Yanayotukonga nyoyo zetu kutoka kwa Rais Samia Suluhu

Kimsingi CCM hajamweka mama pale. Hata ile nafasi ya Makamu wa Rais ilikuwa ya kuzugia tu. Na hawakuwahi kufikiria ipo siku Rais anaweza akafariki akiwa madarakani na Makamu akachukua nchi. Kama hili wangelijua basi Makamu wasingeweka mwanamke. Kudhihirisha nachosema tazama walivyonuna baada ya kuona Samia Katiba imempa nchi.

Wanga wanafiki wakubwa. Kwani wanawake si watu? Mama zao ni wanaume?

Yote tisa, usikivu wa mama. Mama si jiwe!
 
Wanawake bhana! hata kule Instagram Mange nae kutwa kumpamba mwanamke mwenzie yani ni kusifu kwa kila jambo, ubaya akianza kufanya msivyotegemea mnajenga chuki kabisa.
 
Nimedhani JK hujamtendea haki.

Mwanzo wa mama ni mzuri zaidi. Kumbuka tunatoka kwenye vita vya kiuchumi na Nyungu za mawe.

Serikali ya mama ni sikivu si ya mawe. Kwa usikivu wake, tunavuka.
Mvuke? Wameshaanza kutest mitambo kwenye luku, vuta subira uone kazi inavyoendelea.
 
Mama ni mama mama ni mgongo wa familia mama Yuko juu Sana Mungu amlinde mama wa Taifa letu
 
Mabibi na mabwana ni ukweli usiofichika kuwa wengi wa walio wazalendo, wanayo furaha kubwa kumpata mama Samia kama Rais wetu wa JMT kwa sasa.

Katika kumtia shime mama yetu kazi inapoendelea si haba kuyapitia yale ambayo haswa, yanayotukosha nyoyo za zetu kutokana na utendaji wake:

1. Corona na ripoti ya tume: hili linabeba maisha yetu. Mapendekezo ya tume ya wataalamu yamekwisha tolewa na yako mikononi mwake.

2. Kutambua rasmi kuwa tumekuwa tukibambikiziwa kesi na taasisi za serikali. Tayari kesha wanyooshea vidole stahiki: takukuru, TRA, polisi wakiwamo wale wakubrashi viatu, nk.

3. Ripoti za CAG BOT na TPA: Mama machale yameshamcheza (tumekuwa tukipima) amemhitaji CAG awe muwazi zaidi kwenye ripoti zake, wala asimung'unye maneno. Dalili za wazi kuwa mama hana urafiki na majizi hata kama anakaa nayo meza moja kwa sasa. Tulipo tuko mkao wa kula tukimsubiria CAG Kichere kuunguruma.

4. Viongozi washukiwa wakubwa wa ukiukaji haki za watu, habari wanayo. Tayari DC Ole yuko benchi kwa uchunguzi. Huyo ni aliye hadharani. Ole kama Papa waliokuwa wakivuma baharini kweli kweli, yafahamika hakuwa peke yake!

5. Mama kasema hataki dhuluma za namna yoyote. Mama ni mcha Mungu hataki kuchonganishwa na Mola wake. Mungu atupe nini sisi?

6. Mama amekuwa muwazi kueleza hali yetu ilivyo. Nini hakiwezekani na nini kinawezekana sasa, amefafanua kwa kila mtu anayetaka kuelewa. Mama anatambua haki za watu kupandishwa mishahara, kupata ajira, nk. Tayari kuna ajira mpya kwenye hatua za utekelezaji.

Waungwana karibuni nanyi kutupia vya kwenu katika kutambua jitihada za Mama yetu Rais wetu wa JMT, kazi inapoendelea.
Ni wazi mama anataka kuendesha nchi kwa maadili mema na yaliyo wazi.
Kuna viongozi bado hawajamuelewa na wanafikiri bado tuko awamu ya tano.
 
Back
Top Bottom