawapo ni upweke na kutokuwa na mtu wa kusaidiana kubeba mizigo ya maisha na kukumbushana kuhusu afya zetu.....

Hao Mapadri unaowazungumza wanahudumiwa kwa kiwango cha juu na wamezungukwa na masista wanaowahudumia kwa karibu sana, ina tofauti gani na mtu aliyeoa kama unaangalia swala la kuhudumiwa?

Sema tu kinachokosekana ni tendo la ndoa ambao halikuhusishwa katika utafiti huu kama ni chanzo cha kusogeza uhai.
charminglady usiniangushe bana hebu soma mada yangu between the line......... LOL
 
Tutadai mara mbili ya mwanzo
Bora ungefanya mara nne, maana mahari ya wabondei ni rahisis sana ukilinganisha na ya wapare, miye kule upareni niligongwa milioni aisee tena baada ya kuomba sana punguzo, kwani nilipigiwa hesabu ya ng'ombe 10, hebu piga hesabu ya bei ya ng'ombe kwa bei ya miaka kumi iliyopita
 
probably no .. probablly yes.... ni ndoa chache sana ambazo zinaweza pelekea kuishi maisha marefu... ntingi ni stress na presha sijui lakini i will try to pay my card well... bibi kidude mbona kaishi mda bila hiyo ndoa lakini kaishi sana... any way
 
nikweli na ndo maana micba ming ya wanaokufa ni mapadri na masista c ndio?
 
Nadhan itaaplay kwa zile ndoa zenye aman na upendo
Kama ni full stress utaishi miaka mingi?
 
"Marry, and you will regret it;
don't marry, you will also regret it;
marry or don't marry, you will regret it either way.

Laugh at the world's foolishness, you will regret it;
weep over it, you will regret that too;
laugh at the world's foolishness or weep over it, you will regret it either way;
laugh at the world's foolishness or weep over it, you will regret both.

Believe a woman, you will regret it;
believe her not, you will also regret it;
believe a woman or believe her not, you will regret it either way;
believing a woman or not believing her, you will regret it both ways.

Hang yourself, you will regret it;
do not hang yourself, and you will regret that too;
hang yourself or don't hang yourself, you'll regret it either way;
whether you hang yourself or do not hang yourself, you will regret both.

This, gentlemen, is the essence of all philosophy."

― Søren Kierkegaard, Either/Or: A Fragment of Life
 
probably no .. probablly yes.... ni ndoa chache sana ambazo zinaweza pelekea kuishi maisha marefu... ntingi ni stress na presha sijui lakini i will try to pay my card well... bibi kidude mbona kaishi mda bila hiyo ndoa lakini kaishi sana... any way
miss chagga, hebu soma majibu yangu kwa charminglady, huyo Bi Kidude alikuwa amezungukwa na Marafiki, ndugu, vijukuu, vitukuu na vilembwe, hakuwahi kuwa mpweke kutokana na kuwa na nasaba nyingi
 
Last edited by a moderator:
nikweli na ndo maana micba ming ya wanaokufa ni mapadri na masista c ndio?
Acha ubishi, soma mada yangu yote, usikurupuke haya mambo yamefanyiwa utafiti na unachotaka kuwaaminisha wasomaji hapa ni upotoshaji wa kile nilichaoandika.

Kuwepo kwangu hapa JF kumenifundisha mengi, watu wengi hapa hawapo tayari kusoma mada na kuielewa bali hukimbilia kubisha kwa kusoma kichwa cha habari na kuanzisha ubishi usio na maana.

Kwa hiyo sijashangazwa na ulichokisema.
 
Nadhan itaaplay kwa zile ndoa zenye aman na upendo
Kama ni full stress utaishi miaka mingi?
Kuna utafiti nimeusoma na nitauweka hapa umebainisha kwamba ndoa imara huponya hata kansa.....
Lakini utafiti huu uko tofauti kidogo, hapa hata wale waliooa au kuolewa wakaachana wanaweza kuwa na umri mkubwa suala hapa ni kutokuwa na upweke kutokana na kuongeza nasaba kutoka upande wa pili wa mwenzi wako. kumbuka hata kama wanandoa wameoana na kuchana bado ule mtandao wa ndugu na marafiki walioutengeneza hauwezi kufa labda tu utapungua, lakini unaweza kuwa mzuri na imara kiasi cha kuwapa faraja na hivyo kuongeza umri wa kuishi
 
probably no .. probablly yes.... ni ndoa chache sana ambazo zinaweza pelekea kuishi maisha marefu... ntingi ni stress na presha sijui lakini i will try to pay my card well... bibi kidude mbona kaishi mda bila hiyo ndoa lakini kaishi sana... any way

Alichosema mtambuzi kimefanyiwa utafiti acha ubishi!! .Hata TZ tukifanya utafiti matokeo ni hayohayo tena yatakuwa worse
 
Back
Top Bottom