Blessed Tajiri
JF-Expert Member
- Dec 16, 2023
- 221
- 659
Leo ni wakati mwingine tena wa kusikiliza kesi zinanzomkabilo Tundu Lissu.
Nini kitajiri, tutarajie kusikia habari mpya ya Lissu kuachiwa?
Wacha tuone nini kitajiri.
====================================
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi za jinai zinazomkabili ikiwemo kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni.
Lissu ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa International Democrat Union (IDU) anakabiliwa na kesi mbili mbele ya Mahakimu wawili tofauti.
Makama Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche alivyotinga kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu.
Ulinzi mkali umetawala katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati wa kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu
Askofu Mwamakula akiongoza maombi ndani ya chumba cha Mahakama
==========================================
Kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi Juni 16, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mahakama imempa onyo kali kwa kutamka kauli ya "No reform, no election" bila ruhusa akiwa ukumbini, ikitafsiriwa kama dharau kwa Mahakama.
Lissu anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi Aprili 3, 2025 jijini Dar es Salaam, akihamasisha kuzuia Uchaguzi Mkuu wa 2025 na kumshinikiza kiongozi wa serikali.