Yas Yaendeleza Mapinduzi ya Kidigitali kwa Wakulima Kupitia Mpango wa Mikopo ya Simu Janja

Yas Yaendeleza Mapinduzi ya Kidigitali kwa Wakulima Kupitia Mpango wa Mikopo ya Simu Janja

News TZ

Senior Member
Joined
Jun 17, 2015
Posts
169
Reaction score
88
JOM_3547.JPG

Dodoma, Agosti 2025 – Kampuni ya mawasiliano ya Yas imeendelea kuonesha dhamira yake ya kuleta mabadiliko ya kidigitali kwa wakulima kwa kuendeleza mpango wa Device Financing, unaowawezesha wakulima kumiliki simu janja kwa gharama nafuu kupitia malipo ya awamu. Kupitia mpango huu, mkulima anaweza kuanza kutumia simu janja kwa kulipa kuanzia shilingi 1,400 kwa siku kwa kipindi cha miezi sita.

Akizungumza wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, Meneja wa Yas Kanda ya Kati, Bw. Frank Anthony, alisema kuwa mpango huu umetengenezwa mahsusi kwa ajili ya wakulima wa vijijini na wenye kipato cha chini ambao wanahitaji teknolojia ili kuimarisha shughuli zao za kilimo lakini wanakumbwa na changamoto ya gharama za vifaa.

“Katika ulimwengu wa leo wa kidigitali, simu janja si kifaa cha anasa. Ni nyenzo muhimu inayowawezesha wakulima kupata taarifa za hali ya hewa, bei za mazao, masoko, na elimu ya kilimo kwa njia ya mtandao,” alisema Frank Anthony.

Simu zinazotolewa kupitia mpango huu zinakuja tayari zikiwa zimeunganishwa na huduma ya intaneti ya kasi na zimeunganishwa na huduma za kifedha kupitia Mixx by Yas. Kwa njia hii, wakulima wanaweza kufanya miamala ya kifedha, kushiriki kwenye vikundi vya mafunzo ya kilimo mtandaoni, na kutumia fursa nyingine nyingi za kidigitali kuboresha maisha yao na shughuli zao.

“Mpango huu unawasaidia wakulima kuwa sehemu ya mapinduzi ya kidigitali – kutoka kuuza mazao hadi kupata elimu ya mbegu bora na mbinu za kisasa za kilimo. Tunapunguza pengo la kidigitali na kuhakikisha kila mkulima anapata fursa sawa ya kujifunza, kuwasiliana na kujiendeleza,” aliongeza.

Kwa ujumla, hatua hii ya Yas inalenga kuwainua wakulima, hasa waliopo vijijini, kwa kuwapa zana ya msingi ya teknolojia ili waweze kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia matumizi ya simu janja.
 
Back
Top Bottom