Juzinkati hapa kulikuwa na taarifa kuhusu viongozi wa chadema mkoa wa tabora kuvuliwa uanachama.
leo bungeni mh. Halima mdee mbunge makini na wa muda mrefu, ameweka wazi kuwa mh leticia nyerere (akimtaja kwa jina) sio mpinzani na kama anaona serikali imempendeza sana aachane na ubunge wa chadema aende kwa rais amuombe ubunge wa kuteuliwa na rais kwamba katika zile nafasi mbili za uteuzi alizobaki naZo rais amteue leticia..mdee amesisitiza kuwa huo ndio msimamo wa kambi ya upinzani.
kauli nzito kama hii kutolewa bungeni na mbunge wa upinzani dhidi ya mpinzani mwenzake ni dhahiri kuwa hali ya mambo ndani ya chadema si shwari, mficha uchi hazai, chadema kuna kirusi..
my take: tunajenga nyumba moja,kwanini tunagombania fito??