Yanga yapigwa faini na CAF

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
15,191
20,158
Tukisema hii timu ni kihuni inaendeshwa kama timu za ndondo wanakuja juu na kulalamika wanaonewa.

======

1634042521108.png

SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limeipiga faini ya Sh11 milioni klabu ya Yanga baada ya kushindwa kujibu madai ya kuwafanyia fujo baadhi ya watu waliokuwa kwenye msafara wa Rivers United ya Nigeria.

Malalamiko hayo yametokana na mechi ya hatua ya awali iliyochezwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam Septemba 12 na Yanga kupoteza kwa bao 1-0, ambapo kupitia mitandao ya kijamii ya timu hiyo walilalamika kupigwa kwa watu mbalimbali akiwemo Ofisa habari wa timu hiyo, Charles Mayuku. Rivers United walipeleka malalamiko hayo CAF na kupitia mtandao wao wamethibitisha kupokea malalamiko hayo.

Pia CAF wamesema mechi hiyo haikutakiwa kuwepo mashabiki ila walibaini baadhi ya mashabiki uwanjani.CAF ilituma malalamiko hayo kwa Yanga kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), na wamesema hakukuwa na mrejesho wowote kutoka kwenye Shirikisho hilo. Kutokana na hilo bodi ya nidhamu imeipiga faini Yanga kiasi cha 5,000 USD sawa na Sh11 milioni za kitanzania
Mwaka 2016 timu hiyo ilipigwa faini kwa makosa mengine.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF),limeipiga faini ya dola 5,000 Klabu ya Young African kwa kosa la kuchelewesha mchezo baada ya wachezaji wake.

Kumzonga mwamuzi wakati mchezo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya GD SagradaEsperanca uliofanyika Angola Mei 18, 2016.
 
CAf walipokea malalamiko kutoka Rivers na wakataka ufafanuzi kutoka Tff juu ya malalamiko ya Rivers.

Kwamujibu wa CAF Tff hawakuwajibu chochote kwaiyo CAF wamerudi na adhabu ya Dola 5000 kwa Yanga.

Sasa Tff haijulikani Kama wali wasiliana na Yanga juu ya tuhuma izo maana CAF wametoa adhabu kwakua Tff haikutoa ushirikiano walipoulizwa juu ya malalamiko ya Rivers.

Vilevile Tff imeonywa baada ya kutokea malalamiko kutoka timu mbalimmbali za mataifa na vilabu mbalimmbali vinavyo kuja nchini kucheza mechi zimekua zikikutana na mambo ya hovyo kwenye Corona test na mambo ya ajabu katika vyumba vya kubadilishia nguo na kuingiza mashabiki wengi kuliko idadi waliyo elekezwa. Kamati iyo ya nidhamu ilikaa na kupitia malalamiko ya nchi na vilabu mbalimmbali barani Africa
 
Lawama ziirudie Simba kufanikisha kuipatia nafasi ya Kimataifa Vyura..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
Simba ndio timu iliyo Lengwa kwenye tuhuma za kupulizia madawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo Ila kwakua uko nyuma CAF walishapokea malalamiko kutoka katika vilabu mbalimmbali.

CAF walicho fanya ni kuionya TFF juu ya malalamiko ambayo wamekua wakipata kutoka katika vilabu mbalimmbali vinavyo kuja nchini dhidi ya timu zetu.
 
Mlikuwa wapi mikia siku hizi mnakosa tittle mnakujs na topic za ovyo ebu chezeni mpira timu lenu limeharibika juu ya mawe 😂😂
 
Simba ndio timu iliyo Lengwa kwenye tuhuma za kupulizia madawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo Ila kwakua uko nyuma CAF walishapokea malalamiko kutoka katika vilabu mbalimmbali, CAF walicho fanya ni kuionya TFF juu ya malalamiko ambayo wamekua wakipata kutoka katika vilabu mbalimmbali vinavyo kuja nchini dhidi ya timu zetu.
Faini upigwe wewe ila Simba ndio mlengwa.
Aseeee
 
Wanapitaje najua, wanashindaje najua, na nitatumia kujua kwangu kuwaonesha kwamba na mimi najua

Kabla ya mechi ya riverside tulipata kuona short clip ikionesha benchi la ufundi la yanga likika chini na manara kuzungumza namna ya kushinda mechi wanayo i-face kwakua manara alidai kujua mbinu zote walizokua wakitumiwa club bingwa kushinda mechi

Clip ilikua fupi hatukuelewa kilicho jadiliwa na kilikubalika vipi, na mbinu ipi ya manara aliyo propose, ila baada ya mechi tuliwaona wachezaji wa rivers wakiwa na majeraha ya kichwa ambayo yalikuwa mabichi kabisa

Unaweza ukaona ni mbinu gani ambayo ofsa manara aliwapa benchi la ufundi, na hii ndo outcome yake sasa
 
Lawama zangu nazipeleka kwa TFF, Maana ndio imewazoesha huu mtindo wa kuwapiga faini ndogo kila mwaka hadi wamezoea hizi tabia.

Hata kule Nigeria nasikia waliruka ukuta ili kuingia uwanjani pia waligoma kuingia vyumbani, Na msemaji wao alitoa taarifa kuwa HATUCHEZI hadi walipobembelezwa na kupewa Pipi ndio wakakubali kuingiza timu uwanjani.

Pia wanatabia ya Kuvunja nazi na madafu getini kila wanapocheza mechi.
 
Simba ndio timu iliyo Lengwa kwenye tuhuma za kupulizia madawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo Ila kwakua uko nyuma CAF walishapokea malalamiko kutoka katika vilabu mbalimmbali, CAF walicho fanya ni kuionya TFF juu ya malalamiko ambayo wamekua wakipata kutoka katika vilabu mbalimmbali vinavyo kuja nchini dhidi ya timu zetu.
Yanga wamecheza mechi moja tu wamelimwa faini Simba mwaka jana ilicheza mpaka robo fainali lakini hatukusikia hata onyo
 
Simba ndio timu iliyo Lengwa kwenye tuhuma za kupulizia madawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo Ila kwakua uko nyuma CAF walishapokea malalamiko kutoka katika vilabu mbalimmbali, CAF walicho fanya ni kuionya TFF juu ya malalamiko ambayo wamekua wakipata kutoka katika vilabu mbalimmbali vinavyo kuja nchini dhidi ya timu zetu.
Aliewaitaga nyani hakukosea kabisa mna ujinga sana washabiki wa uto..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom