Yanayosemwa kuhusu SHIB-NSSF na Bima ya Afya

Mathayo Fungo

JF-Expert Member
Nov 13, 2018
319
510
Nikiwa katikati ya harakati za kusaka mkate wangu wa siku, nikakutana na hoja ambayo si tu kwamba ilinichosha bali ilinipa mahangaiko kutokana na UPOTOSHAJI mkubwa ambao ukiuangalia kwa ndani unabaini unafanyika makusudi ili kuendelea kunufaisha wachache na kuangamiza wengi. Habari ya mjini iliyopo kwa sasa ni juu ya Muswada wa Bima ya Afya kwa wote, kwa nini umekuja sasa na nini faida zake na je ni sababu zipi zilizopelekea Serikali kuja na mapendekezo hayo.

Ikanilazimu kutulia na kutega sikio, jamaa mmoja akaendelea kushawishi kundi la wananchi aliokuwa nao, nikasikia akisema “Ni muhimu sana kuacha SHIB ya NSSF iendelee kuwepo huko badala ya kuifuta na kuihamishia NHIF kama Muswada unavyopendekeza” hoja hii ikanifanya nizidi kuwa mdadisi ili nijue ni faida zipi zipo SHIB na endapo SHIB ikiondolewa ni kipi wanachama watakikosa.

Nikazichimba huduma za matibabu zinazotolewa na SHIB ambazo kikawaida huwezi kusema hiyo ni bima ya afya kwa kuwa, kwanza huduma zake zimefungwa kwenye vituo kadhaa ambavyo havizidi vitatu katika eneo ambalo mwanachama husika anaishi, jambo ambalo kimsingi halimsaidii hata kidogo mwanachama haswa anapohitaji huduma akiwa nje ya vituo ambavyo anapaswa kutibiwa.

Nikatafakari ni KWA NINI HOJA KAMA HII DHAIFU INAIBULIWA KATIKA KIPINDI HIKI MUHIMU CHA KUPITISHWA KWA MUSWADA WA BIMA YA AFYA KWA WOTE ambao kwa uhakika kabisa umezingatia upatikanaji wa uhakika wa huduma za matibabu kwa wanachama wake na kwa wigo mkubwa wa huduma pamoja na vituo ambavyo mwanachama atapata huduma.

Ikanisukuma kufanya malumbano ya hoja kichwani mwangu na jambo kubwa ambalo nililiona hapa ni watu wachache ambao wameamua kujinufaisha au kuangalia maslahi yao badala ya kuangalia Maslahi mapana ya Watanzania wengi ambao leo kila kona wanahangaika namna ya kupata huduma za matibabu. Ifike mahali masuala ya msingi yanayohusu kunufaika kwa wananchi wote tuyape kipaumbele na kuondoa ubinafsi wa mtu mmoja mmoja ili Taifa letu liweze kupiga hatua za kimaendeleo.

Huwa nashangaa sana ninapoona mtu anasimama na kuusema vibaya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambao kimsingi ndio umesaidia kutoa dira ya kuyaelekea mafanikio ya Bima ya afya kwa wote.

Leo hii tunaona watu wanavyohangaika kufanya udanganyifu ili wanufaike na huduma za matibabu kupitia NHIF na hii inatuonesha moja kwa moja kuwa ni wakati muafaka sasa wa kila Mtanzania kuwa na Bima ya Afya ili anapougua asipate shida na badala yake achukue hatua ya kwenda hospitali kupata huduma kwa kutumia kadi yake ya bima.

Nimekuwa mdau mkubwa wa masuala ya afya na ninakutana na wananchi wengi ambao ni wanachama wa Bima wakiwa katika hospitali mbalimbali na wengi wamekuwa mashuhuda wazuri wa namna Mfuko huu ulivyookoa maisha yao.

Nilibahatika kukutana na Mama mmoja ambaye alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo na alichoweza kuniambia ni kwamba kadi ya Bima kwake ni zaidi ya mume wake na anaitunza kuliko mali yoyote aliyonayo na hii ni kwa sababu huyu ameweza kuona bayana namna kadi ile inavyomsaidia kwenye huduma za mamilioni ya fedha kwa maisha yake yote.

Binafsi na mtu mwenye mapenzi mema atakubaliana nami kuwa kila mwananchi anatamani kuwa na Bima ya Afya ambayo kimsingi huduma zake huwezi kulinganisha na utaratibu mwingine wa kupata huduma za afya mfano, huduma za matibabu kupitia NHIF zinapatikana nchi nzima.

Ni dhahiri kuwa Muswada unaopendekezwa unalenga kuleta usawa katika upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wananchi wote kupitia kitita cha mafao ya huduma muhimu kitakachotolewa na kila skimu ya bima ya afya.

Mapendekezo ya Muswada yanatoa fursa kwa wafanyakazi walio katika sekta rasmi binafsi na wananchi wa sekta isiyo rasmi kuchagua aina ya skimu ya bima ya afya kulingana na mahitaji yao. Hivyo, propaganda inayofanyika juu ya SHIB na NHIF kuwa Muswada unalenga kuhamisha wanachama kutoka NSSF SHIB kwenda NHIF sio sahihi na ni upotoshaji mkubwa na jambo la msingi hapa ni kuangalia faida watakazopata wanachama hao wa SHIB kwa kuhudumiwa na Skimu watakayoichagua.

Kwanza inashangaza sana, SHIB IMEANZISHWA MIAKA MINGI ILIYOPITA NA KAMA INGEKUWA INAFANYA VIZURI KATIKA ENEO LA MATIBABU INGEKUWA NA IDADI KUBWA YA WANACHAMA LAKINI TAKWIMU ZINAONESHA TANGU KUANZISHWA KWA FAO HILO MWAKA 2005 HADI KUFIKIA MWAKA 2021 NI ASILIMIA 0.3 YA WANANCHI WOTE NDIYO WAMEJIUNGA. Kwa takwimu hizo kigezo kuwa fao la matibabu (SHIB) linavutia wananchi wengi kujiunga ni upotoshaji.

Naomba nieleweke kuwa hoja yangu ya msingi hapa ni tuunge mkono utaratibu mzuri unaopendekezwa na Serikali yetu wa kupata huduma za matibabu kupitia Muswada wa Bima ya Afya kwa wote na tuache ubinafsi wa kutaka kulaghai watu ili wabaki na huduma ambazo kimsingi hazikidhi mahitaji.

Kongole sana kwa Serikali ya Mama Samia kwa namna ambavyo imeweza kuonesha njia katika hili kuwa inawezekana kwa kila mwananchi kuwa na bima ya afya na tukaondokana na changamoto zilizopo kwa sasa.

Mtetezi Afya za Watanzania
 
Ni nadhani ni vema Serikali yetu iangalie vema haya masuala ya bima ya afya ili mtu akiwa na bima apate matibabu yote ya msingi. Kama mwanachama wa SHIB unapangiwa vituo vya kuhudumiwa ukipata changamoto inabidi ulipe kwa cash. Kama huna unakufa. Mi nashauri Serikali ilitazame hili hasa kwa sisi wajasiriamali wadogo
 
Back
Top Bottom