Yatakayojiri Bungeni Septemba 2016

Yatakayojiri Bungeni Septemba 2016

dostum

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
215
Reaction score
110
Kukosekana kwa baadhi ya vichwa ktk bunge lijalo la Sep 2016 tutakosa mengi mazuri.

Labda niseme tu huenda ilipangwa kuwaondoa, kwani ukisikia adhabu walizopewa na ukilinganisha makosa walofanya utaona hakuna uwiano.

Kuna ule msemo wa 'funika kombe mwanaharamu apite' . Maana ya ndani kabisa ya msemo huu ni kukubali kufanya au kufanyia jambo usilo lipenda ili kizuia hatari balaa au madhara zaidi.

Kamati ya bunge ya
PAC na LAAC kwenye kikao cha bunge mwezi sep 2016, Pamoja na taarifa nyingine pia itajadili MABILIONI YA Posho walizojimegea baadhi ya watumishi kama HAKI yao ya msingi kwao.

Mfano, Mamlaka ya Ustawishaji Mji wa Dodoma (CDA) mwaka 2015 ilitumia Sh. milioni 124 kwa kufanya vikao sita pekee.

Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambayo mwaka 2015 ilitumia Sh. milioni 250 kwa ajili ya vikao.

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imetumia Sh. bilioni 15 kwenye shughuli za uendeshaji kiasi kikubwa kikiwa ni posho.

Katika hesabu za bodi hiyo, baadhi ya posho zilizowakera wabunge hao ni pamoja na ile iliyopewa jina la posho nyinginezo (other payroll allowance) ambayo mwaka ulioishia Juni 30, ilitumika Sh. milioni 999.45

Posho nyingine inayoitwa posho maalum (special allowance) kwa mwaka 2015 ilikuwa Sh. milioni 582.05.

Posho nyingine iliyoishtua kamati hiyo ni ile ya mahusiano na ukarimu (relationship and hospitality) ambayo kwa mwaka 2015 ilikuwa Sh. milioni 296.77


Jumla ya posho kwa taasisi tatu pekee ni 17bl.

Ukisoma taarifa yote utagundua kuwa kuwa umuhimu wa huyu jamaa ashirikiane na wale anaowaona ni maaduli ili kuirejesha nchi kwenye mstari kwani Kuwa waluokunnywa maji ya bendera wataona hizi ni porojo tu.


Source

Ukawa waja na siri nzito bungeni
 
Magufuli amelithibiti bunge
Hakuna haja ya kufatilia bunge siku hizi

Huwez ukawa unafatilia mawazo ya aina moja
 
Bunge lenyewe kwanza hata hatuoni tena LIVE imebaki story tuu!

Bunge kutokuwa LIVE plus yule dada akikaa kwa kiti plus kukosekana kwa baadhi ya wabunge basi tena bunge linakosa makali yake ni bora liende.
 
Napendekeza IGP apige marufuku na hili BUNGE maana ni MKUTANO WA WANASIASA pia. Kama ameweza kuzuia ile ya nje na ndani hata hili anaweza.

Hili Bunge linakula pesa za walipa kodi halafu wanapitisha MISWADA ya KUMKANDAMIZA huyu mlipa kodi & maskini. Mfano; mambo ya fao la kujitoa, na kodi za mihamala, nk

Kwa uzalendo ule ule wa mwezi uliopita, ewe IGP piga pini huu MKUSANYIKO.

Wamekuwa watukanaji, wasioheshimiana & waliokosa uzalendo.
 
Wafuasi wa chadema wana comment kama wamekunywa viroba
 
Ngoja tusubiri...ila nilimsikia kiongozi wa waliosusa bungeni akisema wanafuata maelekezo ya ''viongozi wa dini''
 
nchi inaendeshwa kwa kauli za mtu1...........yeye ndo hakimu,polisi,tulia,
tutaona mengi
 
Hivi hamkujiandaa siku zote iyo mitambo yenu mpaka ikate kate kila mda tulitegemea msomi ayoub rioba utarudisha tbc enzi za tido lakini wapi mnatia aibu Bunge limeanza leo lakini hatuoni kitu
 
Hivi hamkujiandaa siku zote iyo mitambo yenu mpaka ikate kate kila mda tulitegemea msomi ayoub rioba utarudisha tbc enzi za tido lakini wapi mnatia aibu Bunge limeanza leo lakini hatuoni kitu
cc nape nnauye
 
TBC ni ovyo.Tunataka bunge live.Majibu yao watayapata 2020#Kuminya upatikanaji wa habari
 
Bunge halionyeshwi LIVE mpaka owner wa Bunge atake
 
Hizo nguo nyeusi mlizovaa watu wa ukawa huko bungeni kuna msiba wa Nani?
 
Hivi hamkujiandaa siku zote iyo mitambo yenu mpaka ikate kate kila mda tulitegemea msomi ayoub rioba utarudisha tbc enzi za tido lakini wapi mnatia aibu Bunge limeanza leo lakini hatuoni kitu


!
!
Lengo ni kulifumba mdomo bunge. Kipindi kile ungehamisha tu chaneli ila kwa sasa hakuna kuangalia bunge.
Nauona mpango wa kuwa na idara ya uchapishaji wa bunge amvayo itslazimisha watu wa magazeti nao kuchukua habari toka kwenye ofisi yao miaka kadhaa ijayo.
 
Tatizo sio Riyoba Mkuu. Ndio system yenyewe hiyo!
 
Tanzania ya viwanda. Mtambo bado unatengenezwa kiwandani. Kuweni na subra
 
Back
Top Bottom