Afadhali kila mtu aangalie mambo ya nyumbani mwake!!
Wewe Endelea kubeba mambo ya wenzako,
Eeehh..sawaaa..lakini ujue tu toka tar 17 may..umeme haukupatikana na watu walienda wilayani kupanga foleni kununua umeme..shwani kabisaaa nyiee..subirini awamu hii..nchi itatafunwaaa had unyayooo...na lugumu kasharudi kusupply mavazi ya jeshi...jinga kabisaa tanzanian politician..na watanzania kama nyie wenye funza vichwani..
Hakuńa mtu alianza nch vizurí kama JK.... lakini JPM alianza vizuri zaidi...
Łakini mwisho wa siku wote wakajikuta wanageuka na kuwa TAKATAKA....
tupeane muda tafadhali.
Tuondoleee uchafu wako hapa..ukiona mtu anashindwa jambo alaf anasingizia wengine ni udhaifu mbovu sana..Kamanda Sirro mwingine huyo ongezea kwenye list yako.
Wako busy kumhujumu mama waseme mama kashindwa.
Wa namna kama ulivyo kuwa ukitufanyia awamu ile, hii sukuma ndani!
Tuondoleee uchafu wako hapa..ukiona mtu anashindwa jambo alaf anasingizia wengine ni udhaifu mbovu sana..
Kwaiyo maoni yako ni yapi MATAGAEeehh..sawaaa..lakini ujue tu toka tar 17 may..umeme haukupatikana na watu walienda wilayani kupanga foleni kununua umeme..shwani kabisaaa nyiee..subirini awamu hii..nchi itatafunwaaa had unyayooo...na lugumu kasharudi kusupply mavazi ya jeshi...jinga kabisaa tanzanian politician..na watanzania kama nyie wenye funza vichwani..
Kwa kweli mimi binafsi mpaka muda huu mama nimemridhia kwa zaidi ya asilimia 99.
Anapiga kazi nzuri sana.
Atusaidie kutupa katiba mpya tu na kuleta maendeleo, 2025 Insha Allah anapita kiulaini
Mama ameamua kuachana na mambo maovu ameelekea mambo mema anastahili pongeziMabibi na mabwana ni ukweli usiofichika kuwa wengi wa walio wazalendo, wanayo furaha kubwa kumpata mama Samia kama Rais wetu wa JMT kwa sasa.
Katika kumtia shime mama yetu kazi inapoendelea si haba kuyapitia yale ambayo haswa, yanayotukosha nyoyo za zetu kutokana na utendaji wake:
1. Corona na ripoti ya tume: hili linabeba maisha yetu. Mapendekezo ya tume ya wataalamu yamekwisha tolewa na yako mikononi mwake.
2. Kutambua rasmi kuwa tumekuwa tukibambikiziwa kesi na taasisi za serikali. Tayari kesha wanyooshea vidole stahiki: takukuru, TRA, polisi wakiwamo wale wakubrashi viatu, nk.
3. Ripoti za CAG BOT na TPA: Mama machale yameshamcheza (tumekuwa tukipima) amemhitaji CAG awe muwazi zaidi kwenye ripoti zake, wala asimung'unye maneno. Dalili za wazi kuwa mama hana urafiki na majizi hata kama anakaa nayo meza moja kwa sasa. Tulipo tuko mkao wa kula tukimsubiria CAG Kichere kuunguruma.
4. Viongozi washukiwa wakubwa wa ukiukaji haki za watu, habari wanayo. Tayari DC Ole yuko benchi kwa uchunguzi. Huyo ni aliye hadharani. Ole kama Papa waliokuwa wakivuma baharini kweli kweli, yafahamika hakuwa peke yake!
5. Mama kasema hataki dhuluma za namna yoyote. Mama ni mcha Mungu hataki kuchonganishwa na Mola wake. Mungu atupe nini sisi?
6. Mama amekuwa muwazi kueleza hali yetu ilivyo. Nini hakiwezekani na nini kinawezekana sasa, amefafanua kwa kila mtu anayetaka kuelewa. Mama anatambua haki za watu kupandishwa mishahara, kupata ajira, nk. Tayari kuna ajira mpya kwenye hatua za utekelezaji.
Waungwana karibuni nanyi kutupia vya kwenu katika kutambua jitihada za Mama yetu Rais wetu wa JMT, kazi inapoendelea.
Tunakoelekea kila siku inazidi kuwa bora kuliko jana.Mama anao ujasiri huo wa kutupa katiba mpya bila msuguano. Tumwunge mama mkono.
Kimsingi CCM hajamweka mama pale. Hata ile nafasi ya Makamu wa Rais ilikuwa ya kuzugia tu. Na hawakuwahi kufikiria ipo siku Rais anaweza akafariki akiwa madarakani na Makamu akachukua nchi. Kama hili wangelijua basi Makamu wasingeweka mwanamke. Kudhihirisha nachosema tazama walivyonuna baada ya kuona Samia Katiba imempa nchi.Hakika tumepata Rais msikivu mno....mh.SSH ni jembe haswa ,siku zinavyozidi kwenda tutazidi kuuona UBORA WAKE.....
Hakika hayati Magufuli aliiona hazina kubwa ya KIPAJI CHAKE CHA UONGOZI.....
Hakika CCM imetuletea RAIS BORA WA KUIGWA NA KILA MTANZANIA MZALENDO NA MWENYE KUPENDA UKWELI ,UWAZI ,UWAJIBIKAJI NA KUTHAMINIANA!!!
Mh.SSH amenigusa kwa kuwakumbusha baadhi ya ASKARIPOLISI wajibu wao wa kusimamia haki na kutowabambikia KESI baadhi ya WATANZANIA wenzao......
#StaunchSupporterOfSSH
#DieHardFanOfCCM