Yanayojiri Mwanza Mjini: RC, DC na CD hawataweza tena kukalia ofisi zao

Anguko la serikali hii ni pale tu watakapojitokeza viongozi watakaokua tayari kujiuzuru kwa kushindwana na aliye wateua.
Ningekuwa mie ndo mmoja wa viongozi mwanza, ngejiuzulu. Watu wamefanya kazi nzuri, then mtu anawatibua just to gain sympathy? Bukoba wanamsubiri
 
Mie nilifikiri raisi angewasiliana nao kimya kimya na kuwapa 'amri' ambayo wangetekeleza. Hii ya raisi kuongea na media kuhusu wateule wake na kutoa amri haijakaa vzr kabisa!
Ila hawa nao wamezidi kiburi. Ona kama alivyosema mdau hapo juu kuwa RC Mwanza Mongela alipokuwa anazunguka jana kabla ya tamko la Rais na mama mmoja akatamka "Mungu anawaona" akaambulia kukamatwa na kuwekwa mahabusu. Jee kulikuwa na sababu gani ya kumkamata na kumuweka ndani kwa kauli hiyo kama sio kiburi na kulewa madaraka? Kwani kusema Mungu anakuona ni tusi? Wakati mwingine wacha wakomeshwe hata kuwafukuza kazi hadharani ni sawa tuu
 
Binafsi sioni kama kuna tatizo kuwaondoa wamachinga katika barabara sio Mwanza tu hata Singida wapo, Dodoma, morogoro kote hali ni ile ile. Kama taifa tunahitaji kuacha biashara holela barabarani na kutafuta sehemu rasmi za kufanya biashara. Hawa viongozi wa Jiji la mwanza siwezi kuwalaumu kwa maamuzi waliofanya bali namlaumu Asiyejaribiwa kwa kuingilia mipango miji.
Naamini anafanya kisiasa zaidi na wala sio katika UTU. hata kama alikuwa na hoja alipaswa ashauri tu namna nzuri ya kutekeleza uhamishaji wa biashara hizi holela barabarani.
Hawa jamaa wataendelea kukaa ofisini simply because wanahitaji kazi hizo na pia kubwa kwao ni kuendelea kuitwa MKUU hata kama hawatakuwa na la kufanya jipya zaidi ya kungoja salary na kusubiri siku ziende.
 
Hebu nimnukuu Mwandishi Kondo Tutindaga katika Mwanahalisi la Jumatatu Decemba 5-11,2016, anaposema, "...lakini kwa hulka yake na matendo yake, ni dhahiri aweza kuwa anafurahia mateso ya watu. Ni mtu anayemkanyaga mtu na mtu huyo akilia, rais aweza kuwa anacheka kwa furaha"
Nimeyatafakari sana maneno hayo ya Mwndishi Kondo. Pamoja na ukweli kuwa ustawi wa Machinga ni muhimu, lakini je, hakukuwa na njia nyingine ya kufikisha ujumbe wa kusitisha zoezi hadi iwe ni lazima kuwadhalilisha viongozi hawa?
Sasa ninaanza kuamini kuwa tuna kiongozi mwenye hulka ya kutaka sifa bila kujali kuwa kwa kufanya hivyo anawaumiza wengine!!!

Umechelewa tu kuamini kuwa
 
FM Radio zote za jijini Mwanza sasa hivi ni mjadala wa maamuzi ya Rais na zinawekwa Clip za matamko ya Mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya Nyamagana na Mkurugenzi (CD) wa jiji kuhusu suala la wamachinga waliyotoa siku zilizopita kuhusu suala hilo na kuonekana kuwa walikuwa tofauti kabisa na hiki alichosema Rais.

Hata mbunge wa Nyamagana alipohojiwa amepata nafasi ya kuwaruka kabisa viongozi hao kiasi cha kuonyesha maamuzi yao yalikuwa yao pekee kwa nia ya kukomoa Wamachinga na mama ntilie.

Hii ni fedheha kubwa sana kwa wateule hao wa kisiasa na kiutendaji na wanakosa kabisa sifa ya kuendelea kuwaongoza watu wa Mwanza kwa siku zijazo kwani hawawezi tena kuwa na maamuzi ambayo yatakuwa yamesimama bila kudharauliwa.

