Yanayojiri Siasa za Msumbiji

Yanayojiri Siasa za Msumbiji

katusyo

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2013
Posts
1,455
Reaction score
434
Nchi ya Msumbiji yaingiwa na hofu kali ya kuingia vitani tena, baada ya mwanasiasa wa chama cha RENAMO kutekwa hapo jana akiwa maskani kwake Beira, habari zinasema, maaskofu ndio waliomwita kutoka porini ili kumuomba kwa amani baada ya kuhisi anaweza kufanya kitu kibaya, kufuatia kumkosa kumuua wiki juzi huko tete, akihojiwa na waandishi wa habari Dhlakama amesema, mwisho wa Dhlakama sio mwisho wa RENAMO, kuna Dhlakama atakae kuja huyu atakuwa hatari kuliko mimi, na amesema nataka nione jinsi demokrasia inavyovunjwa Mozambique.

Nikiripoti kutoka mMsumbiji mimi ni katusyo wa JamiiForums
 
Tueleze Jk alikuwa huko hivi majuzi, vipi hao jirani zetu wa kisini wanamuongeleaje?... je nao wanafatilia siasa za kwetu kwa kiwango gani?
 
Katusyo wa JF ahsante kwa taarifa yako. Tunaendelea! Taarifa kutoka Zanzibar zinasema.........
 
Tueleze Jk alikuwa huko hivi majuzi, vipi hao jirani zetu wa kisini wanamuongeleaje?... je nao wanafatilia siasa za kwetu kwa kiwango gani?

Kikwete alikuwa huku juzi alikuwa maputo, jana alikuwa pemba, amezungumza masuala ya amani huku akiviomba vyama vyote kukaa chini kwani vita sio vizuri, pia ametumia nafasi hiyo kuwaaga, lakini pia kuhusu kufuatilia siasa za tanzania wanafuatilia sana, chama kilichopo madarakani frelimo ni chama rafiki sana na ccm, kitu kinachopelekea wapinzani hasa dhlakama kuichukia sana tanzania kwani anadai hujuma nyingi tanzania inahusika na huyu jamaa anapendwa sana na wananchi, licha ya kuwa na jeshi la makomandoo mstuni
 
Nashukuru kwa kunipa picha ya huko.
 
Mara nyingi naskia Tanzania iliwakomboa Msumbiji, sasa mbona bado naona kama wanatafuta ukombozi kila uchao.
 
Hata Kenya imepata uhuru juzi hapa baada ya kupata katiba mpya,Kenya haikuwa huru, mpaka mlipotembeza bakora, wewe hujaitwa icc!!!!!!! Jumapili njema
 
Jamani katusyo yupo? Nasikia mabus yanapigwa risasi kila siku msumbiji
 
Mara nyingi naskia Tanzania iliwakomboa Msumbiji, sasa mbona bado naona kama wanatafuta ukombozi kila uchao.
Ccm inachokifanya tz ni sawa na kule.kwa ikizidiwa na upinzani ujue hata huko matokeo ni Yale yale
 
Back
Top Bottom