Yanayojiri bungeni Dodoma leo 08 Julai 2015

Yanayojiri bungeni Dodoma leo 08 Julai 2015

Wanawake wanapenda sana kutafuta umaarufu kwa gharama yoyote ile, wako radhi wapate "kiatu cha baniani" wakati wanasema ni mbaya!Ona hata Anna Kilango alivyo acha kutumia jina la husband wake wa kwanza akachukua la John Jumanne! Winnie wa South naye Kang'ang'ania la Madiba mpaka kesho. Graca yeye pamoja na kuolewa na Madiba lakini la kakomaa na la Samora kwa vile alikufa kishujaa.
Hahaa unawachokoza wanawake!
 
Wamwshindwa kuweka mpango mathubuti ya kukusanya kodi toka kwa wafanyabiashara ambao ndio wenye kipato kikubwa,serikali yetu imekuwa ikiwagandamiza wafanyakazi zaidi kwa sababu wanakatwa toka kwenye source na hawana uwezo wa kutoa rushwa ili kodi ipunguzwe. Walichotakiwa kufanya ni kuweka mpango ulio bora na watoe elimu kwa umma na wasimamie kodi katika kuleta maendeleo na pia wapunguze warsha,semina na safari zisizokuwa na tija kwa taifa kuliko kujipangia posho ovyo ovyo na hiki ndo kinasababisha wafanya biashara kupiga dili na wafanya kazi wa TRA. Wafanyakazi hawana uwezo wa kugomea kodi lakini wananyonywa mno na serikali na hawana la kufanya. Kodi ni sawa kabisa kwa mfanyakazi kukatwa lakini si kwa kiwango hicho,mafanyakazi wa Tanzania mwenye Gross salary ya 6,000,000/=, kodi anayolipa kwa mwezi ni kodi inayolipwa na mfanya biashara mwenye mtaji wa milioni zaidi ya 100 kwa mwaka!

Wafanyakazi hawajielewi ila siku wakitoka usingizini watasema NO!!!
 
  • Thanks
Reactions: WCM
Akijibu swali Bungeni kuhusu kupunguza kodi ya mapato kwa wafanyakaza(PAYE),naibu waziri wa fedha,Adam Malima, amesema serikali itaendelea na mpango wa kupunguza kodi hiyo kwa awamu kwani kupunguza kodi hiyo kwa asilimia moja tu inapunguza mapato ya serikali kwa kiasi cha shilingi bilioni 21.

hawa dawa yao inachemka kaka,ni kupiga mkasi tu tarehe 25,za kupora na kuficha ughaibuni wanazo,kupunguza kodi wanajiuliza.
 
Kwani wabunge wa Ukawa wana mgomo wa kutoingia vikao vya bunge?nachojua mimi ni kuwa hao ambao hawapo wamesimamishwa na kwa vikao vitano sasa kama leticia hajasimamishwa kwann asihudhurie?
Napita tu
Wewe hujui linaloendelea endeleeni na mchakato wenu wa kukatana majina
 
Nimemsikia pia Machemli Mbunge wa Ukerewe akiuliza swali redioni sasa sijafahamu kama na yeye yupo au ni swali lililoandikwa miezi iliyopita na leo limewasilishwa tu. Naomba mnijuze
 
Hivi huyu Leticia Nyerere uwa wana undugu na Yericko Nyerere kuna sehemu nilisoma Yericko akimuita shangazi.

Nakala; FaizaFoxy.
 
Last edited by a moderator:
Akijibu mwongozo ulioombwa na Dr. Hamis Kigwangala kuhusu minong'ono iliyozagaa hapo bungeni kwa kutokuwepo kwa wabunge wa upinzani wakati wa kufungwa kwa Bunge hilo.

Mh. M/kiti wa bunge Zungu amesema wao wanaendelea kufanya juhudi kubwa kuhakikisha wanafanikisha hilo.

Awali Kigwangala aliomba kuitishwa kwa kamati ya uongozi kuangalia jinsi ya kuepukana na iabu ambayo inaweza kulikuta Bunge hiyo kesho.
 
Mbunge wa Nzega,Hamisi Kigwangala, ameomba muongozo wa kiti kuwa kuna minong'ono (hakuitaja) inaendelea humu Bungeni na hivyo ni bora ikafanyiwa kazi-akapendekeza kikao cha kamati ya uongozi kiitishwe- ili kesho wakati Bunge linavunjwa wasipate aibu!

Akijibu muongozo huo,mwenyekiti wa Bunge,Azan Zungu, amesema kuwa na hapa namnukuu, "nimekuelewa vizuri sana na nitatoa muongozo leo saa saba mchana".Huenda sijamnukuu kwa usahihi ila kwa ujumla hilo ndio jibu la mwenyekiti wa Bunge.

Je,ni minong'ono gani hiyo na inahusu nini?
 
Wamwshindwa kuweka mpango mathubuti ya kukusanya kodi toka kwa wafanyabiashara ambao ndio wenye kipato kikubwa,serikali yetu imekuwa ikiwagandamiza wafanyakazi zaidi kwa sababu wanakatwa toka kwenye source na hawana uwezo wa kutoa rushwa ili kodi ipunguzwe. Walichotakiwa kufanya ni kuweka mpango ulio bora na watoe elimu kwa umma na wasimamie kodi katika kuleta maendeleo na pia wapunguze warsha,semina na safari zisizokuwa na tija kwa taifa kuliko kujipangia posho ovyo ovyo na hiki ndo kinasababisha wafanya biashara kupiga dili na wafanya kazi wa TRA. Wafanyakazi hawana uwezo wa kugomea kodi lakini wananyonywa mno na serikali na hawana la kufanya. Kodi ni sawa kabisa kwa mfanyakazi kukatwa lakini si kwa kiwango hicho,mafanyakazi wa Tanzania mwenye Gross salary ya 6,000,000/=, kodi anayolipa kwa mwezi ni kodi inayolipwa na mfanya biashara mwenye mtaji wa milioni zaidi ya 100 kwa mwaka!

Wafanyakazi hawajielewi ila siku wakitoka usingizini watasema NO!!!

kunamfanyakazi kila mwezi anakatwa 400000/= ni hatari ccm.tukutane oktober
 
Laigwanan kuasi? Hata mwenyekiti naye timu laigwanan.
Au UKAWA wana mbinu mbadala nje ya bunge?
Tusubiri tuone.
 
Habari! naangalia Bunge sasa nimekuwa suprize kumuona Mh. Mbunge huyu wa CHADEMA

Kulikoni wakuu? Kwani amejitoa CHADEMA tayali? na tena kauliza swali la nyongeza.

Teh Teh UKAWA kwisha kazi....
 
Hivi kodi inayopotea kutokana na makampuni ya simu na madini kutosajiliwa katika soko la hisa zisingewza kufidia pengo hili na chenji ikabaki?
Mbali na makampuni ya simu, kwani serikali ikiamua kukata 20% tu ya matumizi ya magari (V8's) si itaokoa mara hamsini zaidi ya hizi!? (Kumbuka kuna ripoti ilisema magari tu yanatumia trillion 5). Alafu anavyoongea utadhani yeye sio mfanyakazi wa serikali na hiyo kodi haimhusu!
Ni bora kuwa na mawaziri kwa profile zao kama rasimu ya Warioba inavyotaka badala ya hizi nafasi kutumiwa kuzawadiwa na kuponya magomvi ya familia.

Aa! kumbejina hata mbuzi analo! ulitegemea nini kama hajapata adhabu yeye atoke kwa adhabu ya wengine? yamepitishwa mangapi wakiwamo! kulikuwa na kosoro ip ktk muswada ule kupelekea wao kugoma, kilajambo lazima upinge hatakama jema kwa wananchi!

Sikulaumu kwani najua CEO bado hajatoa tamko la msimamo wa chama
 
Back
Top Bottom