Je, wataamua wenyewe kujiuzulu ili kulinda heshima zao au watataka waendelee kufanya kazi kama picha tuu? Maana kila anayehojiwa mtaani anawaponda na kuwadharau kuwa kazi imewashinda ndio maana aliyewateua kaamua kuifanya mwenyewe.
Weka hizo clip tuwasikie wanafik
 
kWANI UMESAHAU ILE YA ......................NITUMBUEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE......................... WAKAMJIBU TUMBUAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA...................AKATUMBUA.....................AKAPOTEZA MAISHA.
 
FM Radio zote za jijini Mwanza sasa hivi ni mjadala wa maamuzi ya Rais na zinawekwa Clip za matamko ya Mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya Nyamagana na Mkurugenzi (CD) wa jiji kuhusu suala la wamachinga waliyotoa siku zilizopita kuhusu suala hilo na kuonekana kuwa walikuwa tofauti kabisa na hiki alichosema Rais.

Hata mbunge wa Nyamagana alipohojiwa amepata nafasi ya kuwaruka kabisa viongozi hao kiasi cha kuonyesha maamuzi yao yalikuwa yao pekee kwa nia ya kukomoa Wamachinga na mama ntilie.

Hii ni fedheha kubwa sana kwa wateule hao wa kisiasa na kiutendaji na wanakosa kabisa sifa ya kuendelea kuwaongoza watu wa Mwanza kwa siku zijazo kwani hawawezi tena kuwa na maamuzi ambayo yatakuwa yamesimama bila kudharauliwa.

Je, wataamua wenyewe kujiuzulu ili kulinda heshima zao au watataka waendelee kufanya kazi kama picha tuu? Maana kila anayehojiwa mtaani anawaponda na kuwadharau kuwa kazi imewashinda ndio maana aliyewateua kaamua kuifanya mwenyewe.
Aaaa thubutuuuu kujiuzulu kwa kusutwa na dhamira kwa Tanzania tusubiri miaka mia moja mpaka kizazi hiki kisichokuwa na soni kitakapo isha.
 
Hivi sera ya serikali kuhusu wamachinga wanaofanya bishahara katika maeneo yasiyoruhusiwa, ni ipi hasa???? Kila siku JPM anakumbusha wananchi kufuata sheria, na juzi juzi katoa mifano kadhaa kuhusu waliojenga katika road reserves. Sasa najiuliza: Huyu Machinga anayekwenda kufanya biashara mitaani, barabarani na katika maeneo yasiyoruhusiwa, anavunja au havunji sheria? Je huyu ana tofauti gani na yule anayejenga kwenye road reserve, au bondeni????? Kuna wakati kuishi katika nchi hii unapaswa kuwa kama kichaa! You repeatedly hear and see so many things that don't make sense......
 
Usaliti aupo kwenye mapenzi tu kwenye siasa na swala zima la uongozi nijambo la kawaida Sana. Mtayaona mengi yanakuja mbele.
 
Mie nilifikiri raisi angewasiliana nao kimya kimya na kuwapa 'amri' ambayo wangetekeleza. Hii ya raisi kuongea na media kuhusu wateule wake na kutoa amri haijakaa vzr kabisa!
Hivyo hivyo alivyofanya inafaa maana aliwaambia hadharani "wasiwabugudhi hadi wawaandalie sehemu" wakakubali hadharani je walifanya hivyo?
 
Sasa mbona alichelewa hadi kumekuwa na upotevu wa rasilimali pesa, muda na mengineyo! si angewapa hizo "za uso" tarehe 1/12/2016 kabla hao machinga hawajapoteza mali zao na pia serikali haijatumia rasilimali watu eg. askari, au magari, pesa na vinginevyo. Mgambo walikuwa karibia 900 na kila siku walikuwa wanalipwa Tshs.10,000/=. Issue ni kwamba hilo zuio angelitoa mapema.
Wanatakiwa walipe hizo pesa zote zilizotumika hapo maana walijua fika wanafanya tofauti na maagizo ya mkuu wao.
 
Hili la machinga wa Mwanza halina tofauti na lile la kuzima Mwenge Simiyu...anawavizia wateule wale, anawasubiri watende wakiwa na baraka zake zote ndipo yeye ajitokeze na kujifanya yuko kinyume nao, mawazo ya kutetea Urais wake mwaka 2020 yatamwua ngosha hakyanani
 
FM Radio zote za jijini Mwanza sasa hivi ni mjadala wa maamuzi ya Rais na zinawekwa Clip za matamko ya Mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya Nyamagana na Mkurugenzi (CD) wa jiji kuhusu suala la wamachinga waliyotoa siku zilizopita kuhusu suala hilo na kuonekana kuwa walikuwa tofauti kabisa na hiki alichosema Rais.

