Ijumaa ya Fat-wah Mwanza; RC na RPC Si siku ya Kukaa Ofisini leo

Status
Not open for further replies.

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Ijumaa ya Fat-wah Mwanza; RC na RPC Si siku ya Kukaa Ofisini leo
  • Kanisa lachomwa Moto
  • Maandamano makubwa kufanyika kuelekea eneo laTukio
Uzembe wa kuchukua hatua mapema kwa viongozi wetu ni kansa iliyokosa Tiba katika serikali za awamu katika miongo kadhaa iliyopita.Jana tuliandika hapa kuhusu athari za Viongozi wa Dini kujihusisha na siasa na kushau wajibu wao tukitegemea kuwa ilikuwa ni chanzo kizuri kwa wao kufanya kazi kwa haraka kwa kutumia taarifa za kiintelijensia kutanzua kadhia hiyo ya Mwanza.

Bahati mbaya sana hata wachangiaji waliochangia thread hiyo wengi waligubigwa na hamaki za imani za kidini badala ya kuzingatia mkondo wa sheria na kupeana mawazo chanya yatakayokomesha matabaka ya kidini na kuchanganywa siasa na Dini. (Thanks kwa invisible kutumia hekima kuifunga thread hiyo, hata hii ikipinda leo; Mkuu ifunge pia)

Tusisukumwe sana na ushabiki wa kidini na kusahau shaeria za Nchi na kutaka kuamua mambo kwa hamaki na kudhihakiana imani za kila mmoja tuweke umoja na utaifa mbele ili kuhakikisha tunajenga kuheshimiana kila mtu katika kuabudu kwake hata kama kuabudu huku ni kule kwa mapangoni.

Napoandika thread hii na utangulizi huo ambao sitapenda kabisa ufungamanishwe na ushabiki wa kidini ndugu yangu Mkuu wa Mkoa mpya EVARIST WELLE NDIKILO na Kamanda wa Jsehi la Polisi Mwanza leo si siku ya ninyi kukaa Ofisini wala kujipanga na weekend. Fat-wah kubwa inayotarajiwa kufanyika Mwanza leo ni hatari kama hekima haitatumika mapema kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Inawezekana kabisa Viongozi wa Dini ya Kiislam wakawafuata leo kushauriana katika hili au wasifuate kabisa kutokana na presha kubwa iliyopo kwa baadhi ya waumini wasiokuwa wasikivu kutokana na kadhia ya kuchomwa moto kwa Quran hapo majuzi.

Jana kucheleweshwa kwa maamuzi na ufinyu wa taarifa za kiintelijensia ulitoa mwanya kwa baadhi ya kundi la watu wasiojulikana kuchoma moto kanisa ambalo wanadaiwa kutoa waumini waliochoma moto Quran.

Ni bahati nzuri kuwa uharibifu na moto vilidhibitiwa mapema, bahati mbaya ni kwamaba mamlaka husika ziliteleza kuchukua udhibiti wa tukio zima toka hadhari ya mapema hapa JF ambayo tunajua mnasoma na mnatambua kuwa tunafanya hivi si kwa uchochezi bali kuwapa nyongeza katika intelijensia iliyofeli na matokeo yake tunaishia kulaumiana katika maafa.


Kwa moyo wa kujishusha kabisa watafuteni viongozi wa Dini ya Kiisalam Mwanza, Sheikh wa Mkoa Salum Fereji na wasaidizi wake wawaweke pamoja maimam na kuhahakikisha hii fat-wah inayokusudiwa kufanyiak leo Jijini Mwanza baada ya sala ya Ijumaa haifanyiki na ibada ziendelee kama kawaida huku sheria ikichukua mkondo kwa waliochoma Quran na waliochoma kanisa kwa pamoja.

Kalam na fikara zangu zimenituma kuyasema haya baada ya kupata taarifa muda si mrefu kutoka Mwanza kuwa hali si ya kuridhisha juu ya suala hili. Hofu na mashaka ni mazito na madhara yatakuwa makubwa kama hekima haitatumika mapema.

ADIOS


UPDATES:

Kikao kati ya RC, Sheikh wa Mkoa, Imam wa Msikiti wa Furqaan Lumala na Viongozi wengine kimefanikisha kuzima Jaribio la Fat-wah kubwa iliyotarajiwa leo Mwanza. Uamuzi wa Busara na Mazungumzo yamefanikisha hili...Kumbe inawezekana kabisa.

