Yanga SC wasikilizeni 'Legends' wenu hawa akina Sekilojo na Ivo kisha mfunge 'Mabakuli' yenu na Simba SC iendelee tu Kutamba CL na VPL

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
" Mimi kama Sekilojo Chambua tena Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Yanga SC niseme tu kuwa hatushirikishwi katika Kusajili Wachezaji wa Yanga SC matokeo yake Mtu Mmoja anaamua kwenda Kusajili na anatusajilia Wachezaji wabovu tupu. Simba SC wataendelea Kufanikiwa kwakuwa wanajitambua na hawana ujanja ujanja na upuuzi uliopo huku Yanga SC "

Chanzo: Azam Tv Kabumbu Show

" Mimi kama Ivo Mapunda japo nimeshachezea Simba SC ila hakuna asiyejua kuwa ni mwana Yanga SC lia lia. Tusifiche Yanga SC kumejaa tu Wahuni na si Watu wa mpira. Simba SC wametuacha Yanga SC kwa mbali mno na Yanga SC haina Wachezaji wenye Hadhi ya Kuichezea na sijui Kamati yetu ya Usajili itatuambia nini kwani kwa Simba SC ilivyo sasa Ubingwa Kwao ni kama vile Israeli na Roho ya Binadamu "

Chanzo: Clouds FM Hili Game Show

Mtanuna mno tu mwaka huu hadi Mfe!
 
Timu ambazo Simba SC inaweza kucheza nazo fainali ya Klabu Bingwa Dunia mwaka huu
1.Man City
2.Chelsea
3.Real Madrid
4.PSG"
 
Pamoja na tatizo la usajili mbovu walioufanya lakini bado Yanga ina timu nzuri kiasi cha kuleta ushindani kwenye ligi na hata kubeba kombe. Matatizo ninayoyaona Yanga ni kama ifuatavyo:-
1. Wachezaji wamekosa morali ghafla pamoja na kuwekewa bonasi mara wapatapo ushindi. Kwa sasa viongozi wafanye haraka sana kutafuta wanasaikolojia mahiri wawapeleke kwenye kambi ya timu ili wainue morali upya.
2. Kubadilisha makocha mara kwa mara kiasi timu inakosa muendelezo.
3. Kikosi kidogo. Akikosekana mchezaji mmoja au wawili kati ya wanao cheza mara kwa mara kutokana na kadi au majeruhi basi timu nzima inakosa mwelekeo.
4. Timu haina kikosi cha kwanza cha kudumu. Kila kocha aliyekuja Yanga alikuwa na kikosi chake cha kwanza.
5. Viongozi kujikita kwenye mambo ya ovyo na malalamiko yasiyo ya msingi badala ya kujikita kwenye mambo ya msingi ya kutafuta ushindi halali ndani na nje ya uwanja.
6. Wachezaji na viongozi kujisifu kwa mafanikio madogo kama vile kujisifu kuwa timu haijapoteza mchezo (by then) badala ya kupamabana na kujisifu kwa kushinda mechi nyingi zaidi.
7. Muda mwingi kufuatilia mafanikio ya Simba na kutafuta njia za mkato kuyazuia kama vile kupokea timu pinzani na kuzipa mbinu za kuishinda Simba badala ya kukaa chini na kutafuta kwa udi na uvumba njia za kupatia Yanga ushindi kwenye FA na ligi kuu.

Mwisho Yanga wakae chini wajipange upya kuanzia mechi ya Biashara, wasikate tamaa kwani ligi bado ndefu kiasi lolote linaweza kutokea kwenye mbio za ubingwa na bado pia wana nafasi ya kuchukua FA. Wakipaniki tu sasa hivi kwenye hizi mechi tatu zijazo ambazo ndio "turning point" yao basi wajue kuwa watakuwa wamempa Simba ubingwa kilaini sana kwani kwa wakati huu ndio kuna uwezekano wa Simba kwenda kushika uongozi wa ligi. Inahitajika utulivu wa hali ya juu sana wa kisaikolojia kwa mashabiki, viongozi na wachezaji wa Yanga kwa siku za karibuni kukabiliana na hali hiyo iwapo Simba atafanya vizuri kwenye mechi zake na kukamata uongozi wa ligi.
 
Back
Top Bottom