Udhamini wa Kampuni ya Bia, TBL, kwa klabu mbili tu za Yanga na Simba haujalenga kukuza soka la Bara. TBL walitakiwa kupeleka udhamini wao katika klabu changa zinazoundwa na wachezaji chipukizi.(Jambo wanalolifahamu)
Timu za Simba na Yanga hazikustahili kupewa udhamini wa TBL kwa kuwa hazizalishi wachezaji wake zenyewe na badala yake zimekuwa zikichukua wachezaji kutoka katika klabu changa,
Simba na Yanga zimekuwa zikichuma wachezaji kutoka timu kama za Manyema, Ashanti United na Pan African za jijini Dar es Salaam, AFC ya Arusha na Kagera Sugar ya Bukoba.
Simba imesajili wachezaji watano kutoka Ashanti United na mmoja Pan African, wakati Yanga ina wachezaji watatu kutoka Kagera Sugar kwa ajili ya msimu ujao.
``Huu ni mradi wa wakubwa wanaotaka kufanya biashara zao lakini hizi timu hazistahili kupewa udhamini,``alisema na kueleza zaidi, ``hazijui kutengeneza wachezaji wao... zinasubiri zitengenezewe ndio ziwasajili.``(Huu kama sio Ufisadi ni nini?hata kwenye kusaini mikataba ya udhamini ukiangalia Mafisadi wa Simba na Yanga waliokuwepo ndo ungejua kwamba huu ni wizi mkubwa)
TBL haikuzitendea haki timu nyingine 10 zinazoshiriki ligi kuu ya Bara kwa kutoa fedha kwa Simba na Yanga tu. miongoni mwa timu 10 zilizobaki zipo zenye uwezo mkubwa kuonyesha kandanda safi uwanjani, tofauti na vigogo hivyo ambavyo vimezoea kulalamika mara kwa mara.