Yanga inahitaji Mbuyu Twite watatu kwenye back four yake.

Yanga inahitaji Mbuyu Twite watatu kwenye back four yake.

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,317
Reaction score
3,637
Tar 18.04.2015 Yanga ilikua Uwanja wa Taifa ikiiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa kama kawaida yao,katika mechi hiyo Mbuyu Twite alikua akicheza no 6 baada ya Canavaro kuumia kipindi cha pili,aliingia no 6 nyingine Said Makapu ambapo ilimlazimu Mbuyu Twite kushuka chini kucheza no 5 akimpisha no 6 Makapu,Muda mfupi baadae Juma Abdul aliumia na nafasi yake akaingia no 5 Rajab Zahir,hapa tena Mbuyu Twite alimpisha Zahir kwenye no 5 yeye akaenda kucheza no 2,hapa Mbuyu ukawa
umeweka record ya dunia kwa kucheza nafasi 4 katika mechi moja(dk90) huyu ndiye mtu wa kazi kiraka ama beki ambaye Yanga inamkosa hivi sasa.

Katika historia ya Yanga,katika safu ya back 4 hakuna mchezaji imara aliyepita Yanga na asiye na masihara Mbuyu Twite,ni kweli kwamba kuna vijana wapya wanakuja kwa kasi kina Mwijage,Ngoma,Bacca,Mwamnyeto,Job lakini ni lazima tukubali kwamba hawa wachezaji wa kibongo they do not concentrate,na wanafungwa wakimuangalia Mpanzu akipita na wao kukaa chini kuangalia goli linavyofungwa,tunahitaji beki kisiki kama Mbuyu Twite,tunahitaji mtu kama Mbuyu Twite kwenye centre back,tunahitaji mtu kama Mbuyu Twite kwenye full back ya kulia na kushoto kama Mbuyu Twite au kama Juma Abdul ama alivyokuwa Kessy,tukishindwa sana basi tupate mtu wa kazi kama Kamusoko,Makapu, Telela,

Mbuyu Twite alisajiliwa Yanga kama beki wa kulia,kwa kuwa alikuwa mtu wa shoka,mbuyu kweli kweli usioanguka kirahisi,Mbuyu Twite alifanikiwa kucheza nafasi zote za ulinzi na kuwa mchezaji ambaye aliyetumika zaidi katika kikosi cha timu ya Yanga hasa kunapokuwa na majeruhi na kunapokuwa na uhitaji maalumu wa kushinda mechi,Mbuyu Twite aliweza kubadilishwa na kocha kucheza beki wa kulia,kunapokuwa na uhitaji wa kushinda kwenye hiyo hiyo mechi kocha anambadilisha kwenda kucheza beki wa kati,beki wa kushoto na kiungo mkabaji hadi ushindi unapatikana.Rejea makosa ya Yanga kwenye mechi na Gaborone,Cctv alijaribu style moja ya attack kwenye ukuta wa Yanga na akafunga goli,Jana Clautous Chama,Elie Mpanzu,Neo Maema na Gueye wamejaribu mara tatu na wamepata goli mbili,beki za Yanga zinaona style hiyo hiyo ikirudiwa mara tatu na hawajifunzi!.

-Scout wa Yanga uwa wanafeli kwenye usajili.

Mbuyu Twite hakusajiliwa na Yanga,bali alitafutwa na Scout ya Simba wakamleta bongo,Yanga wakamnyakua kwa style ile ile waliyomnyakua Selemani Mwalimu,Rais wa zamani wa Simba,Aden Rage alikwenda Rwanda akazungumza na Mbuyu Twite kwa ajili ya kumsajili kisha akamleta Dar kwa ajili ya utambulisho,kwenye mazoezi,mabosi wa Yanga wakatumiwa mavitu ya Mbuyu Twite wakasanda,wakaona Mbutu Twite atakuja kuwatoa nishai,Mabosi wa Yanga wakakwea pipa hadi Rwanda,wakauliza kama Simba wameshawalipa mkwanja ili kumchukua Twite,wakaambiwa bado,malipo yanatakiwa yawasilishwe Fc Lupopo kwa kuwa ndio mchezaji wao na huku kote alikuwa kwa mkopo,Yangq wakatuma mkwanja kwenda Congo kwa Fc Lupopo,Mbuyu Twite akaitwa Congo,alivyorudi Dar akapokelewa na Mabosi wa Yanga na sio Rais wa Simba,Ismail Aden Rage.

-Kocha Manqoba Mngqithi,kocha bora ila hajapata kikosi hadi sasa hivi,kumtoa Mudathir na Kangwanda,kuwaingiza komara,Mwijage na chuga,awa wachezaki wametoka uko kmc wanawezaje kucheza derby,mnaishia kufungwa kipigo cha aibu sana,goli linaingia beki kasanda kakaa chini,kipa Diara kapiga msamba kalambwa chenga kafungwa goli huku Mwamnyeto akishuhudia goli,Coach Manqoba Mngqiti lazima utafute kikosi chako cha maangamizi,wewe ni kocha bora sana,uliipa ubingwa timu ya Amazulu,ndipo Mamelody Sundown wakakuita ukawe kocha wao,wewe hauwezi kushindwa kupata kikosi imara cha maangamizi hapo Yanga,wapo watu wa kazi hapo jana hawajacheza Salum Abubakar ("Sure Boy"),Aziz Andambwile,Aziz ki,Mohamed Hussein.Coach Manqoba Mngqithi haiwezekani kwenye mechi na Gaborone,Cctv anajaribu mara tatu na anafunga goli,mechi na Simba Neo Maema anajaribu mara tatu na anafunga goli,Elie Mpanzu anajaribu mara tatu na anafunga goli,Chama na Doumbia nao wangejaribu mara tatu wangefunga goli,hii ni alarm inakulilia.

Nikiishia hapa,
Mimi ni Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro financing on Poverty Reduction.
 
Mimi ninachofahamu mpaka muda huu Yanga haina kiungo mkabaji halisi na pia beki namba 5! Labda Dickson Job arejee mapema kuchukua namba ya Bakary Mwamnyeto, beki aliyekosa kasi ya kupambana na wachezaji aina ya Mpanzu na Libase Gueye.
 
Mkuu nje ya mada
Uliachana na mambo ya CCM? Siku hizi sioni comment zako
 
Back
Top Bottom