Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumanne, Trh 15 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima kwa sura ya 1 & 6

Sugu naona haelewi tofauti ya mwanajeshi kutawala nchi nchi kutawaliwa kijeshi. Dah wadau, imekaa vipi hii? Ni kweli kwamba hajui au anajua ila ameamua kuongeza hivyo kwa malengo fulani.
 
Akichangia bungeni amesema huwa wanataniana na Mwigulu, akasema yeye anaitwa Mzee wa maandamano na yeye humuita gaidi mzee wa utekaji!

My take: Kumbe Mwigulu anakubaliana na ugaidi? Mbona hakuwahi kumshitaki Sugu?
 
Walidhani wanaweza kabisa kutumia usanii kufanya usanii kama walivyozoea, sasa mambo yametibuka - nafikiri wanajilaumu sana kuuanzisha mchakato huu - walikuwa na uwezo kabisa wa kusema tunaendelea na mfumo wetu wa sasa na hakuna mtu angewafanya chochote mbali na kuishia kulaumu tu.

Kudhani kuiua hoja ya CDM kuhusu katiba mpya kwa kuwapatia wananchi katiba feki - umeshindikana. sasa mengi yanafumuka ngoja tusubiri.
 
Joseph Mbilinyi anasema:
Naunga mkono serikali tatu kama ilivyo letwa na Tume ya katiba. kwa hiyo tunaunga mkono maoni ya wananchi.

Aliye haribu huuu mchakato ni Rais aliyekuja kuelezea msimamo wa chama chake baadala ya kuzindua bunge.
Hiki ni kipindi cha kwaresma acheni unafiki. Tumeharibu pesa nyingi. CCM wamehishiwa mikakati wameanzisha mkakati wa kuzomea. Mwingulu anataka serikali moja lakini anaogopa kusema. Tuko kwenye nafasi nzuri sana la kujadili hili swala la sivyo tutalijadili kwa kulazimishwa.

Leo lukuvi anatutishia nchi itatawaliwa na jeshi vizuri. mbona rais wetu alikua mwanajeshi na anatuongoza? wanajeshi ni ndugu zetu, wakitawala kuna tatizo gani?

Serikali tatu ni tija. kila chenye gharama kina faida. Mara nyingi viongozi wa dini wanakosea wanapokua upande wa dola dhidi ya wananchi. Mfano rwanda. Unapo pima maralia inapimwa kwenye kidole sio mwili mzima acheni kuzingua eti walio hojiwa ni wachache.
 
Sugu: mbona hamsemi Znz tunawalipia umeme, fenicha zinabadilishwa kila siku mnasema gharama s3 against nini?
 
Sugu: Unapopima malaria au UKIMWI hauchukui damu lita tano. Unachukua kwenye kidole tu lakini ugonjwa unakuwa mwili mzima
 
Sugu anatia huruma, bendera fuata upepo kuna sehemu nilisema wanatumiwa na PK taratibu wanajidhihirisha
 
Nimeipenda hii conclusio ya Mbilinyi. Safi huko mbele tutagawana nyama na damu za watanzania ni bora matakwa ya wananchi kuzingatiwa katika mchakato huu.
 
Hivi ni kweli Seif Sharifu alimsaliti Abdul Jumbe? Ni kweli kuwa ndiye aliyemtonya Nyerere? Kama ndivyo, yuko sahihi Zitto Z Kabwe kuwa tusiwaamini wanasiasa?? Naomba kwa mwenye taarifa na ushahidi juu ya hili auweke wazi hapa,,,,sababu iko haja ya kurijiridhisha.

Muombe Nape minutes za mkutano wa halmashauri kuu ya taifa ya ccm uliomvua madaraka Aboud Jumbe pale CBE Dodoma mwaka wa 1984 atakupatia na utajionea mwenyewe kilichojiri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom