Yanayojiri makabidhiano ya cheti Diamond Jubelee

Yanayojiri makabidhiano ya cheti Diamond Jubelee

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

attachment.php

Habari wakuu,

Baada ya jana kutangazwa Rais mteule wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015, leo mteule anakabidhiwa cheti kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam. Tayari mambo yashaanza na viongozi wote wa kitaifa wapo pia Rais mstaafu wa Nigeria, Goodluck Jonathan.
==========

Kailima(Mkurugenzi wa uchaguzi): Kata 34 hazikufanikiwa kufanya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali, mchakato wa uchaguzi umekamilika tarehe 25 na jana tarehe 29 tumetangaza mshindi. Tume ilikuwa inapokea matokeo na tume ilikuwa inayatangaza kama yanavyopokelewa.

Matokeo ya uchaguzi wa Urais yalipokelewa kutoka majimbo yote 264 na kila chama cha siasa kilipewa fursa ya kuteua mawakala na tume ilivishirikisha vyama vya siasa katika mchakato mzima. Kabla ya kusaini mawakala wa vyama vya siasa walipewa fursa ya kujiridhisha na matokeo ya wagombea wao kwenye ngazi zote.

Mawakala kutosaini hakuzuii tume kumtangaza mshindi, tume iliahidi kufanya uchaguzi wa kisayansi na kuahidi kumtanga Rais ndani ya masaa 72. Tume ilisukumwa lakini tumesimama na kuweza kumtangaza mshindi.

Lubuva: Napenda kutambua uwepo wa Rais mtaafu wa Nigeria ambae alikuwa kiongozi wa waangalizi wa nchi za jumuiya ya madola na wengine(Anawataja). Nawashukuru serikali ya Jamhuri ya muungano jinsi ambayo wametusaidia tangu tumeanza mchakato wa uandikishaji, 2010 wapiga kura walikuwa milioni 8.3 lakini uchaguzi huu walikuwa milioni 15.5, vyama vyote vilitupa ushirikiano mzuri.

Ibara ya 41(1) 47(2)(anavisoma vifungu), Mgombea kiti cha urais akichaguliwa vilevile makamu wa Rais atakuwa amechaguliwa na zoezi la kutangaza lilifanyika jana kutokana na mamlaka tume iliyopewa(Ananukuu kifungu kinachoipa tume mamlaka hayo).

Tume ya taifa ya uchaguzi baada ya kujumlisha kura zote, tulimtangaza Magufuli kuwa mshindi wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya muungano na mheshimiwa Suluhu kuwa makamu wa Rais, vyama nane vilisimamisha wagombea wa kiti cha Urais.

Kwa niaba ya tume ya taifa ya uchaguzi nawakabidhi hati ya kuchaguliwa washindi hivi punde(John Magufuli na Samia Suluhu wapo mbele)

Jaji Lubuva anaisoma hati ilivyoandikwa na anawakabidhi Rais mteule, John Magufuli na Makamu wake, Samia Suluhu. Magufuli anapongezwa na watu mbalimbali ikiwemo Rais anaemaliza muda wake, Rais jakaya Kikwete, first lady mtarajiwa, mama Janeth Magufuli, Waziri mkuu Pinda, mama Anna Makinda na wengineo.

Anna Mgwira: Miaka 54 tunahitaji kuona mabadiliko, ninaamini Rais mteule atayasimamia. Badiliko la kwanza tunataka katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi, tunahitaji usawa kati ya wananawake na wanaume, mabadiliko katika mfumo wa uchumi, nchi yetu ni tajiri.

Aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT-wazalendo,Anna Mghwira aungana na waliokuwa wagombea wenza waliopata nafasi ya kufika katika hafla hiyo ikiwa ni pamoja na mwakilishi wa Hashimu Rungwe kwa niaba ya CHAUMA, Chief Yemba wa ADC waahudhuria sherehe za kumkadidhi cheti cha Ushindi Rais mteuliwa wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli. Hafla hiyo ilizoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kufanyika katika ukumbi wa Diamond JUbilee, Jijini Dar es Salaam.

Mama Anna Mghwira alipewa nafasi ya kuzungumza kwa niaba ya wagombea wanawake waliojitosa katika vinyang'anyiro mbalimbaliya vya nafasi za uwakilishi katika uchaguzi Mkuu mwaka huu.Asimama kwa niaba na kusema baada ya mateso ya miaka 54 ya Tanzania, sasa Tanzania inahitaji kuona mabadiliko. Aongeza kwa kusema ana amani na Rais mteule katika kusimamia na kutenda ayasemayo. Asisitiza mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na uwepo wa mchakato utakaowezesha upatikanaji wa katiba mpya itayotokana na maoni ya wananchi, usawa kati ya wananawake na wanaume na mabadiliko katika mfumo wa uchumi.

Mama Anna Mghwira alimaliza kwa kumkabidhi Rais mteuliwa Ilani ya chama chake (ACT-Wazalendo) na kusema itakuwa vyema endapo serikali inayoingia madarakani itaona vema kuyatendea kazi yalioainishwa katika ilani hiyo kwa ajili ya maendeleo ya Taifa la Tanzania, kitendo hicho chatafsiriwa na kuonekana kitendo cha kiungwana na kishujaa. Wadau wamasuala ya siasa wampongeza.

