Jinsi CCM itavyonufaika na vurugu katika mikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza kwa kigezo cha Maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi CCM itavyonufaika na vurugu katika mikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza kwa kigezo cha Maendeleo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Losambo, Nov 14, 2011.

 1. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndg WanaJF,
  Itakumbukwa kuwa mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha, Dar – es – Salaam n.k ilikuwa ikiwakilishwa na wabunge toka CCM bila shaka kabla ya uchaguzi wa 2010. Mara baada ya uchaguzi, baadhi ya majimbo mengi makubwa yaliangukia chini ya upinzani. Baadhi ya majimbo hayo ni Mbeya Mjini, Arusha Mjini, Mwanza Mjini n.k

  Tokea matokeo hayo yatangazwe mikoa hiyo hususani majimbo niliyoyataja hapo juu yamekuwa yakikabiliwa na vurugu za mara kwa mara. Vurugu hizo zimepelekea wabunge wanaowakilisha majimbo hayo kupakwa matope kuwa ndiyo wanaochochea vurugu na hivyo kuzorotesha maendeleo ya majimbo yao!
  Hili limeanza kuingia akilini kwa baadhi ya wananchi. Lakini mimi leo hii naomba nipingane na propaganda hiyo ambayo haina mantiki kabisa kwa muono wangu kama Losambo kwa kuangalia mikoa yote mitatu yaani Arusha, Mwanza na Mbeya.

  ARUSHA

  Kama upo makini matokeo ya mikoa yote niliyoitaja nguvu kubwa sana ilitumika kutangaza matokeo hali iliyoashiria kulikuwa na dalili mbaya ya kutaka kuchakachua matokeo. Baada ya matokeo kutangazwa ni wazi kulikuwa na juhudi za makusudi kuhakikisha majimbo hayo hayaongozwi na mameya kutoka upinzani!
  Hiki ndicho kiini cha tatizo la vurugu Arusha. Baada ya meya wa Arusha kupatika katika mazingira yenye utata, CDM waliandaa maandamano yaliyopelekea watu watatu (03) kufa na mamia kujeruhiwa.
  Hili lilipelekea waziri mkuu Pinda kuingilia kati kwa lengo la kutafuta suluhu ambayo hadi leo bado haijapatikana.
  Wakati kiini cha mgogoro hakijapatiwa ufumbuzi yaani mgogoro wa meya, hivi majuzi tena kumetokea vurugu zilizopelekea viongozi wa CDM, Dr. W. Slaa, F. Mbowe, T. Lissu pamoja na wafuasi wao kufunguliwa mashitaka kwa kosa la uchochezi na kufanya mkutano kinyume na sheria.

  Ukichunguza kwa makini kuna madai ya msingi ambayo serikali ya CCM haitaki kuyapa nguvu kwa kigezo cha kuipa nguvu CDM. Kiukweli, katika vurugu za majuzi ni ujinga wa hakimu kushindwa kutumia busara kwa kumnyima dhamana mbunge wa Arusha Ndg G. Lema tu ndiko kulikopelekea mambo yote hayo! Tujiulize kwa nini Lema alinyimwa dhamana;

  • Kwanza kitendo chake cha kukataa dhamana wakati alikuwa na uwezo wa kujidhamini ilikuwa dharau kwa mahakama. Ok, nakubaliana na hakimu lakini ndiyo nae alipize kisasi eti kwa sababu G. Lema aliidharau mahakama kwa kumwambia siku hiyo haikuwa siku ya kesi yake hivyo wadhamini wake waje 14.11.2011 ambapo ndipo shauri lake lilipangwa kusikilizwa? Hekima yake kukosekana ndiyo imesababisha vurugu zile pale NMC. Pamoja na hayo G. Lema alikuwa na madai yake na kwa mujibu wa akili yake aliona ndiyo njia labda ya kuyafikisha kwa wahusika kwa urahisi zaidi.
  • Pili na kubwa, ni serikali kuzima shamra shamra za G. Lema kupokelewa kama shujaa toka jela. Ni wazi G. Lema alikuwa ameandaliwa maandalizi makubwa sana Arusha na Dodoma kiujumla! Sasa ili kuvuruga hayo, ikaonekana Lema anyimwe dhamana technically siku ile.
  Katika yote hayo usisahau wimbo unatakiwa kuingizwa akili mwa watu wa MAENDELEO kutopatikana kwa kuwachagua wabunge wahuni ambao bado hawajaliza starehe na hivyo kutojua nini waache na nini wafanye.

