Hatma Ya Kidole Cha Mrwanda Na Okwi Wiki Ijayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatma Ya Kidole Cha Mrwanda Na Okwi Wiki Ijayo

Discussion in 'Sports' started by Pdidy, Nov 26, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  Hatma Ya Kidole Cha Mrwanda Na Okwi Wiki Ijayo
  [​IMG]
  Danny Mrwanda (kushoto) akishangilia huku akinyoosha kidole kilichokuja kuhusishwa na alama ya matusi kwa mashabiki wa YangaThursday, November 26, 2009 9:01 PM
  HATIMAYE hatma ya washambuliaji nyota wa klabu ya Simba, Danny Mrwanda na Emmanuel Okwi kwa kuonyesha ishara ya kuwatukana mashabiki wakati wa mchezo dhidi ya Yanga sasa itajulikana wiki ijayo.Mrwanda na Okwi wanatuhumiwa kuonyesha ishara ya matusi kwa mashabiki wakati walipokuwa wakishangilia bao lililofungwa na Musa Hassan Mgosi kwenye mchezo dhidi ya wapinzani wao Yanga mwishoni mwa mwezi uliopita.


  Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela aliliambia gazeti moja la kila siku la Tanzania kuwa kamati ya nidhamu ya Shirikisho hilo itakaa mapema wiki ijayo kujadili suala hilo ikiwa ni pamoja na masuala mengine mbali mbali ya ligi.


  Alisema hivi sasa TFF wanakamilisha kufanya tathmini ya ligi kabla ya kufanya kikao hicho ambacho kitatoa maamuzi mbali mbali kufuatia matukio yaliyotokea kwenye ligi hiyo iliyomaliza mzunguko wake wa kwanza hivi karibuni huku Simba ikiwa kinara kwa kuwa na pointi 33 huku ikiandika rekodi ya kutofungwa mechi yoyote
   
Loading...