Yanayotukonga nyoyo zetu kutoka kwa Rais Samia Suluhu

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,623
2,000
Mabibi na mabwana ni ukweli usiofichika kuwa wengi wa walio wazalendo, wanayo furaha kubwa kumpata mama Samia kama Rais wetu wa JMT kwa sasa.

Katika kumtia shime mama yetu kazi inapoendelea si haba kuyapitia yale ambayo haswa, yanayotukosha nyoyo za zetu kutokana na utendaji wake:

1. Corona na ripoti ya tume: hili linabeba maisha yetu. Mapendekezo ya tume ya wataalamu yamekwisha tolewa na yako mikononi mwake.

2. Kutambua rasmi kuwa tumekuwa tukibambikiziwa kesi na taasisi za serikali. Tayari kesha wanyooshea vidole stahiki: takukuru, TRA, polisi wakiwamo wale wakubrashi viatu, nk.

3. Ripoti za CAG BOT na TPA: Mama machale yameshamcheza (tumekuwa tukipima) amemhitaji CAG awe muwazi zaidi kwenye ripoti zake, wala asimung'unye maneno. Dalili za wazi kuwa mama hana urafiki na majizi hata kama anakaa nayo meza moja kwa sasa. Tulipo tuko mkao wa kula tukimsubiria CAG Kichere kuunguruma.

4. Viongozi washukiwa wakubwa wa ukiukaji haki za watu, habari wanayo. Tayari DC Ole yuko benchi kwa uchunguzi. Huyo ni aliye hadharani. Ole kama Papa waliokuwa wakivuma baharini kweli kweli, yafahamika hakuwa peke yake!

5. Mama kasema hataki dhuluma za namna yoyote. Mama ni mcha Mungu hataki kuchonganishwa na Mola wake. Mungu atupe nini sisi?

6. Mama amekuwa muwazi kueleza hali yetu ilivyo. Nini hakiwezekani na nini kinawezekana sasa, amefafanua kwa kila mtu anayetaka kuelewa. Mama anatambua haki za watu kupandishwa mishahara, kupata ajira, nk. Tayari kuna ajira mpya kwenye hatua za utekelezaji.

Waungwana karibuni nanyi kutupia vya kwenu katika kutambua jitihada za Mama yetu Rais wetu wa JMT, kazi inapoendelea.

Nani kama Mama?
 
jailos mrisho

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
411
1,000
Eeehh..sawaaa..lakini ujue tu toka tar 17 may..umeme haukupatikana na watu walienda wilayani kupanga foleni kununua umeme..shwani kabisaaa nyiee..subirini awamu hii..nchi itatafunwaaa had unyayooo...na lugumu kasharudi kusupply mavazi ya jeshi...jinga kabisaa tanzanian politician..na watanzania kama nyie wenye funza vichwani..
 
data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
23,480
2,000
Hakuńa mtu alianza nch vizurí kama JK.... lakini JPM alianza vizuri zaidi...

Łakini mwisho wa siku wote wakajikuta wanageuka na kuwa TAKATAKA....

tupeane muda tafadhali.
 
Kamanda Sirro mwingine huyo ongezea kwenye list yako.

Wako busy kumhujumu mama waseme mama kashindwa.

Wewe kuwa wa namna kama ulivyo kuwa ukitufanyia awamu ile wala usizidishe makali.

Wa namna hii wewe sukuma ndani!
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,623
2,000
Hakuńa mtu alianza nch vizurí kama JK.... lakini JPM alianza vizuri zaidi...

Łakini mwisho wa siku wote wakajikuta wanageuka na kuwa TAKATAKA....

tupeane muda tafadhali.

Ninadhani JK hujamtendea haki.

Mwanzo wa mama ni mzuri zaidi.

Kumbuka tunatoka kwenye vita vya kiuchumi na Nyungu za mawe.

Serikali ya mama ni sikivu si ya mawe. Kwa usikivu wake, tunavuka.
 
jailos mrisho

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
411
1,000
Kamanda Sirro mwingine huyo ongezea kwenye list yako.

Wako busy kumhujumu mama waseme mama kashindwa.

Wa namna kama ulivyo kuwa ukitufanyia awamu ile, hii sukuma ndani!
Tuondoleee uchafu wako hapa..ukiona mtu anashindwa jambo alaf anasingizia wengine ni udhaifu mbovu sana..
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,740
2,000
Hakika tumepata Rais msikivu mno....mh.SSH ni jembe haswa ,siku zinavyozidi kwenda tutazidi kuuona UBORA WAKE.

Hakika hayati Magufuli aliiona hazina kubwa ya KIPAJI CHAKE CHA UONGOZI.

Hakika CCM imetuletea RAIS BORA WA KUIGWA NA KILA MTANZANIA MZALENDO NA MWENYE KUPENDA UKWELI ,UWAZI ,UWAJIBIKAJI NA KUTHAMINIANA!!!

