Yapi madhara ya gari kukaa muda bila kutumika?

Kazwala mkuu

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,034
2,249
Wakuu salaam

Nimefikia kuuliza hivyo mara baada ya kuacha gari yangu aina ya Gx 100 Cresta vvti engine, kwa muda mrefu sana ila sasa nikarudi rasmi nianze kuitumia.

Nilibadilisha oil zote na filter pamoja na mipira na nikaanza kuitumia, awali ilikuwa inaonyesha matatizo kama imekufa mabush lakini mara baada ya kupiga trip ndefu za mikoa ikakaa sawa yenyewe na kurudi kama mpya ila tatizo ambalo haliondoki ni kutoa moshi mweupe muda wote.

Awali nilipoiweka haikuwa na tatizo hilo ila kwa sasa baada ya kuitoa ndipo nikaliona hilo.

Sijaifungua kwa fundi yeyote bado maana sikutaka kukurupuka, wapo walioniambia inaweza kuwa sababu ni kukaa sana hivyo moshi utakata wenyewe, wapo walioniambia inaweza kuwa piston ring zimeanza kufa na pia wapo wanaosema ni valve seel zimekakamaa.

Hapa kuna wataalam wabobezi, naomba ushauri juu ya hili inaweza kuwa ni nini na kipi kifanyike?

Natanguliza shukrani.
 
si unihonge gari moja mkuu unapaki gari wakati wenzio tunaumia kwenye lift?
Najua bado unanipenda ila ni bwana yule tu kaingilia mapenzi yetu, ningekupa moja ila zote ni six cylinders hivyo roho itaniuma wengine wakikuhonga mafuta Upo lakini weye? ngoja nisubiri mafundi wetu wanipe somo kidogo.
 
bwana gani tena? mimi sina bwana
 
Gasket ya kuzuia oil isiingie kwenye combustion chamber itakuwa imeisha,au ina crake,,so kinachotokea hapo ni kuwa engine inachoma mafuta na oil

Badilisha cylinder head gasket..
Ni dm nkupatie huduma chap, nakufata popote kma upo dsm lkn.
 
Wakuu salaam

Nimefikia kuuliza hivyo mara baada ya kuacha gari yangu aina ya Gx 100 Cresta vvti engine, kwa muda mrefu sana ila sasa nikarudi rasmi nianze kuitumia.

Nilibadilisha oil zote na filter pamoja na mipira na nikaanza kuitumia, awali ilikuwa inaonyesha matatizo kama imekufa mabush lakini mara baada ya kupiga trip ndefu za mikoa ikakaa sawa yenyewe na kurudi kama mpya ila tatizo ambalo haliondoki ni kutoa moshi mweupe muda wote.

Awali nilipoiweka haikuwa na tatizo hilo ila kwa sasa baada ya kuitoa ndipo nikaliona hilo.

Sijaifungua kwa fundi yeyote bado maana sikutaka kukurupuka, wapo walioniambia inaweza kuwa sababu ni kukaa sana hivyo moshi utakata wenyewe, wapo walioniambia inaweza kuwa piston ring zimeanza kufa na pia wapo wanaosema ni valve seel zimekakamaa.

Hapa kuna wataalam wabobezi, naomba ushauri juu ya hili inaweza kuwa ni nini na kipi kifanyike?

Natanguliza shukrani.

1.Gari uliipaki kwa muda gani kabla ya kurudi na kuanza kuitumia tena? 2.Una uhakika ulipoiacha hakuna mtu aliigusa? 3. Moshi mweupe unaotoka hutoka kwa muda gani? Ukipiga start unaanza kutoka na haukati hata utembee Km 5 bila ya kusimama? 4. Moshi unaotoka unaacha unyevunyevu wa Oil inayoonekana kwenye Bomba la Moshi la Gari yako au Bomba linabakia kavu pamoja na Moshi kutoka? 5. Gari ni Manual au Auto? Nijibu maswali haya nikueleze tatizo la Gari yako.
 
Kabla ujahitaji info zote izo inabid uwe na self diagnosis Kujua tatizo. Nini kinasabababisha moshi mweupe kutoka.
Sasa maswala ya kuuliza una uhakika kama mtu aliendesha or not, sijui transmission yake ni auto au manual sasa transmission na engine wapi na wapi.
But anyway wewe ni fundi mzuri nimeelewa maelezo
Mkuu uthibitishie Umma
 
Gasket ya kuzuia oil isiingie kwenye combustion chamber itakuwa imeisha,au ina crake,,so kinachotokea hapo ni kuwa engine inachoma mafuta na oil

Badilisha cylinder head gasket..
Ni dm nkupatie huduma chap, nakufata popote kma upo dsm lkn.
Mkuu,ikichoma Mafuta na oil,moshi unatoka mweusi pia kwenye exhaust pipe panakuwa na unyevunyevu wa oil.kama Niko wrong nirekebishe.
 
Kabla ujahitaji info zote izo inabid uwe na self diagnosis Kujua tatizo. Nini kinasabababisha moshi mweupe kutoka.
Sasa maswala ya kuuliza una uhakika kama mtu aliendesha or not, sijui transmission yake ni auto au manual sasa transmission na engine wapi na wapi.
But anyway wewe ni fundi mzuri nimeelewa maelezo
Samahani mkuu kama nimekukwaza na maswali yangu, nilikuwa na nia njema tu ya kutoa mchango wangu kutokana na kuhitaji kwako msaada kuhusu Gari lako, lakini naona yamekuja majibu ambayo sikuyatarajia. Niwie radhi.
Zaidi ya haya pia kutoka sasa inabidi utambue kuna uhusiano mkubwa, mkubwa sana kwa aina hizi 2 za Gear box, Manual na Auto kwenye maisha ya Engine ya Gari.
 
Gasket ya kuzuia oil isiingie kwenye combustion chamber itakuwa imeisha,au ina crake,,so kinachotokea hapo ni kuwa engine inachoma mafuta na oil

Badilisha cylinder head gasket..
Ni dm nkupatie huduma chap, nakufata popote kma upo dsm lkn.
Akhsante mkuu kwa kunipa njia, je haihusiani na piston ring?
 
1.Gari uliipaki kwa muda gani kabla ya kurudi na kuanza kuitumia tena?

NILIIPAKI KARIBU MIEZI SABA

2.Una uhakika ulipoiacha hakuna mtu aliigusa?

NINA UHAKIKA MKUU

3. Moshi mweupe unaotoka hutoka kwa muda gani?
PALE GARI NITAKAPOIKANYAGIA SANA AU KWA FUJO, MUDA MWENGINE INATULIA SAFI ILA MUDA MWENGINE UNATOKA TU NIKIWASHA GARI

Ukipiga start unaanza kutoka na haukati hata utembee Km 5 bila ya kusimama?

WAKATI MWENGINE HAUTOKI ILA IKITOKEA UKATOKA HAUKATI

4. Moshi unaotoka unaacha unyevunyevu wa Oil inayoonekana kwenye Bomba la Moshi la Gari yako au Bomba linabakia kavu pamoja na Moshi kutoka?

BOMBA KAVU

5. Gari ni Manual au Auto?

AUTO
Nijibu maswali haya nikueleze tatizo la Gari yako.
NASUBIRI USHAURI MKUU WANGU
 
Samahani mkuu kama nimekukwaza na maswali yangu, nilikuwa na nia njema tu ya kutoa mchango wangu kutokana na kuhitaji kwako msaada kuhusu Gari lako, lakini naona yamekuja majibu ambayo sikuyatarajia. Niwie radhi.
Zaidi ya haya pia kutoka sasa inabidi utambue kuna uhusiano mkubwa, mkubwa sana kwa aina hizi 2 za Gear box, Manual na Auto kwenye maisha ya Engine ya Gari.
Mkuu aliyekujibu ni mdau na siye mwenye gari, mimi ndiye mwenye tatizo nipe mwanga kaka nimeshakujibu maswali yote.
 
Moshi mweupe ni dalili kuna oil inaunguzwa kwenye piston chamber. Kama ni mwingi na bomba linakuwa bichi (exhaust pipe) basi ni muda wa kubadili piston ring ( mara nyingi 200,000 km)
Kama ni moshi kidogo na hauna mwendelezo itakua ni valve seals zimeathirika kutokana na "tension" ya kukaa muda mrefu bila kulainishwa na oil. Hilo lz valve seals ndo nahisi tatizo lako, sio kubwa sana
 
Back
Top Bottom