Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 56,608
- 93,411
Ni aibu kwa Watanzania mechi kama Simba na Power Dyanamos na Yanga na El Merreck zote zinapigwa kwenye nchi Jirani border to border kama viongozi wanashindwa kuwaandaa mashabiki wa timu hizi kuhudhuria kwa wengi mechi hizo kwa kuwawekea utaratibu rafiki badala ya kuwageuza fursa ili kuwapiga mashabiki.
Kwa mfano upande wa Simba mtu kama Avoid ni mtu wa Simba hamasisha mashabiki wengi wa Mbeya na Tunduma wawekewe utaratibu rahisi na bei nafuu waende Zambia.
Upande wa Yanga INA base kubwa Mwanza, ongea na Zakaria watu wa Mwanza na Geita waende Kigali kwa wingi na makao makuu idili na watu wa labda ya Pwani Moro, Dar, Tanga na Mtwara.
Tu jifunze kuamini matawi ya mikoani yajisimamie yenyewe kama wanaweza kuja kwenye matamasha ya Simba day na Yanga day kwa kujiorganise wenyewe hata hili wanaliweza na uzuri hizo nchi unaingia kwa temporary passport za karatasi tu ambazo hazina shida kuzipata.
Ni wakati sasa wa viongozi wa klabu hizi wachangamshe akili tuwe wanyonge mechi za mbali lakini siyo Zambia au Rwanda, tuukatae unyonge huu.