Misikiti mingi inaarifiwa kuhudhuriwa na waumini wachache katika sala ya Ijumaa huko Mwanza hasa katika Vitongoji vinavozunguka LUMALA, maeneo ya Kilimahewa, Pasiansi, Ilemela na Nyasaka. Inahofiwa waumini wengi walijiunga katika misikiti iliyotangaza hapo jana kufanya maandamano kwenda Lumala na wengine wengi wakisali Lumala kutegemea tamko lolote la kisasi.

Hekima na Subira vimefanikiwa.

Angalizo:

Sauti za chini zinashinikiza Polisi kukamilisha Upelelezi haraka na Mahakama kuendeshan kesi hiyo kwa uwazi na haraka ili kuepusha kadhia nyingine kwani viongozi wamewasihi waumini wao kubuta subira hadi muafaka utakapopatikana.

Source: Afisa Jeshi la Polisi Mza (Jina limehifadhiwa)
 

Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,127
Wote wamekosa religous tolerance. Better be neutral rather than being fundamentalist. God is one.

Wajinga wa kwanza ni wale walioamua kuchoma Quran wakati haina kosa lolote. Kama ndugu zetu mnavyolinda utukufu wa Yesu kristo na dhana nzima ya Utatu na waislamu kwao Quran ni kitabu kitukufu.

Hivyo basi kitendo walichokifanya wale fundamentalist wa kilokole kuchoma moto quran lilikuwa kosa lisiloweza kuvumilika na kukosa hekima ni vema wakachukuliwa hatua hao kwanza kabla hamjageukia waislamu. ACHENI UNAFIKI WENU HAPA!!!

Sishabikii ujinga huu kabisa watu wanakosa hekima na logic na kuishia kufanya jambo kwa imani na emotion zao matokeo yake ndio hayo sasa.
 

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
58,617
116,770
Wajinga wa kwanza ni wale walioamua kuchoma Quran wakati haina kosa lolote. Kama ndugu zetu mnavyolinda utukufu wa Yesu kristo na dhana nzima ya Utatu na waislamu kwao Quran ni kitabu kitukufu.

Hivyo basi kitendo walichokifanya wale fundamentalist wa kilokole kuchoma moto quran lilikuwa kosa lisiloweza kuvumilika na kukosa hekima ni vema wakachukuliwa hatua hao kwanza kabla hamjageukia waislamu. ACHENI UNAFIKI WENU HAPA!!!

Sishabikii ujinga huu kabisa watu wanakosa hekima na logic na kuishia kufanya jambo kwa imani na emotion zao matokeo yake ndio hayo sasa.
Punguza jazba vuta pumzi then tafakari.

Ni kweli hatua ianze kwa kosa la kwanza then na la pili pia lichukuliwe hatua. Hata lile la DC mbakaji wa demokrasia, sheria ichukue mkondo wake kwa kosa la kwanza la kufanya mkutano batili na la hijab lifuatie baadae.
 

BabieWana

Senior Member
Nov 3, 2010
178
29
ofcourse hapa tulipo ndo pazuri maana kila mtu ni mdini asanteni walokole chomeni tena na tena quran waislam watasubiri polisi wawashughulikie.
Nchi ni yenu shaka yao ninini?
 

maulaga

JF-Expert Member
Feb 22, 2009
472
120
Wajinga wa kwanza ni wale walioamua kuchoma Quran wakati haina kosa lolote. Kama ndugu zetu mnavyolinda utukufu wa Yesu kristo na dhana nzima ya utatu na waislamu kwao Quran ni kitabu kitukufu. Hivyo basi kitendo walichokifanya wale fundamentalist wa kilokole kuchoma moto quran lilikuwa kosa lisiloweza kuvumilika na kukosa hekima ni vema wakachukuliwa hatua hao kwanza kabla hamjageukia waislamu. ACHENI UNAFIKI WENU HAPA!!!

Sishabikii ujinga huu kabisa watu wanakosa hekima na logic na kuishia kufanya jambo kwa imani na emotion zao matokeo yake ndio hayo sasa.
Ndugu yangu, kosa haliadhibiwi kwa kosa. Wapo watu wanaojitahidi kumsemea Mungu kana kwamba Mungu hana uwezo. Kwanini wasimuachie Mungu mwenyewe aliyekosewa akawaadhibu wakosaji? kwani wao wanatumia kipimo gani chakujua Mungu amekasirishwa kiasi gani na wakosaji?
 