Attachments

  • Magufuli makabidhiano.jpg
    Magufuli makabidhiano.jpg
    20 KB · Views: 1,694
CCM watimiza rasmi kauli yao ya goli la mkono, hata kushangilia wanaona aibu wamebakia majumbani kwa. Wanamtangaza kwa kumwaga Polisi mitaani kuhofia nguvu ya umma. Asnateni NEC kwa kutuchagulia rais na kubaka democracy.
 
Mkuu, miye naona Tume hawana makosa kwa sababu wao wanasema walikuwa wanatangaza matokeo kama "wanavyoyapokea" kwa maana kwamba hawakufanya edit yoyote tofouti na kujumilisha idadi, kama wametoa idadi ya jumla kuwa tofauti na ile waliyopokea hapo ndo pa kulaum Tume, lakini kama matokeo yalichezewa yakiwa njiani kutoka majomboni kwenda Tume hilo sio kosa la Tume. Aidha, kama yalichezewa wakati wa kuyajumlisha huko majimboni hiyo ni kazi ya mawakala waliowekwa na vyama.
 
Zanzibar ndio imewavua nguo!

Tumebakia kudanganywa na AMANI, eti tutunze amani wakati Gesi anachukuwa mchina, Dhahabu wazungu, Wanyama Waarabu. Watanzania wakitakakujua Rasilimali zao Wapuuzi CCM wanatuambia tutunze AMANI. Amani my asssssssssss. F^%$$# AMANI. Hiyo AMANI ndio itanipa ajira au Elimu? Tumepumbazwa vibaya sana na CCM. CCM wanauza nchi kwa Wageni huku wakituambia tuilinde AMANI na sio Rasilimali zetu.
 
Mkuu, miye naona Tume hawana makosa kwa sababu wao wanasema walikuwa wanatangaza matokeo kama "wanavyoyapokea" kwa maana kwamba hawakufanya edit yoyote tofouti na kujumilisha idadi, kama wametoa idadi ya jumla kuwa tofauti na ile waliyopokea hapo ndo pa kulaum Tume, lakini kama matokeo yalichezewa yakiwa njiani kutoka majomboni kwenda Tume hilo sio kosa la Tume. Aidha, kama yalichezewa wakati wa kuyajumlisha huko majimboni hiyo ni kazi ya mawakala waliowekwa na vyama.

Wasimamizi wa Uchaguzi hawakuwa NEC? au ni CCM? NEC na CCM wamebaka democrasia yetu. Jaji Lubuva alikuwa anajuafika kwamba wanatumikia CCM kwa mwamvuli wa NEC
 
Wewe ni mchohezi unapaswa kukamatwa mara moja!

tumebakia kudanganywa na amani, eti tutunze amani wakati gesi anachukuwa mchina, dhahabu wazungu, wanyama waarabu. Watanzania wakitakakujua rasilimali zao wapuuzi ccm wanatuambia tutunze amani. Amani my asssssssssss. F^%$$# amani. Hiyo amani ndio itanipa ajira au elimu? Tumepumbazwa vibaya sana na ccm. Ccm wanauza nchi kwa wageni huku wakituambia tuilinde amani na sio rasilimali zetu.
 
Si police tu. Hapa Arusha Mkuu wa Wilaya kaleta JWTZ toka Oljoro wako mtaani kudhibiti wanywa viroba. Tia unyayo ubaki Kilema.
 
Wasimamizi wa Uchaguzi hawakuwa NEC? au ni CCM? NEC na CCM wamebaka democrasia yetu. Jaji Lubuva alikuwa anajuafika kwamba wanatumikia CCM kwa mwamvuli wa NEC
Mkuu, ihurumie tume, inafanya kazi katika mazingira magumu. Haina watumishi katika ngazi za majimbo, uchaguzi unasimamiwa na Wakurugenzi wa Halmashuairi amboa unawafahamu vizuri, aidha, ngazi ya madiwani unafahamu Bosi wa uchaguzi katika ngazi hiyo ni nani.
 
Jamani mbona hakuna kiongozi hata mmoja kutoka zanzibar kwenye sherehe ya kukabidhiwa cheti ya magufuli na suluhu?
 
Mkuu, miye naona Tume hawana makosa kwa sababu wao wanasema walikuwa wanatangaza matokeo kama "wanavyoyapokea" kwa maana kwamba hawakufanya edit yoyote tofouti na kujumilisha idadi, kama wametoa idadi ya jumla kuwa tofauti na ile waliyopokea hapo ndo pa kulaum Tume, lakini kama matokeo yalichezewa yakiwa njiani kutoka majomboni kwenda Tume hilo sio kosa la Tume. Aidha, kama yalichezewa wakati wa kuyajumlisha huko majimboni hiyo ni kazi ya mawakala waliowekwa na vyama.
Sawa lakini ilipoambiwa unachosoma sicho halisi ni hiki je ilitaka kusikiliza?
 
Naona watu wameshindwa kupiga makofi mgombea wa ACT alipoomba katiba mpya iliyotokana na maoni ya wananchi
 
Tetetetetetet hiyo Hati iliandaliwa lini Pamoja na hiyo sherehe ya kukabidhi, kweli Wana haraka
 
Back
Top Bottom