kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
Shabiki wa timu ni mhimili laini wa timu ambao kazi Yake kwenye timu ni kusimamia furaha yao isipotezwe na wachezaji, viongozi, wafadhili na wadhamini wa timu yao. Yaani malipo ya shabiki wa timu ni furaha TU ya ushindi wa timu. Mashabiki ndio mjeredi (whip) imara wa timu kuwafanya wachezaji, viongozi, na wadau wengine wasipotee kwenye malengo yao.
Kama Shabiki wa timu anapokuwa karibu zaidi na rafiki mkubwa wa uongozi, wachezaji na mfadhili wa timu ni sawa na Mbunge anapokuwa karibu zaidi na rafiki mkubwa wa serikali, atashindwa kuisimamia na kuikosoa serikali kikamilifu pale ubadhilifu na wizi ndani ya serikali utakapotokea.
Mashabiki wa timu kazi yetu ni kushangalia timu viwanjani na kununua brands za timu na wafadhili na kusubiri kulipwa furaha na wachezaji, uongozi na mfadhili. Kama shabiki atakuwa karibu mno na uongozi ni mbaya sana kwakuwa itampunguzia shabiki uwezo wake na nguvu zake za kumkosoa kiongozi, mchezaji, kocha au mfadhili pale timu itakapofanya vibaya; Utaona aibu kufanya hivyo.
Kuwa karibu zaidi na uongozi, kuitwa kunywa supu pamoja na uongozi na kuvaa misuri sikuungi mkono kwakuwa ni kama rushwa na pombe, inayolegeza nguvu za shabiki, kufunga mdomo, kupofua macho na masikio dhidi ya uongozi na mchezaji pale mambo yatakapokwenda vibaya. Kifupi ni rushwa ya mazingira ambayo itamlazimisha shabiki akae kimya milele na kusababisha migogoro miongoni mwa mashabiki wanaokunywa supu na wasiokunywa supu kama itatokea changamoto.