  MWANZA

  Tatizo la Mwanza ni la Wamachinga. Kumekuwa na tabia kabla ya uchaguzi vitu kuacha vifanywe kiholela hata kama watu wanavunja sheria kwa kigezo cha kutokosa kura.
  Ukichunguza masoko mengi Arusha, Mwanza na hata Mbeya kuna biashara za wamachinga na akina mama zinazofanywa katika maeneo yasiyoruhusiwa. Wafanyabiashara hao wamekuwa wakipata usumbufu wa mara kwa mara toka kwa mgambo wa jiji licha ya kulipa kodi za manispaa kama kawaida.
  Mara baada ya uchaguzi serikali husahau kuwa iliwaachia huru kipindi cha uchaguzi na sasa wameshajenga mazoea na kuamua kuwafukuza ghafla.
  Inapotokea mvutano kuwa mkubwa, serikali hutumia mwanya huo kisiasa kwa kusema kuna mkono wa viongozi wa vyama vya upinzani hususani CDM. Lakini imesahau kiini cha mgogoro ni ukosefu wa ajira na udhaifu wa serikali kukurupuka kuwafukuza watu bila kuwaonyesha maeneo mbadala ambayo yanakidhi haja.
  Hili serikali haitaki kulisemea na kukimbilia vurugu hizo kusababishwa na wabunge wa CDM waliowachagua ili watu wajutie maamuzi yao, japokuwa si dhambi kujutia maamuzi kama kweli umekosea.

  MBEYA

  Kinachotokea Mbeya kinafana kidogo na Mwanza hivyo sioni haja ya kuongelea kitu kinachofanana. Mbeya iliunguliwa na masoko karibu mawili hivi karibuni, hivyo ni tumaini langu wamachinga wengi watakuwa wamekimbilia eneo moja na kuonekana kama vurugu.

  Naomba sasa niunganishe nilichokisema kwa title ya thread yangu na hayo hapo juu.

  Ni ukweli usiopingika kuwa hivi sasa hali ya serikali kifedha ni mbaya na hivyo inachohangaika saizi siyo vurugu zinazoendelea bali kujinasua na aibu ya kushindwa kujiendesha! Serikali inahangaika ipate wapi fedha za kulipa wafanyakazi wake wasiozidi million moja na matumizi mengine.
  Hili la kuwa serikali ina hali mbaya kifedha limeshaanza kuonekana kwa baadhi ya wafanyakazi kuchelewa kupata mishahara, wizara nyingi kutopata migawo kama ilivyo kawaida na kusimama kwa miradi mingi ya maendeleo kwa kuwa serikali haijalipa madeni ya wakandarasi kwa muda mrefu! Mengine ni siri lakini wajio jikoni wanajua serikali ipo ICU kimapato.

  Sasa hili la vurugu linafurahiwaje na serikali ya CCM? Ni rahisi kwa sababu serikali yenyewe inatambua hata kama kungekuwa na amani kiasi cha mtu yoyote kutopigwa hata kibao isingefanya chochote cha maana, hivyo vurugu hizo zinawapunguzia kujibia maswali na hoja nzito kwa nini imeshindwa kuleta maendeleo licha ya amani na utulivu uliotawala.
  Kitakachofanyika ni kuvuna matunda ya mbegu inayopandwa saizi kwa wananchi kuwa wameshachemsha kuwachagua wabunge wanaohamasisha vurugu na migogoro hivyo wasahau maendeleo. Na hili litachagizwa na viongozi vichwa ngumu ambao hawataisha kuanzisha migogoro ya mara kwa na wabunge hao ili wahemkwe na kuanzisha vurugu na kufunguliwa makesi yasiyokwisha.

  Suala la maendeleo yatapatika kwa kuwa miradi mingi haifadhiliwi na serikali ya Tanzania bali ama ni mikopo au misaada toka banki ya dunia au vinginevyo. Hebu jiulize ni miradi mingapi iliyoendeshwa na serikali yenyewe mpaka ikakamilika bila msaada toka taasisi hizo nilizozitaj ahapo juu. Halafu kinachoitwa vurugu ambazo zinaweza kutishia katika mikoa hiyo bado hazionekani kuwa ni tishio kiasi cha kuhatarisha maendeleo, bali ni propaganda tu.

  Mwisho, nawakilisha wanaJF. Hii ni kwa kadiri ya uelewa wangu na vyanzo vyangu.
  Naomba mtakanijibu msini quote kwa sababu ya urefu wa maada na kuleta usumbufu kwa wasomaji. Nategemea changamoto nyingi kutoka kwenu.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hakyanani ukiwa kwenye Cafe na hii stori unaua watoto kwa njaa, na kama uko ofisini unafutwa kazi!
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  stor haina summary yaani point haionekani
   
 4. tikatika

  tikatika JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,670
  Likes Received: 2,205
  Trophy Points: 280
  uko sahihi mkuu , japo umeweka wigo wa kutokoselewa kwa ulefu wa wa topc pls jifunze kufupisha wengine wataongezea!

  SERIKALI INATAFUTA VICHAKA KUFICHA MAOVU YAKE JAPO NI VICHAKA VYA KARANGA VISIVYO WEZA KUSITILI HATA KIATU!
   
 5. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama hakuna point labda uwe na ushabiki fulani hivi.
   
 6. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  PakaJimmy huo ndiyo ukweli, na ukweli siku zote una gharama. Natumaini kama kweli upo ofisi ya serikali utakuwa huna chako.
   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sijui ndiyo kuchoka au kujizira hata sielewi?
   
 8. n

  nyuki dume JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo la Vurugu za Mwanza na Mbeya Mh Kandoro hawezi kukwepa lawama hizi, alipokuwa RC Mwanza yeye alihusika, amefika Mbeya amelianzisha tena kwa lile alichokiita kuliweka jiji la Mbeya katika hali usafi lakini walengwa ni wamachinga tu ambao ni vijana. Kandoro kama kweli ni mkweli atafute njia mbadala.
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  suala la lema kujipeleka mahabusu then tumlaum hakim naona ni kupotosha jamii hasa wale walio mbali.lema alijipeleka jela kutafuta umaarufu.
  suala la vurugu za wamachinga ktk majiji/miji mikubwa hapa nchini lilianzia dar pale kariakoo mtaa wa kongo, hali ilikuwa mbaya sana lakini leo hii wamachinga dar wanakula raha mana wametengewa maeneo maalum na yameboreshwa......mfano mzuri ni machinga complex...kwa hiyo basi ni kewli kabisa baadhi ya wabunge wa chadema wanashiriki kukwamisha maendeleo ya wananchi na sisi tunaoishi ktk majimbo hayo na tuliotoa kura zetu chadema sasa tunajuta......mbona dr slaa,zito,said arf ni wabunge wa chadema lakini hakuna ujinga,hakuna vurugu wala malalamiko??????????????????????????????????tunajta kuipa kura chadema.
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  wabunbe wa chadema wasipobadilika,2015 tunakula vichwa.
   
 11. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wapiga kura ndiyo watakaoamua endapo hakutakuwa na uchakachuaji.
   
 12. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hizo vurugu zinatokana na ubovu wa serikali. Wanaoandamana kudai haki, wanaandamana kwa sababu wamechoka uonevu wa serikali ya CCM, CDM imekuwa inawafungua watu macho, kudai haki zao. Mtu anaandamana si kwa ajili ya CDM bali haki yake.

  Mimi naona kwa jicho jingine kabisa. Migogoro hii inawafanya watu waichukie zaidi CCM na serikali yake, hasa pale inapotumia polisi kuua na kujeruhi. Timeona jinsi wanambeya walivyo msikia mbunge wao, wakasitisha vurugu. Watu wameichoka CCM, na hali itakuwa mbaya kwa uchaguzi mkuu ujao, maana vijana wengi watajiandikisha, hao wamachinga wanaosumbuliwa leo, watalipa machungu kwenye sanduku la kura, kama si kwa mtutu wa bunduki.
   
 13. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mi naona thread yako iko poa sana, umejikita kujadili unachokiamini na umeunganisha mantiki na mazingira uliyoyalenga, hvyo huna sababu ya kunitaka radhi....
  Suala la urefu wa hoja hilo halikwepeki kama hoja hzo zinamtiririko wenye kueleweka kwenye kuchanganua.
  Mengi uliyoyagusia ni sahihi sana,
  hoja hafifu ya "maendeleo" imekuwa ikitumika na serikali katika kuzima mwamko wa watu kuhoji masuala yao, mbele ya umma uliokandamizwa kifikra na wenye kufikiri ya leo tu na kwamba "mustakabali" utajijua ni rahisi sana kununua porojo hizi za serikali.
  Lakini bado tuna nafasi ya kujipa matumaini kwamba kasi ya mabadiliko ya kidunia katika uchumi na kuanguka kwa madola kutawafanya watz pia kuelekea kufanya mabadiliko hata kwa nguvu za upepo.
  Kama Igunga iliweza kuhamasika kiasi kile, naamini hayo majimbo ya mjini kama ulivyoyataja yananafasi zaidi kwenye kuwapima wabunge wao wa upinzani katika utendaji kazi kwa "KUWATUMIKIA"
   
 14. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Upo sahihi, ni kweli watu hawaandamani kwa ushawishi wa kijinga bali kudai haki zao za msingi. Ukichunguza migomo vyuo vikuu, wamachinga na hata kupinga malipo ya Dowans n.k kuna logic ndani yake inayowafanya watu wa risk maisha yao kupigwa mabomu na hata saa nyingine kupoteza maisha.
  Kwa hili la Wamachinga nadhani jana Lowassa alizungumzia kama changamoto dhidi ya serikali. Huwezi kumfukuza mtu ambaye anashazoea kupata 2000 au 3000 kwa siku na kuendesha maisha yake bila kumpa mbadala ya kufanya. Ni lazima utazua vurugu, halafu unasema wamachinga wanatumika na nani? Hili haliitaji PHD kuelewa.
   
 15. m

  mgosiwakaya Member

  #15
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nahisi una maana ya wabunge...yani pamoja na ignorane yako still unaishabikia ccm nani anakujua pale...watu kama nyie, you dont deserve to live in the world! to hell with you!
   
 16. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #16
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa kunipa moyo kwamba mada yangu imeeleweka vizuri, ni ukweli usiopingika jambo hili lilikuwa linanikera sana na kuona jinsi watu wanapandikiziwa uongo mchana kweupe kabisa.
   
 17. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #17
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hoja nzito anajibu kwa majibu mepesi yasiyo na logic kabisa. Hafanyi hata utafiti kidogo kuona kinachoondelea. Binafsi naamini katika kufanya uchunguzi binafsi kwani mwisho wa siku kama umekosea utakosolewa na kubaki na faida ya kuelewa hali halisi.
   
 18. JOASH MUSSA

  JOASH MUSSA JF-Expert Member

  #18
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Soma vizuri, stori imekamilika kama unajua kusoma fanya summary mwenyewe au upo cafe?
   
 19. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #19
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Usisangae ndiyo baadhi ya member walivyo.
   
 20. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #20
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Naona umemnyooshea mkuu, majibu mepesi kabisa haya, hata mleta mada hapati changamoto alizotarajia kuzipata.
   
Loading...