Hata mbunge wa Nyamagana alipohojiwa amepata nafasi ya kuwaruka kabisa viongozi hao kiasi cha kuonyesha maamuzi yao yalikuwa yao pekee kwa nia ya kukomoa Wamachinga na mama ntilie.

Hii ni fedheha kubwa sana kwa wateule hao wa kisiasa na kiutendaji na wanakosa kabisa sifa ya kuendelea kuwaongoza watu wa Mwanza kwa siku zijazo kwani hawawezi tena kuwa na maamuzi ambayo yatakuwa yamesimama bila kudharauliwa.

Je, wataamua wenyewe kujiuzulu ili kulinda heshima zao au watataka waendelee kufanya kazi kama picha tuu? Maana kila anayehojiwa mtaani anawaponda na kuwadharau kuwa kazi imewashinda ndio maana aliyewateua kaamua kuifanya mwenyewe.
Mabula ni mnafiki alipo kuwa kaimu meya wa Jiji la Mwanza 2010/2015 alikuwa akiwachukia sana machinga alikuwa akingombana sana na wenje kisa machnga Leo hii anajifanya anumia sana na kuwatupia lawama viongozi wenzie
 
Tumekuwa tukipiga kelele kila siku kuwa hii nchi imekuwa ni nchi ya matamko...kila MKUU anatamka kulingana na sehemu anayoitawala. Kuwaondoa machinga inaweza ikawa sio kosa kulingana na sheria ambazo jiji limetunga na kukubarika. Mimi tatizo langu ni jinsi zoezi lilivyochukuliwa na matamko makali ya wakuu wetu, pia hawa watu wa jiji kwa nini wasiwe na master plan? Kwa nini kuwe na kuviziana kusikoisha? Machinga wameanza kusumbuliwa siku nyingi hapa Mwanza. Kabla ya langolango ( Mlango mmoja), machinga walikuwa Makoroboi. Wakahamishwa wote na Makoroboi ikawa wazi, mambo yakaenda yanabadirika tokana na nchi yetu kutawaliwa na siasa kwa kila jambo, machinga wakarudi tena na wakaweka makao!!!
Hapo ndo huwa nashika kichwa, hatuna mipango miji mathubuti? Kwa nini hili suala limekuwa kila awamu linatusumbua? Kwa nini lisitafutiwe suruhu?
Leo limemalizwa kisiasa,na nionavyo mimi hawa watendaji (RC,DCs&CD) watakuwa wamenywea kiasi kwamba hawatathubutu kuongelea tena machinga,tusubiri tena baada ya uchaguzi wa 2020 hili suala la machinga kuibuka tena......
Na hawa watendaji pia RC,DC & CD sio lazima waambiwe kustep down kwa kusikiliza tu ile lugha ya mkuu wao wa kazi ni dhahiri kabisa kawaona use less. Nina uhakika mkuu alifuatilia mchakato wote wa kuwatoa machinag toka wanapewa siku saba. Alikuwa na uwezo wa kuwapa maelekezo ya kusimamisha zoezi na upande mwingine kwa hawa watendaji pia,walitakiwa wapate ushari toka tamisemi maana mkuu alikuwa kawaruhusu machinga kuendesha biashara zao bila kusumbuliwa!
Kwa hivyo,wateule hawa yawapasa kujipeleleza wenyewe kama bado wanafaa kuendelea na nyazifa hizo au la!
 
NAAMIN KUNA WATEULE WAKE KWA MAKUSUD WATAKUWA WANAMKWAMISHA KTK BAADH YA MAMBO, YE C ONE MAN ARMY, KITU KTAKACHOWAATHIL WENYEWE NA TAIFA
 
Hapo jumlisha na vitendo alivyowafanyia watu RC kulazimisha wafanyabiashara kuzoa taka kwenye mitaro michafu kwa mikono na mwanamke aliyesema Mungu anakuona kumweka ndani, nafasi ya RC kuendelea na kazi ndani ya Mwanza ni kama kutundika picha ukutani tuu
 
Back
Top Bottom