Yanga vs Azam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanga vs Azam

Discussion in 'Sports' started by saitama_kein, Mar 30, 2011.

 1. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wadau tupenae uhondo live wa mechi kati ya Yanga na Azam.......
   
 2. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Tujikaze tuifunge Yanga
  KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Azam, Ramadhan Chombo 'Redondo' amewataka wachezaji wenzake kujituma kwenye mchezo wao wa leo wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga kwa lengo la kupata ushindi na kujihakikishia nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya CAF hapo mwakani.

  Chombo aliyejiunga na Azam FC akitokea klabu ya Simba msimu uliopita aliliambia Mwananchi jana jijini Dar es Salaam kuwa anawataka wachezaji wenzake kuupa umuhimu mkubwa mchezo huo ili waweze kushinda na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya shirikisho (CAF) hapo mwakani.
  "Nafikiri endapo tutaweza kuishinda Yanga kwenye mchezo huu tutakuwa tumejiweka katika nafasi nzuri ya kumaliza msimamo katika nafasi ya pili na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya CAF."

  "Mchezo utakuwa mgumu ukizingatia, wenzetu wanaitaka nafasi ya pili ama kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa msimu huu, ni kujituma kwa nguvu zote ili kuweza kuibuka na ushindi,"

  "Nafasi ya kutwaa ubingwa tunayo endapo tutamfunga Yanga na Simba akipoteza mechi mbili, lolote linaweza kutokea kwenye mpira," alisema Chombo.

  Azam inashikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 37 baada ya kushukua dimbani mara 19 huku Yanga ikishika nafasi ya pili na pointi 40 kwa michezo 19 wakati Simba inaongoza ikiwa na pointi 44 kwa mechi 19 iliyocheza mpaka sasa.

  Source: Mwananchi
   
 3. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  MABINGWA mara 17 wa Tanzania Bara, Yanga leo inashuka dimbani kuikabili Azam FC katika harakati zake za kusaka ubingwa msimu huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

  Yanga iliyokusanya pointi 40 ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Simba kwa pointi tano wanajua endepo watapoteza mchezo huo wa leo ndoto yao ya ubingwa itakuwa shakani zaidi ya kugomea nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho pamoja na Azam.

  Kocha wa Yanga, Sam Timbe alisema kuwa mchezo wa leo ni mgumu kutokana na mvutano wa pointi uliopo katika ligi hiyo hasa katika timu hizo tatu za juu zinazogombea kuchukua ubingwa au nafasi ya pili.

  ''Najua Azam ni timu nzuri wenye wachezaji bora, lakini mechi hiyo ni muhimu kwetu tushinde ilituweze kuifukuzia Simba katika harakati za kuchukua ubingwa kwani tukipoteza mchezo huo itakuwa ngumu kuchukuwa ubingwa msimu huu,'' alisema Timbe.

  Yanga imebakiza mchezo na Azam leo, Toto na African Lyon, lakini Timbe alisema mechi hizo ni ngumu kwa kuwa timu zote zinapigana kucheza kufa na kupona kuhakikisha inashinda mechi zake.

  Akizungumza na Mwananchi makao makuu ya klabu hiyo jana, Timbe alisema ni vigumu kubashiri timu yake kuchukua ubingwa kutokana na upinzani uliopo wakati wapinzani wao Simba wanashikilia kilele na wanataka kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa mara mbili mfululizo.

  "Ligi ya Tanzania ni ngumu kutokana na uchache wa timu zinazoshiriki, timu 12 ni chache sana, zingekuwa zinashiriki timu 20 sasa hivi tungekuwa tunamechi nyingi bado za kucheza, wala tusingekuwa na presha ya kutwaa ubingwa, lakini kwa mfumo huu wa ligi ni mgumu kusema unachukua ubingwa."

  "Itakuwa ni furaha Simba wakipoteza mechi zao zilizosalia ingawa najua lakini hii ni soka chochote kinaweza kutokea, ningependa kuona nashinda mechi zangu zote zilizobaki na wapinzani wangu wakipoteza nadhani itakuwa njia nzuri ya sisi kuchukua ubingwa."alisema kocha huyo raia wa Uganda.

  Naye Kocha wa Azam, Stewart Hall alisema kuwa anajua kuwa anacheza na timu kubwa na yenye wachezaji wazoefu na mashabiki wengi, lakini kwa upande wake haogopi hilo.

  Alisema anajiamini kushinda mchezo huo kutokana na kuwa na safu nzuri ya ushambuliaji ambayo inaweza kuiletea madhara Yanga.Stewart alisema mchezo huo ni muhimu sana kwao kushinda iliwaweze ujiakikishia kuchukua nafasi ya pili kwani siku zote michezo ya mwisho ndio inakuwa migumu sana kwani kila mmoja anataka amalize ligi hakiwa katika nafasi nzuri.

  Source: Mwananchi
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Leo Yanga namuombea mabaya tu apigwe 2 bila....
   
 5. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Yanga 3 Azam 1 bila ubishi mnyama upoooo?
   
 6. n

  nyuki dume JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Azam 2 Yanga 1, mpo yeboyebo
   
 7. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Leo mtoto hatumwi dukani....hakika picha nzima ya nani atakuwa bingwa 2011/2012 tutaipata leo
   
 8. Magpie

  Magpie Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 26, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  dah naipenda yanga, lakini natamani azam wapate nafasi washiriki michuano ya CAF, tuone wataleta changamoto gani kwenye soka la kimataifa na soka la bongo kwa ujumla.
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Dah tumesha lia kimoja
   
 10. dedam

  dedam JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 846
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  azam 1-0 yanga
   
 11. K

  Konaball JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  mfungaji nani?
   
 12. dedam

  dedam JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 846
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  john boko
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Yebo Yebo .....leo mtajuta
   
 14. K

  Konaball JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  hya mzidi kutupa matokeo basi
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Unahuzunisha nani kawafunga.....lol
   
 16. K

  Konaball JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  vipi umeme ushakatika huko mbona hatupati uptdate
   
 17. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Yebo yebo wasikate tamaa...mpira ni dk 90!!!
   
 18. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  ...Wakiambulia sana ni droo.
   
 19. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Yanga leo watalewa lambalamba mpaka watambae
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Joni Bogo
   
Loading...