Inasemekana TFF wanasubiri jawabu ya ufafanuzi kutoka FIFA kuhusiana na Okwi, anayesemakana kuishtaki Etoile kutomlipa mshahara, Etoile kumshtaki Okwi kwa kutoroka na Simba kuishtaki Etoile kwa kutowalipa hela yao. Atika mantiki ya kawaida, ni lipi kati ya hili linaloweza kumziwia mchezaji kuhamia timu nyengine, ilovyokuwa tayari alishahamishiwa Villa. Jawabu ni kuwa uhamisho wenyewe ulikuwa ni wa muda. Kuna kitu kama hicho FIFA? Na kama kiko, kanuni inasemaje juu ya mchezaji wa aina hiyo kuhama? Na kama kanuni hiyo iko, kwa nini TFF watake ufafanuzi? Mbona FUFA hwakutaka ufafanuzi? Swala la msingi ni vipi FIFA kama kweli kuna kesi hizo imebaki kimya muda wote huo, hata baada ya kuulizwa na TFF? Nadhani kwa hili kuna mawili, kutojiamini kwa TFF au siasa kuendelea ndani ya TFF. Ingawa binafsi siamini iwapo hata kama kuna kesi hizo.