Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 28,382
- 81,845
Hakika umenena vyema! Timu yetu ilishakua na tatizo la washambuliaji tangu mwanzo wa msimu!Inawezekana pia lakini siyo sababu ya msingi. Yanga Ina matatizo kwa pande zote kuanzia kwa kocha, wachezaji, uongozi pia, na sisi Wapenzi na washabiki
1. Kocha
Toka kupumzika kwa kocha Mwambusi benchi la ufundi limekuwa likishindwa kuusoma mchezo husika na kupanga kikosi mahususi. Hata ikiwa tayari imeonyeaha kuelemewa, kocha na bench zima wamekuwa si wepesi wa kusoma na kutambua tatizo ili kufanya sub ya maana kwa wakati. Refer mechi dhidi ya Mbeya city, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar hata hile ya kirafiki dhidi ya African sports madhaifu ni yake Yale kwa upande wa benchi la ufundi. Kiufundi naliona bench Hili la ufundi likizidiwa kwa mbali na like la papa Zahera Mwinyi.
2. Wachezaji
Kiukweli katika vitu ambavyo vimaiangusha timu Ni haina ya wachezaji tuliokuwa nao Sasa. Yaana ubinifu zero. Ukimtoa Mkoko na Tuisila Hawa wengine walioletwa na Eng. Hersi hawafai hata kuchezea Mbao fc. Lazima tufike mahalo tuambiane ukweli wale tumeletewa Mizigo tu, Ni Mara Mia tungesajili wachezaji wa ndani tu kuliko hii Mizigo. Hebu tumlinganishe Sarpong na Yusuf Mhiru, muangalie huyu Eric Msagati, Kuna huyu mchezaji yuko Gwambina anaitwa Meshaki Abeli na wengine wengi wanawazidi kwa mbali Sana Hawa tunaoaminishwa kuwa Ni mapro. Kiufupi Hawa kina Sarpong nawafananisha na watumishi hewa. Ni kheri tungebaki na Moringa David kuliko Hawa walioletwa kwa mbwebwe.
3. Viongozi Mikakati ya mafanikio ni Zero
Hawa Ni tatizo kubwa, kwa kiasi kikubwa Hawa wamefeli kabisa. Wanakosa Mission na Vision. Hadi Sasa nashindwa kuelewa Ni Yanga ya aina gani wanayoitengeneza na watafanikiwa kuifikia kwa njia zipi na kwa muda gani. Timu yoyote duniani lengo kubwa Ni KUSHINDA vikombe kwa uelewa wangu mdogo, au niseme Ni kutengeneza timu yenye ushindani. Sasa hebu tujiulize Yanga pamoja na kuongoza ligi tuna timu ya kushindana? Kwangu Mimi jibu Ni Hapana. Sasa Kama jibu Ni Hapana uongozi ndiyo umeboresha timu kwa kutuletea wachezaji Kama Fiston, alafu tunadanganyana tutunishe vifua ubingwa Ni wetu mwaka huu? Kwa wachezaji Hawa wa kuokoteza? Kazi viongozi imekuwa ni kulalamika tuuu badala kuangalia tunajikwamua vipi. Anyway labda Mimi peke yangu ndiyo sielewi.
4. Washabiki na Wapenzi
Tuna tatizo la kuhemuka, tunaaminishwa mambo mengine ambayo kiukweli hayawezekani nasi tunakubali. Tuungane kuwaambia ukweli Hawa viongozi ndiyo watabadilika. Tukiendelea hivi kuwapa support wanaona sawa tu, mwishowe mtaikuta timu Hiko nafasi ya kumi huko au inastruggle isishuke daraja. Tafadhari tuwe wamoja katika hili. Wakifanya vizuri tuwape sifa, wakiboranga tuwape ukweli wao.
NB:
Ukweli utaniweka huru. Tatizo kubwa la Yanga ni mfumo wa uendeshaji wa klabu. Tufanye haraka twende kwenye mabadiliko ambayo yatafanya timu kuwa vizuri kiuchumi hivyo kutuwezesha kutengeneza timu bora ya ushindani. Wakati Ni sasa Wala hatujachelewa.
Msimu ujao napendekeza Hawa wachezaji wa kigeni tubaki na wachache tu wenye tija, tusajili wachezaji wa ndani na wenye uwezo, hii iatatusaidia kupunguza gharama za uendeshaji kabla ya mabadiliko wakati Mikakati wa mabadiliko ukiendelea.
Mwisho nasisitiza tuwe na Mikakati ya kuutafuta ushindi, kiufundi ndani na nje ya uwanja. Tusiwe wa kulalamika kutafuta huruma. Tuige kwa wenzetu wanafanyaje, tutafika tu. Samahani uandishi nao Ni kipaji na Ni taaluma pia, inawezekana mipangilio na uandishi wangu siyo mzuri Ila nadhani nimeeleweka.
Yanga daimambele, nyuma mwiko,
Asanteni
Cha kushangaza wakati wa dirisha dogo, uongozi wakishirikiana na mwalimu Kaze, wakasajiri washambuliaji wao ambao mpaka sasa hawajaonesha faida yoyote ile kwa timu!
Huyu Fiston sijui hata kama anastahili kuongezewa hata mkataba baada ya huo mkataba wa miezi sita aliopewa kumalizika. Kiukweli kiwango chake kimeshuka sana. Saido ndiyo kwanza anaendelea tu kula mafao.