Mh.SSH amenigusa kwa kuwakumbusha baadhi ya ASKARIPOLISI wajibu wao wa kusimamia haki na kutowabambikia KESI baadhi ya WATANZANIA wenzao.

#StaunchSupporterOfSSH
#DieHardFanOfCCM
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,623
2,000
Tuondoleee uchafu wako hapa..ukiona mtu anashindwa jambo alaf anasingizia wengine ni udhaifu mbovu sana..

Mkuu mimi nimenukuu tu lini alikuwa anaitishwa Sirro awamu ile. Si ilikuwa hivi hivi nilivyomwitisha mimi? Au halali ilikuwa kule si huku? Nyie vipi mara hii mshasahau?
 
cabo

JF-Expert Member
Jun 15, 2016
3,420
2,000
Eeehh..sawaaa..lakini ujue tu toka tar 17 may..umeme haukupatikana na watu walienda wilayani kupanga foleni kununua umeme..shwani kabisaaa nyiee..subirini awamu hii..nchi itatafunwaaa had unyayooo...na lugumu kasharudi kusupply mavazi ya jeshi...jinga kabisaa tanzanian politician..na watanzania kama nyie wenye funza vichwani..
Kwaiyo maoni yako ni yapi MATAGA
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
17,419
2,000
Mabibi na mabwana ni ukweli usiofichika kuwa wengi wa walio wazalendo, wanayo furaha kubwa kumpata mama Samia kama Rais wetu wa JMT kwa sasa.

Katika kumtia shime mama yetu kazi inapoendelea si haba kuyapitia yale ambayo haswa, yanayotukosha nyoyo za zetu kutokana na utendaji wake:

1. Corona na ripoti ya tume: hili linabeba maisha yetu. Mapendekezo ya tume ya wataalamu yamekwisha tolewa na yako mikononi mwake.

2. Kutambua rasmi kuwa tumekuwa tukibambikiziwa kesi na taasisi za serikali. Tayari kesha wanyooshea vidole stahiki: takukuru, TRA, polisi wakiwamo wale wakubrashi viatu, nk.

3. Ripoti za CAG BOT na TPA: Mama machale yameshamcheza (tumekuwa tukipima) amemhitaji CAG awe muwazi zaidi kwenye ripoti zake, wala asimung'unye maneno. Dalili za wazi kuwa mama hana urafiki na majizi hata kama anakaa nayo meza moja kwa sasa. Tulipo tuko mkao wa kula tukimsubiria CAG Kichere kuunguruma.

4. Viongozi washukiwa wakubwa wa ukiukaji haki za watu, habari wanayo. Tayari DC Ole yuko benchi kwa uchunguzi. Huyo ni aliye hadharani. Ole kama Papa waliokuwa wakivuma baharini kweli kweli, yafahamika hakuwa peke yake!

5. Mama kasema hataki dhuluma za namna yoyote. Mama ni mcha Mungu hataki kuchonganishwa na Mola wake. Mungu atupe nini sisi?

6. Mama amekuwa muwazi kueleza hali yetu ilivyo. Nini hakiwezekani na nini kinawezekana sasa, amefafanua kwa kila mtu anayetaka kuelewa. Mama anatambua haki za watu kupandishwa mishahara, kupata ajira, nk. Tayari kuna ajira mpya kwenye hatua za utekelezaji.

Waungwana karibuni nanyi kutupia vya kwenu katika kutambua jitihada za Mama yetu Rais wetu wa JMT, kazi inapoendelea.
Mama ameamua kuachana na mambo maovu ameelekea mambo mema anastahili pongezi
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
17,419
2,000
Hakika tumepata Rais msikivu mno....mh.SSH ni jembe haswa ,siku zinavyozidi kwenda tutazidi kuuona UBORA WAKE.....

Hakika hayati Magufuli aliiona hazina kubwa ya KIPAJI CHAKE CHA UONGOZI.....

Hakika CCM imetuletea RAIS BORA WA KUIGWA NA KILA MTANZANIA MZALENDO NA MWENYE KUPENDA UKWELI ,UWAZI ,UWAJIBIKAJI NA KUTHAMINIANA!!!

Mh.SSH amenigusa kwa kuwakumbusha baadhi ya ASKARIPOLISI wajibu wao wa kusimamia haki na kutowabambikia KESI baadhi ya WATANZANIA wenzao......

#StaunchSupporterOfSSH
#DieHardFanOfCCM
Kimsingi CCM hajamweka mama pale. Hata ile nafasi ya Makamu wa Rais ilikuwa ya kuzugia tu. Na hawakuwahi kufikiria ipo siku Rais anaweza akafariki akiwa madarakani na Makamu akachukua nchi. Kama hili wangelijua basi Makamu wasingeweka mwanamke. Kudhihirisha nachosema tazama walivyonuna baada ya kuona Samia Katiba imempa nchi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom