Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatano tarehe 18 Juni, 2014

Yanayojiri bungeni Dodoma: Jumatano tarehe 18 Juni, 2014

wabungenjaa

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
1,782
Reaction score
337
Amani iwe na nanyi wana jukwaa hili maarufu afrika mashariki na kati na dunia kwa ujumla.

leo tena tunaendelea kufuatilia vikao vya bunge la bajeti linaloendelea jijini dodoma.
bunge limeshaanza ambapo kwa orodha ya shughuli za leo inaonyesha ifuatavyo:
1. Maswali toka kwa wabunge kwa serikali.
2.majadiliano ya hotuba ya bajeti ya serikali

higi sasa kipindi cha maswali na majibu yameshaanza na swali la kwanza liliulizwa na joshua nasari kwenda kwa waairi wa mali asili na utalii......
===majibu ya waziri yanaonekana hayakidhi viwango hivyo kuna maswali mawili ya nyongeza yameulizwa kwake....
fuatilia uzinhuu kwa updates.

===updates
swali la pili limeulizwa kwa wizara ya ujenzi na mh gaudence kayombo,
kwamba je ni lini serikali itajenga barabara ya kitai hadi ruanda hadi lituhi kwa kiwango cha lami ili kuwanusuru wananchi na vumbi linalotokana na usafirishaji wa makaa ya mawe? WaZiri anajibu kwamba fedha zimetengwa katika bajeti ya mwaka huu kujenga barabara hiyo na zoezi hilo litafanyika kwa awamu.
===mh ahmed salum anamuuliza waziri wa ujenzi....nyumba zote ktk barabara ya kutoka buguruni hadi lumumba dsm zimewekwa alama ya x ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo, je wenye nyumba hizo watalipwa fidia??
WaZiri anasema waliowekewa x nyekundu wameingia kwenye hifadhibya barabara na hawatalipwa ila waliowekewa x ya kijani watalipwa.

==== cesilia paresso anamuuliza waziri wa fedha...serikali ilikuwa na upungufu wa kibajeti sh 846.9 bilioni ktk robo ya tatunya mwaka huku deni la taifa linaongezeka kila uchao...serikali inasema nini kuhusu hili? Kwann serikali inategemea mikopo ya nje zaidi kwenye bajeti yake?? Waziri anafafanua kwa umakini mkubwa....kwamba deni la taifa linatokana na nchi kukopa na kuelekeza fedha hizo kwenye miradi mikubwa ya maendeleo kama vile kutandaza bomba la gesi kutoka mtwara to dar.
===mary chatanda anamuuliza waziri wa fedha kwamba kuna baadhi ya malori makubwa yanayofanya safari kati ya tz,malawi zambia kukwepa kodi kwa kulipia bima bandia.
je serikali inavhukua hatua gani? Hatua gani zinafhukuliwa kwa kampuni za bima?......,waziri anajibu kwamba yapo makampuni 40 ya bima yamefungiwa pamoja na kuwakamata wenye magari ambao magari yao yamekamatwa na nyaraka bandia za kodi..anakemea udanganyifu huo mbaya.

====swali linaulizwa na mh augostino masele kwa waziri wa mambo ya ndani..
kuna malalamiko kutoka kwa wakuu wa polisi wa wilaya kukosa mafuta, je serikali itaanza lini kuwapatia wakuu hao wa polisi mafuta moja kwa moja pamoja na vifaa vingine vya kutendea kazi?

===mh faustine ndugulile anamuuliza waziri wa mambo ya ndani....jimbo la kigamboni lina vituo viwili vya polisi ie mbagala na kigamboni lakini vituo hivyo vimechakaa kweli kweli huku kukiwa na uhaba wa vitendea kazi...serikali hailioni hili? Waziri anafafanua.
===mh dickson kilufi anamuuliza waziri wa nishati na madini...ni lini umeme utasambazwa kwenye kata za madibira,miyombweni,mapuguro na vijiji vya uturo,ukwama,itamba na maeneo yote ya jirani?
waziri anasema utekelezaji umeanza februari na unaendelea hivi sasa na vijiji vya usangu, kata ya mchongole wameshaunganishiwa...kwa mwaka 2014 si vijiji vyote vitapata umeme kwani utekelezaji huo unafanyika nchi nzima.

esther matiko anauliza swali la nyongeza...kwanini serikali isipeleke umeme kwenye shule zote za sekondari nchini pamoja na vituo vya afya? Waziri anasema upo mpango wa kuweka sola
===mh neema mgaya anauliza, je ni lini serikali itaanza mradi wa kufua umeme wa maji ya mto tumakalya na ruhudji
waziri anasema tr 21 mach mwaka huu imesaini mkataba wa kufua umeme wa mto ruhudji, yupo mwekezaji mwingine kutoka china ambaye si mda ataanza kuweka mitambo...city group naye alienda kuwekeza kwenye mradi huo lakini bado hakujawa na mafanikio ya kuridhisha.

=====updates
mh rabeca mngodo anaomba mwongozo kuhusu majibu yasiyoridhisha ya waziri wa maliasili na utalii
kwamba hakuna utafiti wa kutosha uliofanyika katika majibu hayo...kwani swala hilo lipo hadi ofisi ya rais...iweje waziri adai kuwa serikali haina mpango wa kurudisha shamba hilo kwa wananchi??? Anaomba waziri afanye utafiti kisha aje na majibu ya kuridhisha.

===mjadala wa bajeti ya serikali umeanza. Na hivi sasa mh .....anachangia
anasema kwamba serikali imekuwa ngumu kutekeleza mapendekezo ya kamati ya bajeti, hali inayopelekea kushindwa kuhimili mambo mbalimbali.
anatetea uvuvi ktk bahari,maziwa na vyanzo vyetu vya maji. Anaongelea uwekezaji hafifu wa kilimo kwenye mazao ya pamba,korosho,.....kwamba hadi sasa ni mwezi wa 8 mkulima bafo ana pamba yake ndani..anaitaka serikali itoe mwongozo ktk hili..vp gov imeshindwa kulipa malimbikizo ya madai ya wafanyakazi yatalipwa.
====mh marry mwanjelwa yeye anatetea wafanyakazi kwamba wasilipe kabisa PAYE iwe kama ni incentive kwao.
-----anashangaa misamaha ya kodi kwa makampuni makubwa nchini, iangaliwe na kila kitu kiwekwe wazi...anazungumzia viwanda,vifufuliwe sasa..pia sekta binafsi imeachwa sana wakati ni mhm sana ktk uchumi wa nchi....amezungumzia ishu ya bomu la ajira kwa vijana kuwa sekta binafsi haijawezeshwa ipadavyo iweze kuwa accomodate vijana.
==kuna huyu mh anayechangia hivi sasa anaitaka serikali iteremshe kodi kwa mfanyakazi hadi 10% badala ya hiki kiasilimia moja moja,hakimsaidii mfanyakazi hata kdg.

===+=+updates
Anaunguruma hamad rashid mohamed....yeye amejikita kwenye suala la uvuvi na melinzilizokamatwa na serikali zinazovua kamba...serikalininapoteza kodi kiasi gani hapa? Tunapoteza resources kiasi gani hapa?? Siunginmkono hoja hii hadi niambiwe ni lini gov itaanza kukusanya mapato kwenye deep sea fishing.
anazungumzia suala la madeni ya serikali...serikali itumie mifuko ya hifadhi za jamii kuwekeza, serikali ibaki na mambo ya utawala tu, kwann research zinazofanywa na wataalam wa serikali yenyewe hazifanyiwi kazi??

===updates
selemani jafo anaishauri serikali kupunguza kodi kwenye mshahara wa mfanyakazi, kwamba 1% ni kiini macho.
---anasema kwanini bandari kavu ya kisarawe haianzi kufanya kazi???? Kwann kuna ugoi goi wa kufanya maamuzi?

===halima mdee
anaanza kwa kusema kuwa yeyey ni mbunge senior hivyo ana uzoefu mkubwa kwa masuala ya nchi.
anasema anaondoa upotoshaji kuwa wapinzani hawalalamiki ila ni kazi yao kuikosoa gov.
==========halima amemlipua mh. Leticia nyerere mbunge mwenzake wa chadema kuwa aache ubunge amuombe jakaya amteue kuwa mbunge wa kuteuliwa na rais, na hiyo ni kaulinna msimamo wa kambi ya upinzani.
===anakazia mchango wa hamad rashid kuhusu kodi kwenye deepsea fishing
===anahoji ni vipi vyanzo vipya vya mapato vimefanyiwa kazi, haoni upya wa mawaZiri waliopo kwani wapo mda mrefu ila hakuna walichokifanya.
===kamati ya chenge haisikilizwi
===fedha zinazotengwa kwa rais kuruka na ndege ni mabilioni lakini kilimo hakina kitu
===tupunguze matumizi kwenye vitu visivyo vya lazima
===waziri wa kilimo analalamika fedha kutengwa kidogo kwenye sekta ya mifugo
===tunapoteza fedha nyingi sana kwenye misamaha ya kodi, pia wafanyabiashara wakubwa na viongoZi wakubwa hawalipi kodi, wakubwa walipe kodi wajichunguze wajitathmini.

---////---updates
juma njwayo sasa...yeye anasikitikia urasimu hasa hii wizara ya fedha, unakuta mtu ameenda kulipa fedha anakuta afisa mhusika hayupo, kila mtu atekeleze wajibu wake ipasavyo.wawekezaji wanatukimbia kwa ulegelege wetu huu.
===inashangaza sana eti soda juice na bia ndio vyanzo vya mapato...

===updates
mchungaji msigwa akitumia ipad.....
anasema haungi hoja mkono
Kwamba yeye binafsi amepeleka magodoro hosp,ujenzi wa machinjio isakamaliwa haujakamilika,bajeti hii haijasema inatekeleza vipi mambo hayo.
==anamshauri mwigulu aende google asome mchango wake wa akili ndogo kutawala akili kubwa
===analalamikia neptisim,undugunisation katika kupeana kazi serikalini kwamba hii ndio sababu kubwa mambo hayaendi
===anasema tuna tatizo la mindset kama taifa
===watu hawataki kuambizana ukweli, bajeti haitekelezeki lakini tunaisifu tuuu, ukiwa na critical mind unaonekaana mkorofi...hv tuna wataalam kweli wanaoweza kutushauri ipasavyo??? Slogan zote za gov zimekwama, watu wanawaza vile vile....change what u see...namuomba speaker tutafute motivational speakers...watu wame stark...tutafute washauri nje ya nchi...iweje rais anatengewa bilions of money kusafiri nje ya nchi wakati kilimo na afya vinatengewa pesa kidogo??? Tumechoka majibu ya kisiasa hapa...

--///---updates
naibu waziri wa afya katka kuweka kumbukumbu sawa amempa taarifa mch.msigwa kuwa bajeti ya wizara ya afya siyo bilioni 46 bali ni trilioni 1.6.
====+++=updates
prof david mwakyusa sasa..anasema tz ni nchi ya 22 ktk nchi maskini duniani, anasema tz siyo nchi maskini bali ni ya nyuma kimaendeleo.
===tofauti ya nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea ni matumizi ya sayansi na technolojia.
===viwanda--tujenge viwanda kuongeza thamani ya uchumi wetu, nchi kama singapore ambayo tulikuwa sawa kimaendeleo hv sasa wao wako juu kiuchumi kwa sababu ya viwanda na exportation
+===kilimo....tunajitapa kuhusu kilimo lakini kilimo chenyewe ni kwa ajili ya kula tu sio biashara, hakina tija. We need mindset change.
==============mh subira mgalu hivi sasa..
anaishukuru gov kwa kuongeza ration allowance kwa wanajeshi na askari
ujenzi wa nyumba za askari, kuboresha miundombinu,...anapigia upatu sheria ya bajeti ila anaona ni vyema tuanze na sheria ya public finance act...kuna maeneo yametumia fedha isivyo kawaida mf balozi zetu. Ile sheria ipitiwe upya then twende kwenye sheria ya bajeti.
anashukuru umeme kufika maeneo mengi ya vijiji vya mkoa wa pwani.
===updates........mh mbunge aliyemaliza kuzungumza hivi punde ameshauri/anaona tatizo la ujangili nchini kuwa ni janga la kitaifa...anaona kuna haja ya serikali kutupia macho eneo hili kwani kuna rasilimali za nchi zinapotea mno kwa ujangili.
===said arfi....anazungumzia bandari ya mtwara kuwa ni bandari ya kimkakati na sio mbegani....anaona ni bora kuboresha bandari ya dsm kuliko kutupa pesa ya nchi mbegani...
==anazungumzia reli kwa kutolea mfano singapore kwamba sekta hii ni mhm sana kwa uchumi wa nchi na kupunguza gharama ya uendesheji...reli na bandari zisipoangaliwa hatuwezi kwenda popote
===kuhusu bajeti sasa anazungumzia fedha za maendeleo kwenye wizara mbalimbali
==anasema ukizingatia maoni ya kamati ya bajeti, bajeti hii haitekelezeki hata kidogo, wabunge tunaikubali kwa sababu tukiikataa bunge linavunjwa na hatutaki kwenda kwenye uchaguzi hivi sasa
===anashangaa serikali kuanzisha big result now iliyoishia kupoteza mamilioni ya shilingi za walipa kodi akati kuna mamlaka zinazohusiana na hiyo kiutendaji

===updates...sylvester mabumba..anasema anashangaa kuambiwa uchumi unakua huku maisha ya watz yanazidi kuwa magumu..anaangalia tatizo la ajira kwamba gijana hawana ajira,wanateseka,wanasoma lakini hawapati kazi,hapa uchumi umekuaje?
==========updates
====willium ngeleja hv sasa...anasema wanaopinga takwimu kuwa umaskini wa nchi unapungua wapinge hoja hiyo kwa takwimu..kwamba takwimu zinapingwa kwa takwimu...anasema taifa linatembea, wastani wa kuishi mtz umeongezeka hadi miaka 61..kwa ukuaji wa uchumi tz ni nchi ya 8 ktk nchi za kusini mwa jangwa la sahara.
===anapingana na madai kuwa serikali ya tz haisikii...anasema kuna mambo makubwa yamefanyika nchini mf.ujenzi wa chuo kikuu cha udom,bomba la gesi kutoka mtwara hd dsm, mradi mkubwa wa mchuchuma liganga,mradi mkubwa wa kusambaZa umeme vijijini ambapo leo 36% ya wananchi wanapata umeme vijijini.
===mchungaji israel natse....anaanza na deni la taifa...kwamba isingekuwa hofu ya wabunge wa ccm bunge kuvunjwa, kwa taarifa hii ya kamati ilifaa bunge livunjwe...deni limefika trilioni 36, anahoji tutazidi kuwa tegemezi hadi lini?
===udhaifu mkubwa wa serikali unatufanya tunakopa kwa hasara, bunge lichukue nafasi yake kwamba mikopo mikubwa ya nchi mikataba yake iidhinishwe na bunge
---\\|_==ukuaji wa uchumi....hauna uhusiano na maisha halisi ya watz
===pAYE iwe single digit..ili kuwasaidia wafanyakazi
=======mh omary nundu anawatetea wafanyakazi kuwa wanakatwa kodi kubwa mno.ipunguzwe hadi asilimia 10
====anawatetea wafanyabiashara wadogo wadogo kuwa watengenezewe mazingira bora ya kufanya kazi zao

 
endelea kutupa updates.....


Maoni ya Anne Kilango kuhusu Haki miliki ya Mount Kilimanjaro.

Mama Kilango aipigania Tanzania kuhusu Mlima Kilimanjaro.

Leo asubuhi akiwa anauliza swali kuhusu suala la ndege za kampuni ya Kenya Airways kuweka nembo ya Mlima Kilimanjaro katika ndege zake,mbunge wa Same Mashariki kupitia Ccm amekumbana na majibu ya kusikitisha kuhusu suala hili.

Mama Kilango aliuliza uhalali wa nchi ya Kenya kutumia ndege zake kuutangaza mlima wa Kilimanjaro kuwa ni kivutio cha utalii kilichopo nchini mwao.

Mama Kilango alipata kiini cha kuuliza swali hili baada ya mmoja wa wanajukwaa la Friends Of Hon.Membe kuweka picha ya moja ya ndege za Kenya Airways zikiwa na aina ya tangazo linalolalamikiwa na Mama Kilango.

Ag Werema kamjibu vibaya Mama Kilango.Anasema sio kosa kwa kinachofanywa na Kenya.Waziri wa Maliasili na Utalii naye kakaa kimya pamoja na kwamba Mama Kilango alimwomba atoe kauli.

Ukimya wa serikali na majibu ya Ag Werema hayana tofauti na mtu limbukeni wa taaluma aliyonayo.Ni aibu kwa mtu msomi asiyeelewa madhara ya mtu kutumia trade mark ya mwingine bila idhini yake.Hata kisheria sio sahihi!

Ag Werema anapotosha ukweli.Ila sisi ndio wenye sio yeye.Mama Kilango katusemea Bungeni,ni jukumu letu kumpigania mitaani hadi serikali ielewe.

Kwasababu hii sio haki kwa nchi yetu.Ukimya wa serikali na majibu yake mepesi ni msumari wa moto kwa maendeleo ya nchi yetu.Tunapaswa tulipwe fidia kwa kitendo kinachofanywa na Kenya.Tunaonekana hatupo serious na rasilimali zetu!
 
Tunataka elimu bora, huduma bora za afya, barabara na maji safi na salama
 
Tunataka elimu bora, huduma bora za afya, barabara na maji safi na salama

Unamwambia nani sasa?
miaka 50 mmeshindwa kufanya hayo,tena ni mambo madogo kabisa, sijui lipi mnaweza?
 
Unamwambia nani sasa?
miaka 50 mmeshindwa kufanya hayo,tena ni mambo madogo kabisa, sijui lipi mnaweza?
Wewe umeweza nini zaidi ya kuitia hasara dunia unakula kunywa na kuvuta hewa ya mungu bure
 
Huyo kiherehere Leticia Nyerere kama anataka aende kujipendekeza kwa Kikwete apewe viti maalumu vya rais.Hatuwezi kuvumilia mbunge hovyo kama huyu aendelee kuwa kambi ya upinzani.Kazi ya wabunge na hasa wa upinzani sio kuiimbia serikali nyimbo za kusifu na kuabudu.
Kama haondolewi mara moja nitakuja Dodoma.
 
ccm ni chama chakavu hawana jipya hawa wahuni ccm
 
Hongera zake, amesemaje?? Mana sisi wengine tuko mashambani huku
cc
mleta mada
 
ameongea ukweli ccm chama chakavu hawana jipya hata kwenye wanapinga
 
Huyo kiherehere Leticia Nyerere kama anataka aende kujipendekeza kwa Kikwete apewe viti maalumu vya rais.Hatuwezi kuvumilia mbunge hovyo kama huyu aendelee kuwa kambi ya upinzani.Kazi ya wabunge na hasa wa upinzani sio kuiimbia serikali nyimbo za kusifu na kuabudu.
Kama haondolewi mara moja nitakuja Dodoma.

Wivu tu umemjaa halima,kama ccm imefanya vizur lazima isifiwe panaoo stahili.tatizo halima anataka mipasho tu
 
Back
Top Bottom