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,768
892
Bado kidogo tu Waislam na Wakiristu waanze kuchapana na sijui itakuaje.

Tuombe mungu atuepushe na hiyo hali, naona tunapoelekea uvumilivu unazidi kutushinda pande zote mbili
 

MUHOGOJ

Member
Sep 13, 2011
11
3
Serikali, Jeshi, Polisi etc wote wako Igunga wanapasua vichwa namna ya kuchakachua matokeo, ila ndo hivyo wanabanwa mbavu na Chadema. Huko kwingine nyie endesheni maisha muonavyo tuu serikali imelala
 

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,316
Hii ni khatari kubwa.

UDINI umeshaanza kuimeng'enya Tanganyika. Bila Tz kulijua hilo na kuanzisha mjadala wa kitaifa kulijadili kwa kina na mapana yake basi kifo kitawaumbua.

Kwani hilo ni kama pembe la ng'ombe.
 

Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,127
Punguza jazba vuta pumzi then tafakari. Ni kweli hatua ianze kwa kosa la kwanza then na la pili pia lichukuliwe hatua. Hata lile la DC mbakaji wa demokrasia, sheria ichukue mkondo wake kwa kosa la kwanza la kufanya mkutano batili na la hijab lifuatie baadae.

Mkuu,

Mie sina jazba ila nasema ifikie wakati watu wawe na logic na kutafakari haingiii akilini kuchoma msahafu haujakufanyia kosa lolote. Kama hukubaliani nao si uache kama ulivyo na sio kuchoma moto. Muanzishaji mada alitakiwa kwanza akemee kitendo cha watu kuchoma msahafu usio na hatia yeyote ndipo aje katika Fatwa ya waislamu.

Kuhusu mada ya DC mie hukunioa kuchangia wala kusema kitu chochote kwani nasubiria mahakama kwanza tujue ilikuwaje kuwaje hadi wakafikia hapo walipofika. Ila hili la kuchoma msahafu ni upumbavu na ujinga na it is unacceptable kwani msahafu haujawafanyia kitu chochote it is just book that express certain ideas na ideology of which to muslims it is believed to be a sacred book.
 

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,316
Hii ni khatari kubwa.

UDINI umeshaanza kuimeng'enya Tanganyika. Bila Tz kulijua hilo na kuanzisha mjadala wa kitaifa kulijadili kwa kina na mapana yake basi kifo kitawaumbua.

Kwani hilo ni kama pembe la ng'ombe.
 

gepema

Member
Mar 25, 2010
97
9
Tujaribu kujiangalia sana kama mtu binafsi na kama taifa lakini kwa aina hii ya bora liende tutakuja kulia sote!!
 

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
58,617
116,770
Hii ni khatari kubwa.

UDINI umeshaanza kuimeng'enya Tanganyika. Bila Tz kulijua hilo na kuanzisha mjadala wa kitaifa kulijadili kwa kina na mapana yake basi kifo kitawaumbua.

Kwani hilo ni kama pembe la ng'ombe.
Wewe ndo hulijui hili coz sio mTz tangu ndoa imekubadilisha uraia huko uarabuni. Sisi wa TZ tulilijua hili mapema tangu CCM waweke sera ya KADHI kwenye chama chao tulishalitabiri hili coz kuna dini flani imejiona bora zaidi baada ya kuwekewa mahamaka yao kama sera ya CCM. Vipi leo hapo uarabuni hakuna walau kijimechi cha kombe la kuku hapo mtaani?
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
46,427
62,544
Ningekuwa RC au RPC ningekusanya wote kwanza na kuwahifadhi Lupango kisha waeleze huo umbea wa kushabikia mambo ya wageni ulianza lini? kama ni dini ni yako sisi wengine haitusaidiii, kama unaabudu Kuran, Biblia, Ng'ombe au jiwe that should be none of our business, wasituaondelee concentration ya kuiondoa CCM
 

Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,230
Ningekuwa RC au RPC ningekusanya wote kwanza na kuwahifadhi Lupango kisha waeleze huo umbea wa kushabikia mambo ya wageni ulianza lini? kama ni dini ni yako sisi wengine haitusaidiii, kama unaabudu Kuran, Biblia, Ng'ombe au jiwe that should be none of our business, wasituaondelee concentration ya kuiondoa CCM

Uwaweke lupango kwa kosa gani? Wote ni kina nani?
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

7 Reactions
Reply
Top Bottom